Je! ni sahihi kuoa/kuolewa na mtu aliyekuzidi umri.

  Ndoa na Mahusiano, Uncategorized

Kuoa/kuolewa na mtu aliyekuzidi umri, ni sawa kibiblia?

Biblia haijatoa katazo lolote la ki umri katika suala la ndoa. Imekataza mambo kama ndoa za jinsia moja, kuoa wake wengi, kufanya tendo la ndoa kinyume na maumbile.. Lakini katika eneo la umri, haijasema chochote, na hivyo, si dhambi, mtu kuoa/ kuolewa na mtu aliyemzidi umri, maadamu tu, jambo hilo limetokana na Upendo.

Lakini tunapaswa tuchukue tahadhari, kwasababu siku hizi za mwisho, ambazo Bwana Yesu, alisema ni za KIZAZI CHA UZINZI, tamaa imeongezeka, watu wamekuwa hawana kiasi tena.. wanaoa na kuolewa bila mipango au taratibu za ki-Mungu. Bwana Yesu alisema;

Luka 17:26 “Na kama ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa katika siku zake Mwana wa Adamu.

27 Walikuwa wakila na kunywa, walikuwa wakioa na kuolewa, hata siku ile Nuhu aliyoingia katika safina, gharika ikashuka ikawaangamiza wote.

28 Na kadhalika, kama ilivyokuwa katika siku za Lutu, walikuwa wakila na kunywa, walikuwa wakinunua na kuuza, wakipanda na kujenga”;

Hapo anaposema walikuwa wakioa na kuolewa haimaanisha tu ndoa za kawaida, hapana, bali ndoa zisizo za kiMungu, angali leo hii ndoa zilivyo nyingi, mtu anaweza kuolewa hata mara 4,  sio kwamba kifo kiliwatenganisha hapana, bali amemchoka tu, anataka kujaribu mwingine.

Vivyo hivyo  asilimia kubwa ya ndoa kama hizi zinakuja aidha kwa Tamaa  ya mwili au kwa tamaa ya mali.

Binti wa miaka 20 kuolewa na mzee wa miaka 70, si kitendo cha kawaida utagundua wengi wa hao wamefuata mali, na si kingine. Vilevile au kijana wa miaka 25 kuoa bibi wa miaka 80, asilimia kubwa ni pengine ameona kuna maslahi Fulani kwa mzee huyo.

Halikadhalika mzee, kufikia uamuzi wa kutaka kuolewa/kuolewa na kijana, kwa asilimia kubwa ni tamaa ya mwili isiyo ya kawaida ndiyo inayomwendesha, ambayo kwa umri kama wa kwake, hastahili kufanya hivyo.

Lakini kama haijatokea katika vitu hivyo viwili, yaani tamaa ya mwili au mali, na kwamba wamekutana, wamependana,upendo wa kweli, basi ni sawa na hakuna makosa yoyote,  wakifunga ndoa na wakiishi katika upendo na kumcha Mungu, watabarikiwa kama tu ndoa nyingine zibarikiwavyo.

Bwana akubariki.

+255693036618/ +255789001312

One Reply to “Je! ni sahihi kuoa/kuolewa na mtu aliyekuzidi umri.”

  • Nimeelewa somo vizuri..!
    Nami pia niombe kuuliza je kupendana na mwanamke mwenye mtoto na kanizidi miaka 3 mimi 27 yeye 30.. na pia mimi nina mtoto kwa mwanamke mwingine, yeye mwanaume wake kaoa huko na mimi mwanamke wangu kaolewa huko.. lakini me nakuwa na hofu sana kwakuwa kanizidi umri na pia ni msomi ana degree zake mimi nina elimu ya kawaida lakini anaonesha kunipenda na kuniheshimu.. je ni naweza muoa huyo mwanamke KIBIBLIA au nifanyaje maana nataka mambo yakienda vizuri nimuoe kwa. Harusi.. Je natakiwa niangalie upendo au niangalie nini naomba ushauri🙏🙏🙏

LEAVE A COMMENT