TOKA KATIKA NYUMBA ZA MAKAHABA

  Kanisa, Uncategorized

Biblia inasema katika 

Yeremia 5:7  Nawezaje kukusamehe? Watoto wako wameniacha mimi, na kuapa kwa hao ambao si miungu; nilipokuwa nimewashibisha chakula, walizini, WAKAKUTANA WENGI PAMOJA KATIKA NYUMBA ZA MAKAHABA.

Ukiona kanisa lako lina sifa fuatazo basi tambua kuwa, hilo sio kanisa bali ni nyumba ya makahaba ambayo mnakutana pamoja na kufanya ukahaba huko.


1 Uvaaji wa mavazi ya kikahaba kwa wanawake.

Mithali 7:10 Na tazama, mwanamke akamkuta, ANA MAVAZI YA KIKAHABA, mwerevu wa moyo; 

Ukiona kanisa lako linaruhusu wanawake kuvaa mavazi ya kikahaba, ambayo hayana utofauti na yale yanayovaliwa na makahaba na kufanya ukahaba, toka katika hilo kanisa.


Mavazi yote ya vimini kwa mwanamke (nguo fupi), suruali zote kwa wanawake, nguo za nusu uchi, nguo zote zinazoonesha maungo ya mwanamke kama mapaja, kifua (maziwa), mavazi ambayo yanayotamanisha wanaume na yanayochochea uzinzi na uasherati ni mavazi ya kikahaba, na kila mwanamke anayevaa hayo ni kahaba kwani hana tofauti na makahaba, (haijalishi yeye ni nani). 

Hivyo, kama kanisa lako linaruhusu hivyo vitu unapaswa utoke hapo haraka kwani hiyo ni nyumba ya Makahaba.


2 Mapambo kwa wanawake.

Kama Kanisa lako linaruhusu mapambo kwa wanawake kama vile, kucha bandia, kupaka rangi kucha, nywele bandia na mawigi, hereni puani na masikioni, kwenye ulimi, make ups n.k ni nyumba ya makahaba na kusanyiko la makahaba hilo toka huko. Mama wa makahaba ndio kapambwa kwa hivyo vitu (ufunuo 17), na wanawake makahaba kama Yereberi ndio walifanya hivyo vitu3 Kusujudia miti (masanamu) na mawe.

Huu ni ukahaba na uzinzi wa kiroho. Kama kanisa lako linachonga mti au jiwe, na kulipamba kwa rangi na dhahabu, na kuliweka nje ya kanisa au ndani ya kanisa, na kuambiwa kuliinamia, kulibusu na kuliomba, basi tambua kuwa hilo sio kanisa bali ni nyumba ya makahaba, na wewe mwenyewe unayebusu na kuliomba  hilo sanamu la mti au jiwe unafanya ukahaba. Na haya ni masanamu yote ya miungu wake, masanamu ya Yesu, Mariamu, masanamu ya Yosefu, masanamu ya mabudha na masanamu yote yenye mikono kumi kumi. toka kati hiyo nyumba ya ukahaba kwani waabudu sananamu wote hawana sehemu katika ufalme wa Mungu

1 Wakorinto 6:9 Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, WALA WAABUDU SANAMU, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, 

Hivyo toka katika hiyo nyumba ya makahaba na acha kufanya ukahaba.

Bwana akubariki, Shalom.


Mada zinginezo:

SANAMU ZISIZONENA


IKIMBIENI IBADA YA SANAMU.


Je! Ni dhambi kwa mwanamke wa Kikristo kuvaa suruali?


Je! Binti kujipamba mwili wake si ni jambo jema kwani atakua analipamba hekalu la Mungu?


Kuuza cheni na hereni ni sawa kwa Mkristo?

LEAVE A COMMENT