Je! Waraka wa mtume Paulo kwa Wakorintho, ulikuwa ni kwaajiri ya Wakorintho pekee?

JIBU NI HAPANA! Waraka huo haukuwa kwaajiri ya Wakorintho pekee

kumekuwa na mapokeo baadhi leo hii katika kanisa, ambayo yanapinga maagizo ya moja kwa moja ya Mungu kutoka katika maandiko matakatifu [Kwenye waraka wa Paulo kwa Wakorintho]  kwa kisingizio kuwa, maagizo hayo yaliwahusu watu wa Korintho tu. Na maagizo hayo yanayopingwa na wengi ni  suala la WANAWAKE KUFUNIKA VICHWA VYAO WAKATI WA IBADA na WANAWAKE KUTOKUSIMAMA MADHABAHUNI KUFUNDISHA AU KUWA WACHUNGAJI kama Mtume Paulo alivyoandika katka waraka huo. Sasa mapokeo hayo si sahihi kabisa kulingana na biblia takatifu, biblia ipo wazi kabisa kuwa, waraka huo haukuwa kwaajiri ya watu wa Korintho peke yao, bali na kwa Wakristo wote wa kila mahali duniani. Tunaweza lithibitisha hilo katika….

[1 Wakorintho 1:1]  Paulo, aliyeitwa kuwa mtume wa Yesu Kristo kwa mapenzi ya Mungu, na Sosthene ndugu yetu, 

[2] kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, wale waliotakaswa katika Kristo Yesu, walioitwa wawe watakatifu, PAMOJA NA WOTE WANAOLIITIA  JINA LA BWANA WETU YESU KRISTO KILA MAHALI, Bwana wao na wetu.

Umeona hapo aliyekuwa mlengwa wa  waraka huo? Ni kanisa la Korintho, PAMOJA NA  WOTE WANAOLIITA JINA LA BWANA KILA MAHALI. Sasa wewe kiongozi wa kanisa, unathubutu vipi kusema na kufundisha kuwa, waraka huo ulikuwa ni kwaajiri ya Wakorintho pekee? Huoni kama andiko hilo lipo wazi? Hivyo mafundisho hayo ya kusema kuwa waraka huo ulikuwa kwaajiri ya Wakorintho tu! si sawa hata kidogo. Hivyo wanawake wa Kikristo wanapaswa kufunika vichwa vyao wakati wa ibada kanisani kama maandiko yalivyosema katika.

[1 Wakorintho 11:12]…………………HUKUMUNI NINYI WENYEWE KATIKA NAFSI ZENU.

 [13]  JE! INAPENDEZA MWANAMKE AMWOMBE  MUNGU ASIPOFUNIKWA KICHWA?

Na hii ni kwa faida yao kulingana na [1 Wakorintho 1:10]. Tena biblia haijaruhusu wanawake kuwa wachungaji kama ilivyoandikwa kwenye [1 Wakorintho 14:34-38]  hivyo wewe mwanamke unayejiita askofu au unamiliki kanisa, fahamu kuwa maandiko hayo ya waraka huo yamekukataza na usiseme kuwa hayakuhusu.

Na kitu kingine cha kufahamu ni kuwa, nyaraka hizi sio kwamba waliandikiwa watu wa kanisa fulani peke yao, hapana, bali baada ya kusomwa hapo zilikuwa zikipelekwa katika makanisa mengine, na zile za makanisa mengine zilikuwa zinakuja kwa kanisa lingine, hivyo hivyo kwa kwa kubadilishana, soma..

Wakolosai 4:16  WARAKA HUU UKIISHA KUSOMWA KWENU FANYENI KWAMBA USOMWE KATIKA KANISA LA WALAODILIA PIA; na ule wa Laodikia usomwe na ninyi. 

Waraka kwa Waebrania ulisomwa pia na wakolosai, na wa Wakolosai ulisomwa pia sehemu nyingine, hivyo ndivyo makanisa ya Kristo yalivyoimarishwa.

Bwana akubariki, Shalom.

+255652274252/ +255789001312

Tafadhari washirikishe na wengine habari hii njema.



MADA ZINGINEZO:

Kulingana na 1 Wakorintho 11:5 Mwanamke anaruhusiwa kusimama madhabahuni na kuhubiri (kufundisha)?


Mariamu Magdalene alikuwa ni mtume? (Yohana 20:17) 


Ni lini Bwana alivitakasa vyakula vyote kulingana na 1 Timotheo 4:3?


INJILI YA KRISTO HAIENDI NA WAKATI


Je! ni kweli karama ya kunena kwa Lugha haikupewa kipaumbele na mtume Paulo kama yafanyavyo baadhi ya makanisa leo hii?

5 thoughts on -  Je! Waraka wa mtume Paulo kwa Wakorintho, ulikuwa ni kwaajiri ya Wakorintho pekee?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *