Je Kusheherekea siku ya kuzaliwa (birthday), ni sawa kibiblia?

  Maswali ya Biblia, Uncategorized

Sherehe yoyote ile, iwe ni  ya kuzaliwa, au ya mahafali, au ya ndoa, au ya kitaifa, biblia haijakataza kwa namna yoyote ile kusheherekewa. Isipokuwa sherehe za ulafu ndio zimekatazwa…

Sherehe za ulafi ni sherehe, zinazoambatana na mambo kama ulevi, anasa, mashindani, uvaaji mbovu, matusi, mauaji, n.k.

Kwamfano, Herode alipokuwa anasheherekea, sikukuu yake ya kuzaliwa, alimwalika binti yake amechezee, na alipomchezea, akampa kichwa cha Yohana kama malipo ya ahadi yake kwake. Hivyo, sikukuu kama ile, mbele za Mungu ni sikuu  ya damu na anasa, na hivyo Mungu hairidhii

Mathayo 14:6 “Hata ilipofika sikukuu ya kuzaliwa kwake Herode, binti Herodia alicheza mbele ya watu, akampendeza Herode.

7 Hata akaahidi kwa kiapo ya kwamba atampa lo lote atakaloliomba.

8 Naye, huku akichochewa na mamaye, akasema, Nipe hapa katika kombe kichwa cha Yohana Mbatizaji.

9 Naye mfalme akasikitika; lakini kwa ajili ya viapo vyake, na kwa ajili ya wale walioketi chakulani pamoja naye, akaamuru apewe;

10 akatuma mtu, akamkata kichwa Yohana mle gerezani.

11 Kichwa chake kikaletwa katika kombe, akapewa yule kijana; akakichukua kwa mamaye”.

Biblia inasisitiza na kusema..

1Petro 4:3 “Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuenenda katika ufisadi, na tamaa, na ulevi, na karamu za ulafi, na vileo, na ibada ya sanamu isiyo halali”;

Biblia bado imetabiri, kuwa katika siku za mwisho, watu watakuwa ni wa kupenda sana anasa kuliko kumpenda Mungu(Timotheo 3:4). Watu watakuwa ni wa kupenda sherehe sherehe za ulafi, party party.. Hivyo ni kuwa makini na sherehe tunazozifanya, tujiulize Je, ni za kiasi au zinavuka mipaka?

2Petro 2:13 “Wakipatikana na madhara, ambayo ni ujira wa udhalimu wao, wakidhania kuwa ulevi wakati wa mchana ni anasa; wamekuwa ni mawaa na aibu wakifuata anasa zisizo kiasi katika karamu zao za upendo, wafanyapo karamu pamoja nanyi;”

Hivyo ili tuwe salama, tuhakikishe, lolote tulifanyalo, basi ni katika utukufu wa Mungu, yaani tunaliweka katika misingi ya kiimani. Tumtangulize yeye, huku tukiwa na kiasi. Hapo ni uhakika kuwa karamu zetu zitampendeza Mungu, lakini kama tutashindwa, ni heri tuache tu. Tunaweza kuishi bila sherehe. Lakini hatuwezi kuishi bila Mungu.

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT