Sabato zilizowekwa na wanadamu ni zipi? 

  Maswali ya Biblia, Uncategorized

SWALI: Ni sabato zipi hizo zilizowekwa na wanadamu? Na je! Ni sahihi mtu kuwahukumu wakristo kwa kutokushika Sabato hizo?

JIBU: Hakuna sabato yoyote iliyowekwa na wanadamu kwenye maandiko, katika biblia sabato zote ziliwekwa na kuamriwa na Mungu mwenyewe, na Mungu aliwapa wana wa Yakobo ziwe kama ishara kati yao na Mungu, na Mungu alizitambua hizo Sabato kama SABATO ZAKE.

Ezekieli 20:12  Tena naliwapa  SABATO ZANGU, ziwe ishara kati ya mimi na wao, wapate kujua ya kuwa mimi, Bwana, ndimi niwatakasaye.

Soma tena katika.

Walawi 26:2   ZISHIKENI SABATO ZANGU, na kupastahi patakatifu pangu; mimi ndimi Bwana. 

Sasa kama Mungu alivyowaambia “ZISHIKENI SABATO ZANGU” akimaanisaha kuwa, zilikuwako sabato zaidi ya moja ambazo Mungu aliwaamuru wana wa Yakobo wazishike.  Mfano: kila baada ya siku sita, siku iliyofuata ilikuwa sabato (Sabato ya SIKU). Kila baada ya miezi sita, mwezi  uliofuata ulikuwa ni sabato (Sabato ya mwezi) na kila baada ya miaka sita, mwaka wa saba uliofuata ulikuwa ni sabato pia. 

Nchi nayo pia ilikuwa na sabato yake ambayo iliangukia kwenye mwaka wa saba baada ya miaka sita kupita, mwaka wa saba ulikuwa ni sabato ya nchi, wana wa Yakobo hawakuruhusiwa kupanda chochote wala kuvuna chochote kwani ilikuwa ni sabato ya Bwana kwaajiri ya nchi.

Walawi 25:1  Kisha Bwana akanena na Musa katika mlima wa Sinai, na kumwambia,

 2  Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Hapo mtakapoingia katika nchi niwapayo, ndipo hiyo NCHI ITASHIKA SABATO KWA AJILI YA BWANA.

3 PANDA SHAMBA LAKO MIAKA SITA, na miaka sita lipelee shamba lako la mizabibu, na kuyachuma matunda yake; 

4 LAKINI KATIKA MWAKA WA SABA ITAKUWA NI SABATO YA KUSTAREHE KABISA KWA AJILI YA HIYO NCHI, ni Sabato kwa Bwana; usipande shamba lako, wala usipelee shamba lako la mizabibu.

5  Hicho kimeacho chenyewe katika mavuno yako, usikivune, wala zabibu za mizabibu isiyopelewa usizitunde; utakuwa mwaka wa kustarehe kabisa kwa ajili ya hiyo nchi. 

Sasa je! Wakristo wanatakiwa kuzishika hizi sabato za SIKU, MIEZI na MIAKA? Jibu ni la! Hayo yote yalikuwa ni kivuli cha mambo yajayo (ukitaka kufahamu ni kwa namna gani, acha ujumbe kwenye sanduku la maoni) na wala hatutakiwi kuyarudia hayo mafundisho ya kushika SIKU NA MIEZI NA MIAKA na nyaka, kama maandiko yanavyosema katika.

Wagalatia 4:9  Bali sasa mkiisha kumjua Mungu, au zaidi kujulikana na Mungu, kwa nini kuyarejea tena mafundisho ya kwanza yaliyo manyonge, yenye upungufu, ambayo mnataka kuyatumikia tena?

 10  Mnashika siku, na miezi, na nyakati, na miaka. 

Nachotaka uone hapo ni kuwa, hadi mtume Paulo anawaandikia wakristo wa Galatia kuwa, hakuna haja ya kuyarudia mafundisho hayo manyonge ya kushika siku na miezi na miaka ni wazi kuwa, walikuwapo watu ambao, waliwahubiria hao wakristo wa Galatia kuwa wanapaswa washike siku, miezi n.k  Kufunua kwamba, kama injili iliyohubiriwa na akina Paulo inaendelea kuhubiriwa hadi sasa, basi ni wazi kuwa, hata sasa watu ambao waliwafundisha watu wa Galatia kushika siku na miezi na miaka wapo hadi sasa hivi na bado wanaendelea kuhubiri hayo mafundisho. Biblia inasema katika.

Wakolosai 2:16  Basi, mtu ASIWAHUKUMU ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au SABATO; 

17 mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo. 

Na Sabato zinazozungumziwa hapo ni hizo hizo walizopewa wana wa Yakobo na wala si sabato zilizowekwa na mwanadamu, hakuna sehemu ambayo mwanadamu ameweka sabato kwenye maandiko.

Bwana akubariki. Shalom.


Mada zinginezo:

Je! Ni kweli Bwana Yesu alishika sabato kuninganana luka 4:16?


Siku sahihi ya kuabudu ni ipi, siku ya sabato ni lini?Je! Ni kweli majuma sabini aliyoambiwa Daniel yamekwisha timia?(Daniel 9:23-27)


Je! Ni kweli mke anapaswa kumtii mumewe kwa kila jambo hata kama ni ovu?

2 thoughts on - Sabato zilizowekwa na wanadamu ni zipi? 

  • Kwa habari ya Sabato maelezo hayo hayazungumzii Sabato ya siku ya saba (Jumamosi) ambayo ni amri ya nne katika amri 10 za Mungu. Ikumbukwe kuwa maagizo aliyopewa Musa na Mungu katika mlima wa Sinai yako katika mkundi 4:
    1. Civil laws : hizi zilikuwa ni amri zilizowahusu wana wa Israel kama Taifa na zilikoma Israel ilipokoma kuwa taifa teule mwaka 34 B.K Stephano alipopigwa mawe hadi kufa alipotamka kuwa sasa tunawageukia mataifa.

    2. Ceremonial laws: Hizi zilikuwa ni taratibu za ibada na utoaji wa kafara ambazo zilikoma Yesu alipokufa msalabani. Akasema ” imekwisha” . Hizi zilikuwa kivuli cha kafara uhalisia yaani Yesu Kristo.

    3. Health laws: Hizi zilikuwa ni kanuni za afya zilizohusisha uchimbaji wa vyoo na vitu Mungu alivyoruhusu vitumike kama chakula. Hizi huendelea hadi mtu anakuja kuishi hapa duniani.

    4. Moral laws. Hizi kanuni za madaili ambazo ni amri Kumi za Mungu ikiwemo amri ya Sabato ya siku ya saba. Hizi hazina mwisho maana ni muhtasari wa tabia ya Mungu ambayo imejengwa juu ya msingi wa upendo.

LEAVE A COMMENT