Biblia inamaanisha nini kusema “Yaliyopotoka hayawezi kunyoshwa,”

  Dhambi, Uncategorized

Tusome;

Mhubiri 1:15
[15]Yaliyopotoka hayawezi kunyoshwa,
Wala yasiyokuwapo hayahesabiki.

Mwandishi wa kitabu hiki cha mhubiri ni Sulemani..na katika uandishi wake alilenga kutafiti mambo yanayotamaniwa na wanadamu bila kujali yanavyochukuliwa na watu katika jamii kwamba ni mazuri au mabaya..alijaribu yote

Lengo lake lilikuwa ni kutathimini kama ipo hekima au uhalisia wowote ndani ya hilo linavyozungumziwa..hivyo akajaribu mpaka anasa na starehe zote na ulevi..

Na baadaye akapata jibu kwamba vile. Vitu ambavyo Mungu kaviona havifai au kavikataza kamwe mwanadamu hata ajitahidije kuviremba haviwezi kuvifanya viwe vizuri.

Kwa namna nyingine ni sawa na kusema Mungu aliyoyapotosha kamwe hayawezi kunyoshwa.

Ndio maana sehemu nyingine mhubiri anasema;

Mhubiri 7:13
[13]Tafakari vema kazi yake Mungu; kwa sababu ni nani awezaye kukinyosha kitu kile alichokipotosha yeye?

Haijalishi wanadamu wataisifia pombe kiasi gani, kama Mungu kaikataa itabakia kuwa mbaya tu.

Haya ndio maneno ya Sulemani..

Mhubiri 2:3,11
[3]Moyoni mwangu nikapeleleza jinsi ya kuuburudisha mwili kwa mvinyo, na (moyo wangu ukali ukiniongoza kwa hekima) jinsi ya kushikana na upumbavu, hata niyaone yaliyo mema ya kuwafaa wanadamu, ili wayafanye hayo chini ya mbingu siku zote za maisha yao…

[11]Kisha nikaziangalia kazi zote zilizofanywa kwa mikono yangu, na taabu yote niliyotaabika katika kuzitenda; na tazama, yote ni ubatili na kujilisha upepo, wala faida hakuna chini ya jua.

Haijalishi watu watahalalisha vipi ushoga, kiserikali na kidini kama Bwana ameshaukataa utabakia tu kuwa ni dhambi..

Vivyo hivyo na sisi, tusiyajaribu yaliyopotoshwa na Mungu..punyeto, pornography, vimini, kujichua, tunajua kabisa hata kwa dhamiri zetu ni dhambi..

Hivyo tuchue tahadhari..tuitii sheria ya Mungu. Nyakati hizi za mwisho roho ya kuhalalisha mambo ambayo Mungu kayakataza ndio imekithiri na ubaya zaidi imefika mpaka katika nyumba za ibada, kwamfano andiko la mwanamke kuwa kiongozi kanisani ni jambo ambalo Mungu kalipiga marufuku katika biblia..1Wakorintho 14:34 lakini, linachukuliwa katika mtizamo hasi..

Sasa haijalishi tutalinyoosha hilo namna gani, Mungu tayari ameshalikataa..tunapaswa tutii.

Bwana atusaidie sana

LEAVE A COMMENT