SABURI NI NINI KATIKA BIBLIA?

  Maswali ya Biblia, UncategorizedSABURI KATIKA BIBLIA ni uwezo wa kukubali mateso, dhiki, na shida kwa ajili ya Mungu, ni uwezo wa kuvumilia ukawiaji wa ahadi kutoka kwa Mungu, pasipo kuchoka na wala kupoteza imani na tumaini kutoka kwa Mungu, na ahadi kubwa na ya thamani tunayoingojea kutoka kwa Mungu, ni kuurithi uzima wa milele katika Yesu Kristo Bwana wetu.

Sasa Biblia inasema…

Waebrania 10:36 Maana mnahitaji SABURI, ili kwamba mkiisha kuyafanya mapenzi ya Mungu MPATE ILE AHADI. 

Kumaanisha kuwa, ili tuipate hiyo ahadi, hatuna budi kufanya mapenzi ya Mungu (Mathayo 7:21). Lakini  kuyafanya mapenzi ya Mungu sio kitu rahisi na chepesi kama wengi wetu leo hii tunavyodhani. Biblia inasema kuwa, tunapaswa tuwe na SABURI katika kuyafanya mapenzi ya Mungu, ikimaanisha kwamba, pale tutakapoamua tu! Kuwa ndani ya Kristo na Kuyafanya mapenzi ya Mungu na kumgeukia yeye kwa mioyo yetu yote, basi, hapo tutapitia shida, mateso, dhiki na dhihaka, kutanga tanga huko na huko tukiwa wahitaji na kuonekana kama watu waliorukwa na akili, hivyo hatuna budi kuwa na SABURI tutakapopitia hivi vyote.


Pale tutakapoamua kuyafanya mapenzi ya Mungu kwa kuacha dhambi na uovu wote, hatuna budi kuwa na SABURI kwani tutapitia shida na taabu hapa duniani, pengine hata kutoka kwa ndugu zetu na marafiki zetu, kwani yeyote atakayeamua kuishi hayo maisha ya utakatifu katika Kristo Yesu, hana budi kupitia hayo.

2 Timotheo 3:12  Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa. 


Kristo mwenyewe kama njia ya kufuatwa na mfano wa kuigwa na watu wote wamfuatao, alipitia hivyo vyote. Alipitia dhihaka, kutukanwa, na kukataliwa na watu wa taifa lake mwenyewe, lakini katika hayo yote alikuwa na SABURI katika kuyastahimili mateso akiyafanya yale yote yampendezayo Mungu. 


Hata Mitume wake na wanafunzi wake wote pia, wakiifuata njia hiyo hiyo, walistahimili mateso kwa SABURI,  huku wakipigwa kwa mawe na mapigo mbali mbali hadharani, waliburutwa na kutupwa magerezani wakionekana kama ni watu waliokuwa wasaliti na wenye wazimu, lakini walidumu katika imani wakiyafanya yote yampendezayo Mungu kwa SABURI


Hata mimi na wewe tulioamua kuchukua misalaba yetu kila siku na kumfuata Yesu Kristo, hatuna budi kupitia hayo na wala tusivunjike moyo tupitiapo mambo kama hayo, bali, tunahitajika kuwa na  SABURI ilimradi tu!   tupo katika njia sahihi ya Mungu na kuyafanya yampendezayo yeye, maana hatuna budi kuuingia ufalme wa Mungu kwa njia hiyo kama maandiko yanavyosema katika…

Matendo Ya Mitume 14:22  wakifanya imara roho za wanafunzi na kuwaonya wakae katika ile Imani, na ya kwamba IMETUPASA KUINGIA KATIKA UFALME WA MUNGU KWA NJIA YA DHIKI NYINGI. 

Kinyume chake tunapaswa kufurahi  katika huo uvumilivu wetu, tukijua kuwa ni udhihirisho wa kuwa,  Roho wa Bwana yupo pamoja nasi…

1 Petro 4:14  Mkilaumiwa kwa ajili ya jina la Kristo ni heri yenu; kwa kuwa Roho wa utukufu na wa Mungu anawakalia. 

Lakini kama upo nje ya Kristo na unapitia mateso na dhiki, basi fahamu kuwa saburi yako ni bure, hivyo tubu leo dhambi zako kwa kumaanisha na kumgeukia Muumba wako.

Tafadhari washirikishe na wengine ujumbe huu

Ikiwa utakuwa na swali lolote kuhusu biblia, basi, wasiliana nasi kwa namba hizi

+255652274252/ +255789001312

Bwana akubariki, Shalom.MADA ZINGINEZO:

Nini maana ya mstari huu “Nimesulubiwa pamoja na Kristo?” (Wagalatia 2:20)


KWANINI MAKUHANI WALIAMRIWA KUTWAA MKE MWANAMKE AMBAYE NI BIKIRA TU? (Walawi 21:14)


YOSHUA MWANA WA NUNI.


Kwanini Gombo la chuo lililokunjuliwa mbele ya nabii Ezekiel likikuwa limejaa maombolezo, na vilio na Ole ndani yake? (Ezekieli 2:10).


NANYI KWA SUBIRA YENU MTAZIPONYA NAFSI ZENU


KAMA YOSHUA ANGALIWAPA RAHA, ASINGALIINENA SIKU NYINGINE BAADAE. 


AKASEMA YASIYO FAA KWA MIDOMO YAKE.HATAINGIA NDANI YAKO ASIYETAHIRIWA.

11 thoughts on - SABURI NI NINI KATIKA BIBLIA?

LEAVE A COMMENT