NAO WATAJIEPUSHA WASISIKIE YALIYO KWELI

  Biblia kwa kina, Uncategorized



Biblia inasema…

2 Timotheo 4:3 MAANA UTAKUJA WAKATI WATAKAPOYAKATAA MAFUNDISHO YENYE UZIMA; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti; 

4 NAO WATAJIEPUSHA WASISIKIE YALIYO KWELI , na kuzigeukia hadithi za uongo. P



Biblia ilitabiri kuwa, utafika wakati ambao Wakristo wengi watakapoyakataa (watakaposhindwa kuvumilia na kudumu katika) mafundisho yenye uzima kutokana na tamaa zao wenyewe za kupenda udunia, kama vile, uvaaji vimini, make-ups, unywaji pombe, ibada za sanamu, tamaa za mali, starehe, umaarufu, n.k  kisha kujifanyia waalimu au watumishi watakao wafundisha mambo hayo yasiyo pingana na tamaa zao hizo. Lakini kitu kibaya zaidi ni kuwa, si kuyakataa tu hayo mafundisho yenye uzima, bali, WATAJIEPUSHA KABISA  WASIUSIKIE UKWELI WENYEWE. Hicho kitu ndicho kinachoendelea sasa hivi katika Ukristo, Wakristo wengi leo hii licha ya kuyakataa mafundisho yenye uzima, wanajiepusha kabisa na hawapendi kabisa kuyasikiliza hayo mafundisho yenyewe.


Wakristo wengi leo hii wanajiepusha na hawapendi kusikiliza mafundisho yanayokemea unywaji wa pombe, hivyo kupelekea kufuata tamaa zao za unywaji wa pombe kwa kuwasikiliza watumishi wanao halalisha pombe na kuzibariki kabisa.


Wakristo wengi leo hii wanajiepusha na hawapendi kusikiliza mafundisho yanayokemea maisha yao ya uzinzi wanayoishi na mabinti au wavulana kihorela horela bila kufunga ndoa na kupelekea kwenda kwa watumishi wanaokumbatia huo uovu bila kuwaambia ukweli.


Wakristo wengi leo hii wanajiepusha na hawapendi kisikiliza mafundisho yanayo sisitiza kuwa waombaji kwa kukesha na kumtafuta Mungu kwa bidii, hivyo kupelekea kupenda shoti-kati za haraka haraka za matumizi ya udongo, maji ya upako, na mafuta ili kutatua shida zao.


Wakristo wengi leo hii wanajiepusha na hawapendi kusikiliza mafundisho yanayokemea uvaaji wao usio na maadili kanisani, makazini, majumbani, n.k 


Wakristo wengi leo hii wanajiepusha na hawapendi kusikiliza mafundisho yanayokemea uombaji kwa watu waliokufa kama mtakatifu Yosefu, Teresia, n.k   kwa kisingizio kuwa walizaliwa katika imani hiyo.

Ndugu yangu, hizi ni siku za mwisho, rudi na ugeukie biblia yenye mafundisho ya uzima yaliyohubiriwa na manabii watakatifu na mitume wa Bwana kwa faida na wokovu wa roho yako, mafundisho yoyote yaliyo kinyume na mafundisho ya Kristo na mitume wake kama vile kumwomba Maria, mtakatifu yasinta, ubatizo wa vichanga, unywaji pombe, uvaaji nusu uchi na mapambo kwa wanawake, yapo china ya laana kwa kila ahubiriye na kuhubiriwa kama biblia inavyosema katika…

Wagalatia 1:8 Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe.

 9 Kama tulivyotangulia kusema, na sasa, nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe. 

Hivyo tubu leo dhambi zako na kumpa Yesu Kristo maisha yako na kubatizwa katika ubatizo sahihi kisha kupokea Roho wake Mtakatifu (sawa sawa na matendo 2:38). Bwana anapenda wote tuifikilie toba ili tuwe na uzima wa milele kwa kuyasikiliza mashauri yake, kakini tukiyakataa itakuwa hasara kubwa kwetu.

Mithali 1:23  Geukeni kwa ajili ya maonyo yangu; Tazama, nitawamwagia roho yangu, Na kuwajulisheni maneno yangu.

24 Kwa kuwa nimeita, nanyi mkakataa; Nimeunyosha mkono wangu, asiangalie mtu; 

25 Bali mmebatilisha shauri langu, Wala hamkutaka maonyo yangu; 

26 Mimi nami nitacheka siku ya msiba wenu, Nitadhihaki hofu yenu ifikapo; 


Ikiwa utakuwa na swali lolote kuhusu biblia, basi, wasiliana nasi kwa namba hizi

+255652274252/ +255789001312

Tafadhari washirikishe na wengine ujumbe huu

Bwana akubariki, shalom.



MADA ZINGINEZO:

ITAMBUE NA KUIFANYA HUDUMA YA YOHANA MBATIZAJI  KATIKA UKRISTO WAKO.


KWANINI MNANIITA BWANA, BWANA, WALAKINI HAMYATENDI NISEMAYO?


Ni maneno yapi ya unabii yaliyotangulia juu ya Timotheo? (Kulingana na 1 Timotheo 1:18)


Nilimwona Shetani, akianguka kutoka mbinguni kama umeme.(Luka 10:18)

LEAVE A COMMENT