IKIMBIENI IBADA YA SANAMU.

  Biblia kwa kina, Uncategorized

Moja ya vitu ambavyo biblia imevitaja kuwa ni vitu vya kukimbiwa, ni IBADA ZA SANAMU. Vingine vikiwemo zinaa na tamzaa za ujanani.

Sasa Biblia inasema katika…

1 Wakorinto 10:14   Kwa ajili ya hayo, wapenzi wangu, IKIMBIENI IBADA YA SANAMU. 

Nabii Yeremia aliwaambia watu wa Yuda walionusurika kwenda utumwani Babeli na kushuka Misri, kuwa, waache (WAZIKIMBIE) hizo ibada za masananu na kumfukizia uvumba MALKIA WA MBINGUNI, kwani ni machukizo mbele za Mungu na kwa sababu ya hayo, ghadhabu ya Mungu imewaka juu yao. Lakini wale watu walikataa shauri la Mungu kwa kinywa cha nabii Yeremia.

Yeremia 44:15 Ndipo watu wote waliojua ya kuwa wake zao waliwafukizia uvumba miungu mingine, na wanawake wote waliosimama karibu, mkutano mkubwa, yaani, watu wote waliokaa katika nchi ya Misri, katika Pathrosi, wakamjibu Yeremia, wakisema, 

16 Neno lile ulilotuambia kwa jina la Bwana, SISI HATUTAKUSIKILIZA. 

17 LAKINI BILA SHAKA TUTALITIMIZA KILA NENO LILILOTOKA KATIKA VINYWA VYETU, KUMFUKIZIA UVUMBA MALKIA WA MBINGUNI, na kummiminia sadaka za kinywaji, KAMA TULIVYOTENDA SISI, NA BANA ZETU, na wafalme wetu, na wakuu wetu, katika miji ya Yuda, na katika njia kuu za Yerusalemu; maana wakati huo tulikuwa na chakula tele, na kufanikiwa, wala hatukuona mabaya. 

Umeona?  Sasa maandiko yanasema kuwa, Mungu ni yule yule, jana na leo na hata milele, na hata sasa bado anazichukia ibada za sanamu na kuwaagiza watu wazikimbie hizo ibada za sanamu, lakini kitu cha kushangaza ni kuwa, hadi sasa watu bado wanashingo ngumu kama walivyokuwa watu wa Yuda, watu bado wanasema hivi ndivyo walivyofanya babu zangu na wazazi wangu kama tu walivyosema watu wa Yuda.

Ndugu yangu, ibada ya sanamu sio kitu cha kuking’ang’ania hata kidogo, kwani inamchukiza sana Mungu, sio kitu cha kusema kuwa, mimi kwetu babu yangu na wazazi wangu walikuwa wanafanya hivi, la!  Bali ni kitu cha kukikimbia kabisa, kama neno la Mungu linavyosema katika…

1 Wakorinto 10:14   Kwa ajili ya hayo, wapenzi wangu, IKIMBIENI IBADA YA SANAMU. 

Inawezekana babu yako au wazazi wako walishindwa au wanashindwa kuikimbia ibada hiyo ya sanamu kama ilivyokuwa kwa mababu, na wazazi wa watu wa Yerusalemu, lakini wewe neno la Mungu leo hii linakwambia  kuwa, IKIMBIE IBADA YA SANAMU. Acha kumwabudu na kumwomba huyo unayemwita MALKIA WA MBINGUNI ukidhani kuwa unamwomba Mungu kwa njia hiyo, hapo humwombi Mungu ndugu yangu, isipokuwa unaabudu mapepo yaliyoabudiwa na watu wa Yuda pasipo wewe mwenyewe kufahamu, Mungu anakutaka utoke huko kwani waabudu sanamu kama hao wanao mwabudu MALKIA WA MBINGUNI sehemu yao ni katika ziwa la moto.

Ufunuo wa Yohana 21:8  Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na HAO WAABUDUO  SANAMU, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.

Ikiwa utakuwa na swali lolote kuhusu biblia, basi, wasiliana nasi kwa namba hizi

+255652274252/ +255789001312

Bwana akubariki, Shalom.


MADA ZINGINEZO:

Je! Bikira Maria ni mkamilishaji wa mahitaji yetu pale tunapokwama? (kulingana na Yohana 2:3-5)


Biblia imeruhusu ubatizo wa vichanga? (kulingana na matendo 16:33)


Je! Ni dhambi kibiblia kuwaomba wafu (watakatifu)?

4 thoughts on - IKIMBIENI IBADA YA SANAMU.

LEAVE A COMMENT