Kivipi tunafarakana na imani kwa kutamani fedha?

  Maswali ya Biblia, Uncategorized

SWALI: Ni kwa namna gani wakristo wengi leo hii tunafarakana na imani kwa kuitamani fedha? (1 Tomotheo 6:10)

1 Timotheo 6:10 Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi. 

JIBU: Shalom, katika mstari huo tunaona kuna vitu viwili vinavyozungumziwa ambavyo ni imani na fedha, sasa imani inayozungumziwa hapo ni imani kwa Bwana wetu na Mungu wetu Yesu Kristo kama tulivyoipokea kutoka kwa manabii na kuletwa kwetu na mitume 

2 Petro 3:2 mpate kuyakumbuka yale maneno yaliyonenwa zamani na manabii watakatifu, na ile amri ya Bwana na Mwokozi iliyoletwa na mitume wenu. 

Sasa lengo na dhumuni la imani hii ni kutupatia sisi wokovu wa roho zetu kama maandiko yanavyosema 

1 Petro 1:9 katika kuupokea mwisho wa imani yenu, yaani, wokovu wa roho zenu. 

Hiyo ndiyo imani inayozungumziwa hapo, sasa imani hii ilivyoletwa ilikua na amri na maagizo ambayo tunayasoma katika maandiko matakatifu yaani biblia. Sasa katika amri hizo na maagizo kuna vitu ambavyo imani hii imesema kuwa tuepukane navyo kwani vitatufarakanisha na imani yetu na hatimaye kupata hasara za roho zetu, sasa vitu hivi ndivyo ambavyo wakristo wengi hawataki kuviacha kwasababu tu vinawapatia fedha na hivyo kufarakanishwa na hii imani.

Wewe mkristo wa leo, ni hizo fedha za rushwa ndizo zinazo kufarakanisha na imani? Acha mara moja kwani utapata hasara ya roho yako ndugu yangu.

Wewe binnti,Ni hiyo fedha unayopata kwa kazi yako inayokulazimu uvae mavazi yasiyokusitiri mwili wako kama vimini suruali n.k ndo inakufanya ufarakane na imani? Acha mara moja kwani utapata hasara ya roho yako 

Ni ni hizo fedha unazopata kwa kuuza mwili wako ndizo zinazokufarakanisha na imani? Acha mara moja kwani utapata hasara ya roho yako. 

Ni hizo fedha unazozipata kwa kucheza kamali kama kubet n.k zinakufarakanisha na imani yako? Acha mara moja usije ukapata hasara ya nafsi yako

Hivyo kazi yoyote au kitu chochote ambacho kitakufarakabisha na imani yako lakini kinakupatia fedha ndio vinavyowafanya wakristo wengi leo hii wafarakane na imani yao. Mpendwa acha hicho kitu au kazi ambayo inakupatia fedha lakini inakufarakanisha na imani yako kwani utapata hasara ya roho yako na hiyo fedha haitakusaidia chochote 

Bwana mwenyewe aliyetuachia imani alisema kuwa

Matayo 16:26 Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake? 

Ilinde hiyo  imani uliyoipokea mara moja tu kwani ndio wokovu wa roho yako wala fedha zisikugombanishe nayo.

Shalom.


Mada zinginezo:

Itakuwa shida tajiri kuingia katika ufalme wa Mbinguni.


TAFUTA PESA!  TAFUTA PESA! 

USIBATILISHE KAZI YA MSALABA WA YESU KWA INJILI ISIYOWEZA KUOKOA ROHO ZA WATU.


Maskini wa roho ni watu wa namna gani?(Mathayo 5:3)


WEWE HU MBALI NA UFALME WA MUNGU.


Je! matumizi ya mimea ya asili kwa matibabu ni dhambi kwa mkristo?

LEAVE A COMMENT