MCHUNGAJI WAKO NI NANI?

Biblia kwa kina, Uncategorized No Comments

Mchungaji wako ni nani? Je! Ni Bwana (Yesu Kristo), ndiye aliye mchungaji wako? Au ni Ibilisi ndiye aliye mchungaji wako?

Shalom, jina la Bwana na Mwokozi Wetu Yesu Kristo litukuzwe, sifa na Utukufu ni vyake milele na milele, Amina. 

Leo hii kwenye dunia tunayoishi, imekuwa ni kitu cha kawaida kwa takribani kila mtu anayejiita mkristo kusema, “Bwana ndiye Mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu” pasipo kuwa na maarifa na ufahamu wa maandiko hayo.

Zaburi 23:1 BWANA NDIYE MCHUNGAJI WANGU, Sitapungukiwa na kitu. 

Katika hali ya kawaida, hakuna mtu yoyote  yule anayeweza kukana kwamba, Bwana siye Mchungaji wake, hata manabii na waalimu wa uongo hawawezi kukana hicho, utawasikia tu wakisema hivyo hivyo, “Bwana ndiye Mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu” na huku mioyoni mwao wakifahamu kabisa kama wao ni watumishi wa uongo, lakini pia sio hao tu, hata kijana aliyetoka kufanya uasherati dakika chache nyuma, naye atasema vivyo hivyo, binti aliyetoka kutoa rushwa ya ngono saa moja nyuma, naye atasema kitu hicho hicho, au mwanamume aliyetoka nje ya ndoa yake dakika tano  nyuma, na yeye atasema vivyo hivyo, hawezi kana kwamba Bwana siye Mchungaji wake, mtu aliyetoka kwa mganga wa kienyeji, mtu aliyetoka kunywa pombe na kuvuta sigara, kiongozi dhalimu na mpokea rushwa pia, wote hawawezi kana kwamba, Bwana siye Mchungaji wao, kila mtu atakwambia Bwana ni Mchungaji wake, kwa sababu ndivyo ilivyo.


Lakini je! Kitu hicho ni sahihi kwamba, Bwana ni Mchungaji wa kila mtu kama tunavyodhani? Jibu ni hapana, hayo ni mawazo yasiyo sahihi yetu sisi wanadamu, ambayo tunayojifariji nayo kwa kukosa maarifa, biblia inatuambia kuwa, Bwana si Mchungaji wa kila mtu, (MBUZI NA KONDOO), hapana! bali ni MCHUNGAJI WA KONDOO TU, na sio Mchungaji wa mbuzi.

Waebrania 13:20 Basi, Mungu wa amani aliyemleta tena kutoka kwa wafu MCHUNGAJI MKUU WA KONDOO, kwa damu ya agano la milele, yeye Bwana wetu Yesu, 

Soma tena

Yohana 10:16 NA KONDOO WENGINE NINAO, ambao si wa zizi hili; na hao nao imenipasa kuwaleta; na sauti yangu wataisikia; KISHA KUTAKUWAKO KUNDI MOJA NA MCHUNGAJI MMOJA.

Umeona hapo?..lakini pia wapo na mbuzi (Mathayo 25:33), ambao na wao pia wanao mchungaji wao kama vile kondoo walivyokuwa na mchungaji wao, na mchungaji wa mbuzi si mwengine zaidi ya ibilisi. Sasa je! Mchungaji wako wewe ni nani kati hao? Ni Yule Mchungaji wa kondoo au wa mbuzi? Je! Wewe ni mbuzi au kondoo? Na je! Kondoo ni nani na mbuzi nani?


Kondoo ni wale wote walio wa uzao wa Ibrahimu kwa imani (Wagalatia 3:7), taifa la Israeli, walio mwamini Yesu Kristo na kubatizwa kwa jina lake, Na ndio maana ukisoma maandiko, utaona sehemu kadha wa kadha Mungu akilifanisha taifa la Israeli, uzao wa Ibrahimu kimwili na kondoo (1 Wafalme 22:17), kufunua kuwa, wale walio wa uzao wa Ibrahimu rohoni au kwa imani ndio kondoo wa Bwana, walio mwamini Yesu Kristo na kubatizwa katika jina lake, na kuishi maisha ya utakatifu na kutembea katika mapenzi yake.

Lakini kinyume cha hayo ni kweli, ukijiona hadi leo hii hujatubu dhambi zako na kubatizwa katika ubatizo sahihi ambao ni wa maji tele na kwa jina la Yesu Kristo (Matendo 2:38), na kibaya zaidi unapinga, na maisha yako ni ya dhambi na hutembei katika mapenzi ya Mungu, kusema uongo na kutukana ni wewe, kulaani watu na kuwasengenya ni wewe, anasa za ulimwengu, miziki ya kidunia, pombe, sigara, kubet, ni wewe, mavazi ya kikahaba mwanamke ni wewe, fashion, kwenda kwa waganga, kusujudia sanamu na kuwaomba watu waliokufa ni wewe, na huku unakazana kusema, Bwana ni Mchungaji wako hutopungukiwa na kitu. Ndugu yangu mpendwa, tambua kuwa unajidanganya, kwa sababu Bwana hachungi watu wa aina hiyo bali ibilisi, Bwana Yeye ni Mchungaji wa kondoo na si mbuzi, Unachotakiwa kufanya ni kutubu dhambi zako leo na kumgeukia Mchungaji Mkuu wa kondoo, na kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi na wa kimaandiko, ili Bwana awe Mchungaji wako

1 Petro 2:25 Kwa maana mlikuwa mnapotea kama kondoo; lakini sasa mmemrudia Mchungaji na Mwangalizi wa roho zenu. 

Tafadhari washirikishe na wengine ujumbe huu.

Bwana akubariki, Shalom.

+255652274252/ +255789001312


Mada zinginezo:

Makuhani wa Mungu ni watu gani katika biblia?


AKAJIBU AKASEMA, NAENDA, BWANA; ASIENDE.


AKASEMA YASIYO FAA KWA MIDOMO YAKE.


Msaidizi wa kufanana naye ni nani ambaye Mungu alimfanyia Adamu? (Mwanzo 2:18)


Bwana alimaanisha nini aliposema “Heri ayawe yote asiyechukizwa nami?” (Mathayo 11:6)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *