KUWA NA TABIA HII YA NUHU KATIKA NYAKATI HIZI ZA UOVU ILI UPATE KUSALIMIKA NA GHADHABU YA MUNGU.

Biblia kwa kina, Uncategorized 6 Comments

Jina la Bwana na Mwokozi Wetu Yesu Kristo litukuzwe milele na milele, karibu tujifunze neno la Mungu Wetu maadamu saa ya wokovu wetu ipo karibu nasi Kama mtume Paulo alivyoandika katika.

Warumi 13:11 Naam, tukiujua wakati, kwamba saa ya kuamka katika usingizi imekwisha kuwadia; KWA MAANA SASA WOKOVU WETU U KARIBU NASI KULIKO TULIPOANZA KUAMINI

Kama mfuasi wa Yesu Kristo (wewe uliyetubu dhambi zako kwa kumwamini na kuzaliwa upya kwa maji na Roho sawasawa na maandiko), na wewe ambaye bado hujafanya hivyo sasa, ipo tabia moja ya Nuhu ambayo unapaswa kuwa nayo sasa hivi katika nyakati hizi za uovu ili upate kuwa salama na ghadhabu ya Mungu inayokuja kwa sababu, dunia ya wakati ule wa Nuhu iliangamizwa kwa maji, bali hii ya sasa tuliyopo mimi na wewe imewekwa akiba kwa moto na kwa kuangamizwa kwa wanadamu wote wasiomtii Mungu.

2 Petro 3:6 kwa hayo dunia ile ya wakati ule ILIGHARIKISHWA NA MAJIIKAANGAMIA

LAKINI MBINGU ZA SASA NA NCHI ZIMEWEKWA AKIBA KWA MOTO, KWA NENO LILO HILOZIKILINDWA HATA SIKU YA HUKUMUNA YA KUANGAMIA KWAO WANADAMU WASIOMCHA MUNGU

Hivyo basi, ili uwe Salama, huna budi kuwa na tabia kama ya Nuhu tunayoisoma, ambayo iliyomfanya Nuhu kuokoka yeye na nyumba yake na ghadhabu ya Mwenyezi, kwa sababu habari ya tabia hiyo ya Nuhu iliandikwa kwa jinsi ya mfano, ili kutufundisha sisi watu wa sasa (Warumi 15:4), na tabia hiyo ya Nuhu ambayo unayopaswa kuwa nayo sasa  si nyingine zaidi ya “KWENDA PAMOJA NA MUNGU”

Tunasoma..

Mwanzo 6:9 Hivi ndivyo vizazi vya Nuhu. Nuhu alikuwa mtu wa haki, mkamilifu katika vizazi vyake; NUHU ALIKWENDA PAMOJA NA MUNGU

Umeona hapo tabia hiyo ya Nuhu iliyoelezwa na maandiko? Kwamba Nuhu alikwenda pamoja na Mungu? Ndugu mpendwa, ukitaka kuwa salama na ghadhabu ya Mungu iliyotayari kuujia ulimwengu katika nyakati hizi tulizopo zenye uovu uliokithiri ule uliokuwa ukifanyika wakati wa Nuhu, huna budi KWENDA PAMOJA NA MUNGU (kuwa kama Nuhu), huu si wakati wa kwenda pamoja na wengi kwa kutazama mamia ya watu wanafanya nini, bali ni wakati wa wewe KWENDA PAMOJA NA MUNGU.


Ni wakati wa kuwa na tabia hii ya Nuhu kwa kwenda pamoja na Muumba wako ili uwe Salama bila kujali wewe ni nani, vinginevyo utaangamia, kwa sababu wakati wa Nuhu walikuwapo watu kama wewe, walikuwepo vijana wenye nguvu kama wewe, Walikuwepo mabinti wazuri na warembo kama wewe, walikuwepo Vikongwe na wazee kama wewe, walikuwepo mayatima na wajane kama wewe, walikuwepo maskini na matajiri kama wewe, walikuwepo majemedari wa vita na mashujaa kama wewe, walikuwapo watu wanyonge kama wewe, walikuwapo wasomi na wenye hekima kama wewe, walikuwapo wenye vyeo, sifa na umaarufu kama wewe, walikuwepo wakuu wa nchi (wafalme n.k) kama wewe ulivyo mkuu wa nchi leo hii, walikuwepo mawaziri na magavana kama wewe, walikuwepo wanaojiita viongozi wa dini kama wewe. 


Lakini hao wote waliangamia kwa ile gharika kama tunavyofahamu, kwa sababu walikuwa waovu kwa kukataa kwenda pamoja na Mungu bali matendo yao na tamaa zao.

Ndivyo itakavyokuwa katika mbingu na nchi hizi za sasa, Mungu atazigharikisha (lakini si kwa maji tena bali kwa moto), na kuwaangamiza wale wote wasiomcha Mungu.

2 Petro 3: 7 LAKINI MBINGU ZA SASA NA NCHI ZIMEWEKWA AKIBA KWA MOTO, KWA NENO LILO HILOZIKILINDWA HATA SIKU YA HUKUMUNA YA KUANGAMIA KWAO WANADAMU WASIOMCHA MUNGU

Hivyo basi, ili usalimike na hukumu hiyo ya Bwana, huna budi kuwa na tabia hiyo ya Nuhu sasa katika maisha yako kwa kwenda pamoja na Mungu.


Sasa nini maana ya kwenda pamoja na Mungu? Au unaanzaje kwenda pamoja na Mungu?


Kama Wewe upo ndani ya Kristo, yaani umeshatubu dhambi zako na kubatizwa katika Ubatizo sahihi na kupokea Roho Mtakatifu aliye muhuri wake Mungu, unachopaswa kufanya ni kudumu katika mafundisho matakatifu ya Mungu, (Injili iliyohubiriwa na mitume na manabii), pasipo kwenda kulia wala kushoto.


Lakini Kama bado haupo ndani ya Kristo, yaani hujafanya hivyo, Unachotakiwa kufanya ni kutubu dhambi zako kwa kumwamini Yesu Kristo, na kwenda kubatizwa katika Ubatizo sahihi Sawasawa na maandiko, nawe utapokea kipawa cha Roho Mtakatifu, kisha kaa ndani ya Kristo kwa kudumu kwa uaminifu wote katika utakatifu kama injili ya Kristo inavyoagiza, na kwa kufanya hivyo hukumu ya adhabu haitakuwa juu yako kama biblia inavyosema.

Warumi 8:1 Sasa, basi, HAKUNA HUKUMU YA ADHABU JUU YAO WALIO KATIKA YESU KRISTO

Kumbuka: Unapokataa kwenda pamoja na Mungu leo hii katika maisha yako kwa kuwa ndani ya Yesu Kristo na kuitii Injili yake, maana yake ni kuwa, moja kwa moja wewe mwenyewe binafsi unaukataa na kuutupilia mbali uzima wako wa milele.

Bwana akubariki, Shalom.

Tafadhari washirikishe na wengine habari hii njema.

+255652274252/ +255789001312


Mada zinginezo:

Akaifanya iwe ishara kwa watu watakaokuwa hawamchi Mungu baada ya haya.


Kwanini Kuzimu kuongeze tamaa yake na kufunua kinywa chake bila kiasi? (Isaya 5:14).


JIFUNZE TABIA HII KUTOKA KWA MITUME ANDREA NA FILIPO.


Jifunze tabia hii kutoka kwa mtume Paulo.


MCHUNGAJI WAKO NI NANI?


JINSI AMRI YA UPENDO INAVYOWAFANYA WATU WADUMU KATIKA DHAMBI

6 thoughts on - KUWA NA TABIA HII YA NUHU KATIKA NYAKATI HIZI ZA UOVU ILI UPATE KUSALIMIKA NA GHADHABU YA MUNGU.
  1. Mara nyingi uwa napanga ratiba yangu yakuomba, sasa uwanatoka nyumbani na kwenda kusali chumbani kwangu je jambo hili ninjema?

  2. Jibu ni Ndio, na wala halina shida, kwani maandiko yenyewe yanasema

    Matayo 6:6 Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.

  3. sawa lakini vipi mtu akiwa mtakatifu lakini anashiriki katika nanisa lisilo na uamsho au tuseme lisilo kiroho anaweza kosa ufalme wa mbinguni na alikuwa mtakatifu?

  4. na pia kanisa letu lamaali linachangamoto nyingi maana kuna wanawake wanaingia wakisukia mesh zakila aina nawengine vijana wamenyolewa mitindo na jambo hili liko katika makanisa mengi au yote hapa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *