MADHARA YA KUTOKUSOMA BIBLIA YAKO.

Biblia kwa kina No Comments


Shalom, Bwana Wetu Yesu Kristo apewe sifa milele na milele amina. Karibu katika kujifunza neno la Mungu na tafakari yetu ya leo ina kichwa kinachosema “madhara ya kutosoma biblia zetu”. Tukumbuke kuwa, Mungu alituahidia uzima wa milele katika Yesu Kristo kwa kila atakayeamini na kubatizwa, lakini hiyo pekee haitoshi kwa sisi kuuingia ufalme wa mbinguni kwani kuna taratibu au sheria mbali na kumwamini Kristo, na taratibu yenyewe au sheria yenyewe ni kuyafanya  mapenzi ya Baba yake aliye Mbinguni 


Matayo 7:21 Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; BALI NI YEYE AFANYAYE MAPENZI YA BABA YANGU ALIYE MBINGUNI. 

Hata katika dunia hii ya sasa tunayoishi, unapotaka kuingia nchi nyingine mfano Urusi, kuna unataratibu wake, lakini hata unapotaka kuingia kwenye kazi au ajira fulani au kampuni fulani kuna utaratibu wake ambao upo kwa kila anayetaka kuingia au kujiunga na ajira hiyo au kampuni hiyo, sasa  hivyo ndivyo ilivyo na kwa Mungu wetu pia, kuna utaratibu wake aliouweka kwa wale wanaotaka kuingia katika ufalme wake, na utaratibu huo ni KUTAFANYA MAPENZI YAKE baada ya kumwamini Bwana Yesu kuwa ni Bwana na Mwokozi wa maisha yako na kubatizwa.


Taratibu za kuingia katika nchi fulani au kujiunga na ajira au kampuni fulani unaweza zikuta kwenye mitandao yao husika ya kijamii  na sehemu ambazo wameziahinisha kama vile barozi, mawakala, n.k ila utaratibu au kanuni (mapenzi ya Mungu) yenyewe yapo kwenye maandiko yake matakatifu yaani biblia. Utaratibu mwingine wowote unao dai kujihusisha na ufalme wa Mungu lakini unaotoka nje ya biblia, ni batili na wakufoji ambao lengo lake ni kukupotosha wewe unayetaka kuuingia ufalme wa Mungu. 


Biblia ina utaratibu wote yaani mafundisho yote yatakayomwezesha mwanadamu kuuingia ufalme wa Mungu, lakini cha kushangaza ni kuwa, watu wengi leo hii tunapenda kuuingia huu ufalme lakini taratibu zake hatupendi kuzijua kwa kusoma biblia zetu, hivyo kupelekea madhara mkubwa ambayo ni KUCHUKULIWA NA UPEPO WA MAFUNDISHO YA KILA NAMNA kutoka kwa adui ambayo lengo lake ni kutupoteza, hii ni hatari sana. Wengi wamekumbwa na madhara haya ya kuchukuliwa na mafundisho ya namna nyingine ya kujiepusha na vyakula ambavyo Mungu alivitakasa ili vipokelewe kwa shukrani na wao wenye kuijua kweli, kwa kuto kutaka kusoma neno la Mungu angali biblia imesema tusichukuliwe na mafundisho ya namna hiyo.


Waebrania 13:9  Msichukuliwe na mafundisho ya namna nyingine nyingine, na ya kigeni; maana ni vizuri moyo ufanywe imara kwa neema, wala si kwa vyakula, ambavyo wao waliokwenda navyo hawakupata faida. 


Wimbi kubwa la watu leo hii limechukuliwa na mafundisho ya KUABUDU SANAMU na wanaabudu masanamu pasipo kujua kwa sababu tu hawataki kusoma neno la Mungu yaani biblia ili kupata ufahamu. Ndugu yangu unayefanya hivyo, huo utaratibu ni feki na wakufoji na wala haupo kwenye biblia na chanzo chake ni ibilisi mwenyewe ambaye aliingiza hayo kwa welevu ili kukupa utaratibu bandia wa kumfikia Mungu, na si hilo tu, bali yapo mengi aliyoyaingiza kama vile, kuwaomba wafu, ubatizo wa vichanga, ibada za miungu mitatu, na upotoshaji wa kila namna katika imani unaofanywa na manabii na watumishi wa uongo katika siku hizi za mwisho kama vile matumizi ya mafuta ya upako, maji ya mto Yordani, chumvi, udongo, n.k hivyo anza sasa upya kurejea katika mstari wa kuyajua mapenzi ya Mungu na kanuni zake kwa kusoma biblia yako na kumwomba Roho Mtakatifu akuongoze kama ulishamwamini Bwana Yesu na kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo, lakini kama bado hujafanya hivyo, basi, nenda katika kanisa sahihi la kiroho lililopo karibu nawe ukabatizwe na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu ambaye atakuwezesha kuishi maisha matakatifu na kukupa uelewa wa maandiko ili usiwe mtoto mchanga tena na kuchukuliwa na upepo wa kila mafundisho na udanganyifu.


Waefeso 4:14  ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu. 

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Bwana akubariki, Shalom.

 +255652274252/ +255789001312



MADA ZINGINEZO:

Akaifanya iwe ishara kwa watu watakaokuwa hawamchi Mungu baada ya haya.


Na wewe umefuata uzushi ulioingizwa kwa werevu? 


 Je! Waraka wa mtume Paulo kwa Wakorintho, ulikuwa ni kwaajiri ya Wakorintho pekee?


Ni lini Bwana alivitakasa vyakula vyote kulingana na 1 Timotheo 4:3?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *