1 Wakorinto 3:16 Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?
SWALI: Maandiko yanasema kuwa, miili yetu ni hekalu la Mungu wa Mbinguni aliye hai, sasa kama mwili wangu ni hekalu la Mungu si ninatakiwa nilipendezeshe hekalu la Mungu kwa kujipamba (kupaka make up na wanja) kama mfalme sulemani alivyolipamba hekalu la Mungu?
JIBU: ni kweli maandiko yanasema kuwa mtu aliyeamini na kubatizwa katika ubatizo sahihi mwili wake unakua ni hekalu la Mungu, lakini ni dhambi kujipamba kwa kujipaka make up na wanja kwasababu Mungu ametuumba kwa jinsi ya ajabu sana na kama angetaka kutuumba na make up na wanja wala asingeshimdwa
Zaburi 139:14 Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa Kwa jinsi ya ajabu ya kutisha. Matendo yako ni ya ajabu, Na nafsi yangu yajua sana,
Umeona hapo? Kwanza unapaswa ushukuru kwa hivyo ulivyoubwa kwani umeumbwa kwa jinsi ya ajabu sana dada yangu wala huna haja ya kupaka ma-lipstick na ma-make up, hivyo kufanya hivyo utakua unamwambia Mungu kuwa amekosea kukumba kwasababu alisahau kukoleza rangi ya midomo yako, alisahau kukoleza rangi ya nyusi zako na hata hiyo rangi ya ngozi yako alikosea kukupa. Sasa kama utafanya hivyo basi fahamu kuwa unashindana na muumba wako dada yangu na kitu kimoja tu kitakupata soma
Isaya 45:9 Ole wake ashindanaye na Muumba wake! Kigae kimoja katika vigae vya dunia! Je! Udongo umwambie yeye aufinyangaye; Unafanya nini? Au kazi yako, Hana mikono?
Sasa maandiko yanakwambia OLE wewe unayeshindana na muumba wako, wewe umwambie Mungu kuwa hii rangi ulikosea kunipa kwahiyo mimi naenda kujichubua au naweka make up, acha mara moja hiyo tabia dada yangu.
Lakini sasa huu utamaduni wa kujipamba na kujipaka wanja ulitokea wapi? Ukisoma maandiko utaona kuwa kulikuwa na mtu mmoja ambaye alifanya hayo mambo na mtu huyo alikua akiitwa Yezeberi na pia maandiko yanasema kuwa alikuwa ni mzinzi japokua alikua ni malkia na alikua ni mchawai pia.
2 Wafalme 9:22 Ikawa, Yoramu alipomwona Yehu, akasema, Je! Ni amani, Yehu? Akajibu, Amani gani, maadamu uzinzi wa mama yako Yezebeli na uchawi wake ni mwingi?
Soma tena
2 Wafalme 9:30 Hata Yehu alipofika Yezreeli, Yezebeli akapata habari; akatia uwanja machoni mwake, akapamba kichwa chake, akachungulia dirishani.
Unaona hapo? Sasa unaweza kujiuliza kwanini baada ya Yezebeli kupata taarifa kuwa Yehu anakuja, akaenda kujipamba kwa kujipaka wanja na nywele zake? Lengo ni ili kumvutia Yehu kwani alikua ni mzinzi kama maandiko yanavyosema, sasa wewe dada yangu unayepaka hivyo vitu fahamu kuwa hizo ni tabia za huyu yezebeli za kutaka kuwavutia watu, unachochea uzinzi kama ufahamu wala usijidanganye kuwa unapamba hekalu la Mungu ni uongo.
Na hayo mafundisho yake ndio hayo ya wanawake kujipamba nyuso zao na Bwana Yesu alishatoa onyo kuwa uyaache hayo mafundisho yake.
Ufunuo 2:20 Lakini nina neno juu yako, ya kwamba wamridhia yule mwanamke Yezebeli, yeye ajiitaye nabii na kuwafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, ili wazini na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu.
Maandiko yanasema “ na kuwafundisha watumishi wangu” kumaanisha kuwa anayomafundisho yake na ndo hayo ya kujipaka marangi usoni na muda wote kuwaza uzinzi, lakini Bwana hakuishia hapo akaendelea na kusema “na kuwapoteza” akimaanisha kuwa hayo mafundisho yake hayaishii hapo tu bali yanapoteza, hivyo dada yangu unayesema kuwa unalipamba hekalu la Mungu fahamu kuwa unajidanganya kwa haya mafundisho ya Yezebeli na unapotea, hivyo acha kama Bwana alivyotoa shauri.
Bwana akubariki. Shalom
Mada zinginezo:
Je! Ni dhambi kwa mwanamke wa Kikristo kuvaa suruali?
JE! MAPAMBO YA VITO NI DHAMBI?
ONDOENI MIUNGU MIGENI ILIYO KWENU.
Kuuza cheni na hereni ni sawa kwa Mkristo?
Asanteni Sana, Mungu Baba AWABARIKI SANA. Nashukuru Sana
assante sana kwa neno