Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.

Maswali ya Biblia, Uncategorized No Comments

Swali: Je pale Bwana Yesu aliposema, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Alimaanisha tukawahubirie injili mijusi, na swala, na ngamia?

Marko 16:15 “Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.

16 Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa”.

JIBU: Bwana hakuwa na maana, kwamba tukawahubirie Wanyama hawa injili, hapana, kwasababu mnyama hawezi kuamini na kubatizwa.. Wala hakuna mahali popote biblia inarekodi mitume walikwenda kuwahubiria Wanyama nao wakaokoka.

Lakini Bwana Yesu alimaanisha nini kusema vile?

Kumbuka yapo maono yanayofanana na hayo mtume Petro alionyeshwa na Bwana Yesu, hivyo tukiyatafakari vizuri tutafahamu Bwana Yesu alimaanisha nini kusema vile.  Na maono yenyewe yalikuwa ni kuhusu aina mbalimbali za Wanyama, walioshushwa kutoka juu katika shuka, kisha Petro akaambiwa awachinje ale, Lakini yeye akakataa na kusema, kamwe sijawahi kula kitu najisi. Na sauti ikamwambia, alichokitakasa Mungu usikiite wewe najisi.

Matendo 10:9 “Hata siku ya pili, walipokuwa wakisafiri na kuukaribia mji, Petro alipanda juu darini, kwenda kuomba, yapata saa sita ya mchana;

10 akaumwa na njaa sana, akataka kula; lakini walipokuwa wakiandaa, roho yake ikazimia,

11 akaona mbingu zimefunuka, na chombo kikishuka kama nguo kubwa, inatelemshwa kwa pembe zake nne hata nchi;

12 ambayo ndani yake walikuwamo aina zote za wanyama wenye miguu minne, na hao watambaao, na ndege wa angani.

13 Kisha sauti ikamjia, kusema, Ondoka, Petro, uchinje ule.

14 Lakini Petro akasema, Hasha, Bwana, kwa maana sijakula kamwe kitu kilicho kichafu au najisi.

15 Sauti ikamjia mara ya pili, ikimwambia, Vilivyotakaswa na Mungu, usiviite wewe najisi”.

Na baadaye ndipo akatambua kuwa maono yale, yalikuwa ni kuwapelekea injili watu wa mataifa. Kwani hapo kwanza mitume walikuwa hawachangamani na mataifa, hata injili walikuwa hawawahubirii .

Kwahiyo, tunaweza kuona hapo, kuhubiri injili kwa kila kiumbe maana yake, ni kuhubiri kwa jamii zote za watu, bila kuchagua, lugha, rangi, kabila, dini, itikadi, jinsia,, maumbile n.k. wote wanastahili injili..wote, wanastahili kumjua Kristo, kila jamii ya watu,wenye dhambi nyingi, na wenye kidogo, matajiri au maskini, wakubwa na wadogo, wote wasikie injili.

Lakini sio kwenda kuwahubiria Samaki, na vinyonga injili hapana.

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *