BWANA ALIMAANISHA NINI ALIPOSEMA “HAPA YUPO ALIYE MKUU KULIKO HEKALU?”

[Mathayo 12:6]  Lakini nawaambieni, kwamba HAPA YUPO ALIYE MKUU KULIKO HEKALU.

Maneno hayo Bwana aliyasema juu ya SIKU YA SABATO, alipokua akiwajibu Mafarisayo baada ya kuwaona wanafunzi wake wakivunja masuke shambani na kuyala, hivyo kupelekea Mafarisayo kumwambia Bwana kuwa, wanafunzi wake wanatenda yasipasa siku ya sabato. 

[Mathayo 12:1] Wakati ule Yesu alipita katika mashamba siku ya sabato wanafunzi wake wakaona njaa, wakaanza kuvunja masuke, wakala.

 [2] Na Mafarisayo walipoona, walimwambia, Tazama! Wanafunzi wako wanafanya neno ambalo si halali kulifanya siku ya sabato.

Lakini Bwana alianza kuwajibu Mafarisayo kwa kuwafundisha. Sasa ili na sisi tuelewe, hebu tuanzie kusoma msatari wa [5], Bwana aliwambia hivi…

[5]  Wala hamkusoma katika torati, kwamba SIKU YA SABATO MAKUHANI HEKALUNI HUINAJISI SABATO WASIPATE HATIA?

Umeona hapo? Kwamba siku ya sabato Makuhani nao huinajisi sabato HEKALUNI na hawapati hatia. Lakini sababu ya wao kutokupata hatia ni kuwa wanayatenda hayo ndani ya HEKALU, umeona? Tena aliendelea na kuwafundisha hivi…

[Mathayo 12:3]  Akawaambia, Hamkusoma alivyotenda Daudi, alipokuwa na njaa, yeye na wenziwe?

[4]  jinsi alivyoingia KATIKA NYUMBA YA MUNGU, akaila mikate ile ya wonyesho, ambayo si halali kwake kuila wala kwa wale wenziwe, ila kwa makuhani peke yao?

Sasa hapo kwa Daudi anasema “KATIKA NYUMBA YA MUNGU” ni kwasababu hekalu bado halikujengwa wakati huo [ lakini nyumba ya Mungu ndio baadae likaja kujulikana kama hekalu]  hivyo pia Daudi na wenzake nao, hakuhesabiwa kuwa wamekosa kwa kufanya vile ni kwa sababu tu walikiwa kwenye nyumba ya Mungu, yaani ndani ya Hekalu.

Ndipo Bwana akasema sasa, Kama Daudi na wenzake hakuhesabiwa kuwa na hatia, na hao Makuhani hawahesabiwi kuwa na hatia japo kuwa wanainajisi sabato, na hawahesabiwi hatia kwasababu tu wanafanya hivyo katika Hekalu, basi na Mafarisayo nao watambue kuwa, hata hao wanafunzi wake ambao wapo ndani ya Kristo, hawafanyi kosa, kwani Yeye   Mwenyewe, yaani Bwana wetu Yesu Kristo ni MKUU KULIKO HILO HEKALU.

[Mathayo 12:2] Na Mafarisayo walipoona, walimwambia, Tazama! Wanafunzi wako wanafanya neno ambalo si halali kulifanya siku ya sabato.

[3] Akawaambia, Hamkusoma alivyotenda Daudi, alipokuwa na njaa, yeye na wenziwe?

[4] jinsi alivyoingia katika nyumba ya Mungu, akaila mikate ile ya wonyesho, ambayo si halali kwake kuila wala kwa wale wenziwe, ila kwa makuhani peke yao?

[5] Wala hamkusoma katika torati, kwamba siku ya sabato makuhani hekaluni huinajisi sabato wasipate hatia?

 [6]  Lakini nawaambieni, kwamba HAPA YUPO ALIYE MKUU KULIKO HEKALU.

Hicho ndicho ambacho Bwana alikimaanisha hapo, na ndio maana maandiko yanasema hivi juu ya wanafunzi wa Yesu Kristo

[Wakolosai 2: 16] Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au SABATO

Tafadhari, washirikishe na wengine habari hii njema.

Bwana akubariki, Shalom.

+255652274252/ +255789001312



MADA ZINGINEZO

Je! Tunapaswa kushika sabato kulingana na Isaya 66:23?


Sabato zilizowekwa na wanadamu ni zipi? 


Je! Ni kweli Bwana Yesu alishika sabato kuninganana luka 4:16?


NA HAPA YUPO ALIYE MKUU KULIKO YONA.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *