Kwanini Gombo la chuo lililokunjuliwa mbele ya nabii Ezekiel likikuwa limejaa maombolezo, na vilio na Ole ndani yake? (Ezekieli 2:10).

Maswali ya Biblia, Uncategorized No Comments

Tusome.

Ezekieli 2:9 Nami nilipotazama, mkono ulinyoshwa kunielekea; na tazama, gombo la chuo lilikuwa ndani yake. 

10 AKALIKUNJUA MBELE YANGU; nalo lilikuwa limeandikwa ndani na nje; NDANI YAKE YALIKUWA YAMEANDIKWA MAOMBOLEZONA VILIONA OLE

JIBU: Kwanza kabisa inatakiwa tufahamu kitu kimoja, kuwa, Mungu alipolikunjua gombo hilo la chuo mbele ya nabii Ezekieli, haina maana kwamba haliishia pale kulikunjua tu halafu basi, la hasha! Bali aliendelea mbele zaidi kwa kumlisha nabii Ezekieli gombo hilo, na baada ya kumlisha, akamwambia aende akaseme na wana wa Israeli.

Ezekieli 3:1 AKANIAMBIAMWANADAMUKULA UONACHOKULA GOMBO HILIKISHA ENENDA UKASEME NA WANA WA ISRAELI

2 Basi nikafunua kinywa changu, NAYE AKANILISHA LILE GOMBO

Lakini si nabii Ezekieli tu, hata mtume Yohana pia na yeye alikula kitabu, soma (Ufunuo 10:10), na baada ya kukila kitabu hicho, mtume Yohana na yeye alitumwa kama tu ilivyokuwa kwa nabii Ezekieli alivyotumwa kwa wana wa Israeli baada ya kulishwa lile gombo, ndivyo na mtume Yohana naye alivyotumwa baada ya kukila kile kitabu na kuambiwa kwamba, imempasa kutoa unabii tena juu ya watu na taifa na lugha na wafalme.

Ufunuo 10:10 Nikakitwaa kile kitabu kidogo katika mkono wa malaika yule, nikakila; nacho kikawa kitamu kama asali kinywani mwangu, na nilipokwisha kukila tumbo langu likatiwa uchungu. 

11 Wakaniambia, IMEKUPASA KUTOA UNABII TENA JUU YA WATU NA TAIFA NA LUGHA NA WAFALME

Maana yake ni nini? 

Maana yake ni kuwa, Mungu anapomtuma mtumishi wake, huwa anamlisha maneno yake, au huwa anaweka ujumbe Wake au maneno Yake ndani ya mtumishi huyo anayemtuma sehemu husika, mfano nabii Yeremia.

Yeremia 1:7 Lakini Bwana akaniambia, Usiseme, Mimi ni mtoto; maana UTAKWENDA KWA KILA MTU NITAKAYEKUTUMA KWAKENAWE UTASEMA KILA NENO NITAKALOKUAMURU

8 Usiogope kwa sababu ya hao maana mimi nipo pamoja nawe nikuokoe, asema Bwana. 

9 Ndipo Bwana akaunyosha mkono wake, akanigusa kinywa changu; BWANA AKANIAMBIATAZAMANIMETIA MANENO YANGU KINYWANI MWAKO

Lakini ni kwanini maneno hayo yawe yamejaa au kushamiri maombolezo, na vilio, na ole kama alivyoona nabii Ezekieli?

Ezekieli 2:10 AKALIKUNJUA MBELE YANGU; nalo lilikuwa limeandikwa ndani na nje; NDANI YAKE YALIKUWA YAMEANDIKWA MAOMBOLEZONA VILIONA OLE

Hii ni kutufundisha kwamba, Mungu kamwe hajawahi mtuma mtumishi wake yo yote yule duniani kwenda kuwahubiria watu mafanikio na faraja wakati wanafanya machukizo mbele zake, badala yake ni maombolezo, vilio, na ole kwa kututaka wanadamu tugeuke katika njia zetu mbovu na Matendo yetu ya dhambi kwa kumgeukia Yeye na kumtii na kumtumikia, hivyo Ndivyo ilivyokuwa tangia wakati wa Henoko, Nuhu, Musa, na manabii kama wakina Yona, Hosea na Yohana mbatizaji, au wahubiri wa injili kama wakina Filipo, Paulo, Petro n.k


Hawa wote jumbe zao zilijaa hukumu na ghadhabu ya Mungu kwa kututaka wanadamu tutubu na kumgeukia Mungu ili tupate msamaha wa dhambi zetu.

Matendo 2:38 Petro akawaambia, TUBUNI MKABATIZWE KILA MMOJA KWA JINA LAKE YESU KRISTOMPATE ONDOLEO LA DHAMBI ZENU, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. 

Soma tena.

Matayo 3:2 TUBUNIKWA MAANA UFALME WA MBINGUNI UMEKARIBIA

Soma tena.

2 Wathesalonike 1:8 katika mwali wa moto; huku akiwalipiza kisasi wao wasiomjua Mungu, na wao wasioitii Injili ya Bwana wetu Yesu; 

9 watakaoadhibiwa kwa maangamizi ya milele, kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa nguvu zake; 

Hivyo ukiona unahubiriwa na mtumishi yo yote yule habari za mafanikio na kuuburudisha moyo wako, majumba na magari, kufunguliwa kiuchumi na biashara, baraka na miujiza, mafuta ya upako n.k, na huku ni mzinzi na mwasherati, mtukanaji na mlevi, mpenda anasa na starehe, mwenda kwa waganga na mchawi, mwabudu sanamu na muomba wafu, mvaaji vimini na suruali kwa mwanamke (Mavazi ya kikahaba), Mtoaji mimba, makucha bandia, rasta, mawigi, make up, kujichubua, lipstick n.k,  (yaani kwa ufupi hufundishwi kuitii injili ya kweli ya Utakatifu ya Kristo).

Basi tambua kuwa, huyo mtumishi hakutumwa na Mungu wa Ibrahimu, na Isaka na Yakobo, la sivyo, ameshindwa kuwa mwaminifu katika kweli ya neno la Mungu (maandiko matakatifu), au ametumwa na mungu wake mwenyewe ambaye tumbo lake.

Wafilipi 3:18 Maana wengi huenenda, ambao nimewaambieni mara nyingi habari zao, na sasa nawaambia hata kwa machozi, kuwa ni adui za msalaba wa Kristo; 

19 mwisho wao ni uharibifu, MUNGU WAO NI TUMBOUTUKUFU WAO U KATIKA FEDHEHA YAOWANIAO MAMBO YA DUNIANI

Bwana akubariki, Shalom.

Tafadhari washirikishe na wengine habari hii njema.

+255652274252/ +255789001312


Mada zinginezo:

Je! Mtu anaweza kuwa na kipawa cha Mungu kabisa na Bado akawa mtumishi wa uongo?


KAZI NYINGINE YA MAANDIKO MATAKATIFU KWA WAFUASI WA YESU KRISTO (SEHEMU YA KWANZA).


NAONA KUNA SINTOFAHAMU KUHUSU KRISMASI, HIVI NI KWELI IPO KWENYE MAANDIKO?


NAO WALIOPOKEA NENO LAKE WAKABATIZWA.


Je! Ni dhambi kwa mwanamke wa Kikristo kuvaa suruali?


LAKINI NABII ATAKAYENENA NENO KWA KUJIKINAI KWA JINA LANGU, AMBALO SIKUMWAGIZA KULINENA, AU ATAKAYENENA KATIKA JINA LA MIUNGU MINGINE, NABII YULE ATAKUFA.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *