Kwanini Bwana alisema ‘Ninyi ni chumvi ya dunia’?

Maswali ya Biblia No Comments

Mathayo 5:13
[13]Ninyi ni chumvi ya dunia; lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee? Haifai tena kabisa, ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu.

Chumvi ni kiungo kinachodumu milele kama ikihifadhiwa vizuri, ikiwa na maana kama kuna chumvi ilitumiwa na akina Martha kuungia mbona ya Bwana Yesu miaka 2000 iliyopita, na kutunzwa vema basi mpaka leo hii yaweza kutumika tena ikiwa na ubora wake ule ule..

Na kama vile tunavyojua ili chakula kiwe na ladha haijalishi kitaungwa na viungo vizuri vingi namna gani vikikosa chumvi tu, kinapoteza ladha yote..

Vivyo hivyo na sisi watakatifu mbele ya Bwana..Ndivyo anavyotuona tulivyo katika ulimwengu huu, ni kama vile chumvi kwa walimwengu.tusipokuwepo sisi, huu ulimwengu hauna maana yoyote kwake haijalishi wanadamu watakuwa na ustaarabu mzuri namna gani..

Lakini bado anaendelea kusema..

“lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee”?

Kwa kawaida chumvi haiponyeki, ikishaharibiwa kwa kutiwa dosari, au kuachwa katika mazingira yasiyostahili, haiwezi tumika tena ni kuitupa tu jalalani.

Hiyo ni kuonyesha kuwa sisi watakatifu tunapaswa tuwe makini sana na wokovu wetu, dosari ndogo ndogo sana zitatufanya tusiwe na maana tena kwenye huu ulimwengu na hata mbinguni..

Jiulize kwanini mwenye dhambi akifumaniwa na mchungaji akifumaniwa..yule mchungaji ndiye atakayeleta ukakasi mkubwa zaidi kuliko yule mwingine..

Hata akitubu mpaka aeleweke tena kwamba alidondoka katika dhambi na sasa hayupo hivyo tena..hakuna atakayemwelewa isipokuwa tu labda kwa watakatifu wenzake..Lakini kwa ulimwengu hafai tena..kwasababu yeye alikuwa ni chumvi lakini sasa si chumvi tena.

Hivyo Bwana Yesu anatazamia sote sisi tuliookoka, tuuchunge wokovu wetu na imani yetu kwasababu tumekabidhiwa mara moja tu, tukiudondosha tusahau kuupata tena.

Yuda 1:3-4
[3]Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ili niwaonye kwamba mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu.
[4]Hukumu kwa Waalimu Waongo.

Ikiwa tunaishi maisha ya kutokujali, maisha ya uvuguvugu, maisha ya mguu mmoja njw mwingine ndani, basi tuache, tugeuke, tufahamu kuwa sisi ni chumvi ambayo inapaswa iwe na ubora ule ule tangu mwanzo hadi mwisho.

Hakuna namna tunapaswa kuupoteza ubora wetu na viwango vyetu.

Maran Atha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *