Je! kupiga punyeto ni dhambi kwa mujibu wa biblia?

  Dhambi, Uncategorized

Dhambi hainzii mwilini, bali dhambi inaanzia rohoni, na ndio maana Bwana Yesu alisema..

Mathayo 15:18 “Bali vitokavyo kinywani vyatoka moyoni; navyo ndivyo vimtiavyo mtu unajisi.

19 Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wivi, ushuhuda wa uongo, na matukano;

Hivyo, kabla ya kutaka kufanya tendo lolote la zinaa, huwa linaanzia kwanza moyoni, kwa kutamani.  Pale unapotamani tu, tayari umeshazini kabla hata ya kukutana na yule mtu kwa mujibu wa maandiko.

Mathayo 5:28 “lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake”.

Kama ‘wazo’ tu ni dhambi, si Zaidi ‘tendo la wazo’?

Hivyo, punyeto/ Masturbation ni dhambi, kwasababu hilo ni zao la tamaa ya uzinzi. Na haupaswi kufanya kama mtoto wa Mungu, kwasababu wote wanaofanya hivyo hawawezi kwenda mbinguni.

Ukiwa mfanyaji wa dhambi hii, wewe mwenyewe tu dhamiri yako itakushuhudia unachokifanya sio sawa, bila hata kuhubiriwa au kusoma biblia.

Kabla hujafanya chochote, tafakari kwanza, Je! Yesu anaweza kufanya hilo jambo? Kama hawezi basi, ujue ni dhambi.

Lakini pengine umejaribu kuacha kwa nguvu zako umeshindwa.. Yupo atakayeweza kukusaidia kuacha, kwasababu hata na mimi nilipokuwa dhambini, sikuwahi kufikiri kama jambo hilo linawezekana, kwasababu nilikuwa tayari nimeshakuwa teja wa dhambi hiyo, tangu nikiwa mdogo.

Lakini siku nilipokusudia kumpa Yesu Maisha yangu kwa moyo wangu wote, na kufuta picha zote za ngono kwenye kompyuta yangu, na kuacha kutazama hata thamthilia na muvi zenye maudhui hayo..

Ghafla nilishangaa Bwana ameniondoelea kiu hiyo, na kunipa nguvu mpya ya kuishinda dhambi hiyo Pamoja na uzinzi. Hadi sasa ni miaka mingi sana imeshapita sijawahi hata kutamani kufanya kitendo hicho.

Hakuna linaloshindikana kwa Mungu, kwasababu yeye ndio anayetupa uwezo wa kushinda dhambi, na kufanana na Kristo, sio kwa akili zetu (Yohana 1:12). Kifungo hicho anachoweza kukufungua ni Kristo tu peke yake.

Hivyo kama iliwekezana kwangu itawezekana na kwako pia.. Ikiwa upo tayari kuacha kabisa kabisa dhambi hiyo, basi bofya hapa, upokee mwongozo utakaokusaidia kuacha uzinzi na punyeto moja kwa moja.>>> MOTO HUFA KWA KUKOSA KUNI

Bwana akubariki.

4 thoughts on - Je! kupiga punyeto ni dhambi kwa mujibu wa biblia?

LEAVE A COMMENT