Biblia imeruhusu ubatizo wa vichanga? (kulingana na matendo 16:33)

  Maswali ya Biblia, Uncategorized

Matendo Ya Mitume 16:33 Akawakaribisha saa ile ile ya usiku, akawaosha mapigo yao, KISHA AKABATIZWA, YEYE NA WATU WAKE WOTE WAKATI UO HUO. 

SWALI: Je! Biblia imeruhusu ubatizo wa watoto wachanga kulingana na kitabu cha  Matendo ya mitume 16:33? Kwasababu maandiko yanasema kuwa, yule mlinzi wa gereza alibatizwa yeye na watu wote waliopo nyumbani mwake, hivyo ni wazi kuwa, kulikuwapo na watoto wachanga ambao walibatizwa na akina Paulo na Sila.

JIBU: Shalom, Bwana Yesu apewe sifa. Hebu tusome mistari hiyo kuanzia juu kidogo ili tupate jibu kamili la swali letu.

Matendo Ya Mitume 16:25   Lakini panapo usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza.

 26 Ghafula pakawa tetemeko kuu la nchi, hata misingi ya gereza ikatikisika, na mara hiyo milango ikafunguka, vifungo vya wote vikalegezwa.

 27 Yule mlinzi wa gereza akaamka, naye alipoona ya kuwa milango ya gereza imefunguka, alifuta upanga, akataka kujiua, akidhani ya kuwa wafungwa wamekimbia.

 28 Ila Paulo akapaza sauti yake kwa nguvu, akisema, Usijidhuru, kwa maana sisi sote tupo hapa. 

29 Akataka taa ziletwe, akarukia ndani, akitetemeka kwa hofu, akawaangukia Paulo na Sila; 

30 kisha akawaleta nje akasema, Bwana zangu, yanipasa nifanye nini nipate kuokoka?

 31 Wakamwambia, Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako.

 32 WAKAMWAMBIA NENO LA BWANA, YEYE NA WATU WOTE WALIOMO NYUMBANI MWAKE. 

33 Akawakaribisha saa ile ile ya usiku, akawaosha mapigo yao, kisha akabatizwa, yeye na watu wake wote wakati uo huo. 

34 Akawaleta juu nyumbani kwake, akawaandalia chakula, akafurahi sana, yeye na nyumba yake yote, maana amekwisha kumwamini Mungu. 

Nachotaka uone ni hapo kwenye mstari wa 32, ukisoma kwa makini huo mstari, utapata jibu la watu ambao walibatizwa nyumbani mwa huyo mlinzi wa gereza.

Matendo Ya Mitume 16:32 WAKAMWAMBIA NENO LA BWANA, YEYE NA WATU WOTE WALIOMO NYUMBANI MWAKE. 

Huo mstari umeelezea vizuri kabisa kuwa, watu waliolezwa NENO LA BWANA akiwemo na huyo mlinzi ndio waliobatizwa, sasa biblia haijaseama kama walikuwapo watoto wachanga au la!   Ila hata kama walikuwepo, watoto wachanga huwezi waeleza neno la Bwana na wakaamini, hivyo, wote waliobatizwa ni wale walio amini neno la Bwana baada ya kuelezwa na akina Paulo na Sila.

Ata Bwana Yesu kipindi anapaa kwenda mbinguni, alisema kuwa, ATAKAYEAMINI NA KUBATIZWA ataokoka (Marko 16:16). Hivyo hatua ya kwanza ni mtu kuamini na kinachofuta baada ya hapo ni kwenda kubatizwa kama hao watu wa nyumbani mwa mlinzi wa gereza.

Kwenye biblia hakuna sehemu yoyote ambayo mtoto mchanga alibatizwa, ubatizo huo sio sahihi kulingana na maandiko na wala hautokani na maandiko. Wakristo wote kwenye biblia walibatizwa kwa ubatizo mmoja ambao ni kuzamishwa na kwa jina la Yesu.

Waefeso 4:5 Bwana mmoja, imani moja, UBATIZO MMOJA. 

Hivyo ubatizo wowote tofauti na huo si sawa kilingana na maandiko. Je! Umeshamwamini Bwana Yesu na kubatizwa katika ubatizo sahihi? Kama bado chukua uamuzi leo, tafuta kanisa lolote sahihi la kiroho lililopo karibu nawe ili usaidiwe na kupokea Roho matakatifu ndani yako atakaye kuwezesha kuishi maisha ya utakatifu hadi siku ile Bwana atakaporudi kwaajiri ya watakatifu wake.

Bwana akubariki. Shalom.


Mada zinginezo:

Je ubatizo sahihi ni kwa jina la Yesu au Baba, Mwana na Roho Mtakatifu?


Je! Bikira Maria ni mkamilishaji wa mahitaji yetu pale tunapokwama? (kulingana na Yohana 2:3-5)


IKIMBIENI IBADA YA SANAMU.


MADHARA YA KUTOKUSOMA BIBLIA YAKO.

LEAVE A COMMENT