JE! NI LAZIMA TUNAPOSALI TUPIGE MAGOTI?

  Maswali ya Biblia, Uncategorized


SWALI: Je! Ni lazima kila tunaposali au kuomba, tupige magoti? Kwa sababu tunaona katika habari ya Danieli, biblia inasema kuwa, alikuwa AKIPIGA MAGOTI MARA TATU KILA SIKU alipokuwa akisali (Danieli 6:10) Je! Kwa sababu hiyo tuhitimishe kuwa NI LAZIMA kupiga magoti tunaposali au kuomba?

JIBU: Ni kweli kabisa kuwa, Danieli alikuwa akipiga magoti mara tatu kwa siku alipokuwa akisali, ila hatupaswi kuhitimisha kuwa, hiyo ndio kanuni au utaratibu tunapotaka kwenda mbele za Mungu, kwamba ni LAZIMA tupige magoti, hapana! Sio kila mtu kwenye maandiko, alipokuwa akisali au kuomba alipiga magoti kana kwamba ndio amri na pasipo kupiga magoti basi tunakuwa tunafanya makosa hapana! Kuna wafalme na manabii kadha wa kadha ambao biblia inaeleza kuwa, hawakuwa wamepiga magoti walipokuwa wakiomba na Bwana alijibu maombi yao, mfano nabii Eliya. Nabii Eliya alikuwa amesujudu kifudifudi hadi uso wake ukafika magotini alipokuwa akiomba na Bwana alijibu maombi yake.

1 Wafalme 18:42  Basi Ahabu akainuka ili ale na kunywa. Naye Eliya akapanda juu mpaka kilele cha Karmeli; akasujudu kifudifudi, akainama uso mpaka magotini. 

Na tena ni kweli kuwa, Bwana Yesu alikuwa akipiga magoti alipokuwa akiomba, biblia inasema hivyo katika..

Luka 22:41  Mwenyewe akajitenga nao kama kiasi cha kutupa jiwe, AKAPIGA MAGOTI AKAOMBA,

Lakini si kila mahali alipoomba alikuwa akipiga magoti, kwani kuna saa alikuwa akishukuru huku amesima, na wakati mwengine alikuwa akiomba akiwa ameanguka kifulifuli na maombi yake yalikuwa bora sana mbele za Mungu.

Matayo 26: 39  Akaendelea mbele kidogo, AKAANGUKA KIFULIFULI, AKAOMBA, akisema, Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke; walakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe. 

Lakini pia, hata yule mtoza ushuru ambaye Bwana alimtolea mfano pamoja farisayo, Bwana alisema kuwa, yule mtoza ushuru alikuwa AMESIMAMA mbali na hekalu na kujipiga piga kifua na Kuomba toba akiwa amesimama na maombi yake yalifika kwa Mungu na Mungu alimwesabia haki.

Luka 18:13 Lakini yule mtoza ushuru ALISIMAMA MBALI, wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, bali alijipiga-piga kifua akisema, Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi.

14 Nawaambia, huyu alishuka kwenda nyumbani kwake amehesabiwa haki kuliko yule; kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa. 

Hivyo basi, unaweza kuomba ukiwa umekaa kwenye basi kama upo safarini, au ukiwa umesimama kwenye daladala, au ukiwa unatembea, au ukiwa umepiga magoti tu, au hata ukiwa umepiga magoti na kuinua mikono yako juu, au ukiwa unasujudu, n.k na Mungu atasikia tu maombi yako. Ila kitu kikubwa unachopaswa kuzingatia ni kuwa, hakikisha upo katika hali ya utakatifu, yaani kujitenga na dhambi, tunapoenda mbele za Mungu hatuna budi kuomba toba na rehema kwanza.

Lakini endapo kama upo kanisani, na kuna utaratibu fulani mfano, kusimama wakati wa sifa, au kuabudu, au kufungua ibada, basi hapo utafuata utaratibu wa kanisa kwa muda husika, au kama upo na wapendwa baadhi na mmekubaliana kufanya jambo fulani basi hapo mtafanya hicho mlichokubaliana.

Bwana akubariki, Shalom.

Tafadhari, washirikishe na wengine ujumbe huu.

+255652274252/ +255789001312



MADA ZINGINEZO:

Je! ni sahihi kuoa/kuolewa na mtu aliyekuzidi umri.


Bwana alimaanisha nini kusema ‘Na kondoo wengine ninao, ambao si wa zizi hili?


Neno Daawa linamaana gani kibiblia?


Je! kupiga punyeto ni dhambi kwa mujibu wa biblia?

4 thoughts on - JE! NI LAZIMA TUNAPOSALI TUPIGE MAGOTI?

LEAVE A COMMENT