Msaidizi wa kufanana naye ni nani ambaye Mungu alimfanyia Adamu? (Mwanzo 2:18)

  Maswali ya Biblia, Uncategorized

SWALI: Biblia inasema kuwa, Mungu alipomuumba mtu wa kwanza Adamu, aliona si vyema awe peke yake, hivyo akamfanyia msaidizi wa KUFANANA NAYE, je! Msaidizi huyo wa kufanana naye ni nani?

Mwanzo 2:18 Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia MSAIDIZI WA KUFANANA NAYE

JIBU: Msaidizi wa kufanana naye ambaye Mungu alimuumbia mwanamume (Adamu) ni mwanamke (Hawa), na wala si mwanamume mwenzake Adamu, tunalithibitisha hilo katika kitabu hicho cha Mwanzo

Mwanzo 2:20 Adamu akawapa majina yao kila mnyama wa kufugwa, na ndege wa angani, na kila mnyama wa mwituni; lakini HAKUONEKANA WA KUMSAIDIA ADAMU ALIYEFANANA NAYE.

 21 Bwana Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake, 

22 na ule ubavu alioutwaa katika Adamu Bwana Mungu AKAUFANYA MWANAMKE, AKAMLETA KWA ADAMU. 

Umeona hapo msaidizi wa kufanananaye ambaye Mungu alimuumbia mwanamume ni mwanamke (Hawa)?


Sasa nini maana ya WA KUFANANA NAYE 

Jibu ni kwamba? Mungu aliviumba viumbe vyote wawili wawili kwa jinsi zao kwa lengo la kuzaliana (Mwanzo 1:22), yaani kama ni simba dume basi na jike, njiwa dume na jike, swala dume na jike, kuku dume na jike, kambale dume na jike, kila kiumbe na mwenzake wa wakufanana naye.

Mwanzo 1:25 Mungu akafanya mnyama wa mwitu KWA JINSI ZAKE , na mnyama wa kufugwa KWA JINSI ZAKE, na kila kitu kitambaacho juu ya nchi KWA JINSI YAKE; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. 

Sasa katika hali hiyo pale bustani ya Edeni, Adamu hakuwa na mwenzake wa kufanana naye yaani mwanamke, kama vile ilivyokuwa kwa hao viumbe wengine, ndipo sasa Mungu akasema si vema mtu huyu (mwanamume) awe peke yake, nitamfanyia msaidizi WA KUFANANA NAYE (mwanamke), kama ilivyokuwa kwa viumbe wengine kwa lengo lile lile la kuzaliana. 


Mwanzo 1:28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, ZAENI, MKAONGEZEKE, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi. 


Wapo watu wengi leo hii duniani wanaotumia andiko hilo la (Mwanzo 2:18), kuhalarisha mahusiano au ndoa za jinsia ya kiume na kiume (ushoga), kwa kisingizio kuwa, kama Adamu alikuwa mwanamume, na Mungu alimuumbia mwenzake wa kufanana naye, sasa huyo wa kufanana naye ni nani kama sio mwanamume mwenzake? Huo ni uongo na upotoshaji mkubwa wa sheria ya Mungu.

Biblia inasema katika..

Walawi 18:22 USILALE NA MWANAMUME MFANO WA KULALA NA MWANAMKE; NI MACHUKIZO. 

Na WACHUKIZAO WOTE wakiwemo wanaofanya kitendo hicho bila kujali ni maskini kiasi gani au ni tajiri kiasi gani, sehemu yao ni katika ziwa liwakalo moto milele na milele, (ufunuo 21:8), hivyo basi, kama na wewe unayesoma ujumbe huu ni mmoja wapo wa hao wanaofanya hicho kitendo basi ACHA MARA MOJA, acha mara moja na uutubie uovu huo na uovu wako wote kwa kumwamini Yesu Kristo, kuwa ni Bwana na Mwokozi wa maisha yako, na kisha kwenda kubatizwa katika maji tele na kwa jina lake, nawe utapata msamaha wa dhambi zako zote kabisa sawasawa na (Matendo 2:38)


Lakini ikiwa wewe ni mkristo, umeokoka na kubatizwa katika jina lake Yesu Kristo, tambua kuwa, hupaswi kushiriki kwa namna yoyote ile katika ndoa hiyo chafu ya jinsia moja na ya machukizo, hupaswi kwenda kanisani wala ukumbini, hupaswi hata kushona nguo za harusi kwa ajili ya ndoa hiyo ya machukizo kama wewe ni mshonaji, hupaswi kwenda kupamba kwenye ndoa hiyo ya machukizo kama wewe ni mpambaji, hupaswi kwenda kupika chakula kwenye ndoa hiyo ya machukizo kama wewe ni mpishi, na pia hupaswi hata kutengenzena keki kwenye ndoa hiyo ya machukizo kama wewe ni mtengenezaji keki, kwani kwa kufanya hivyo utakuwa UNAKUBALIANA NAO KATIKA MACHUKIZO YAO kama biblia inavyosema.

Warumi 1:32 ambao wakijua sana hukumu ya haki ya Mungu, ya kwamba wayatendao hayo wamestahili mauti, wanatenda hayo, wala si hivyo tu, BALI WANAKUBALIANA NAO WAYATENDAO.

Bwana akubariki, Shalom.

Tafadhari washirikishe na wengine ujumbe huu.

+255652274252/ +255789001312


Mada zinginezo:

Akaifanya iwe ishara kwa watu watakaokuwa hawamchi Mungu baada ya haya.IJAPOKUWA NALIWAUZUNISHA KWA WARAKA ULE, SIJUTI


Kwanini Bwana Yesu alijeruhiwa ubavuni pale msalabani?


NIFANYE NINI KAMA MKRISTO ILI MUNGU ANIONGEZEE IMANI KWAKE?


Mkia wa joka kubwa jekundu anaoutumia kuziangusha nyota chini ni nini? (Ufunuo 12:4)

LEAVE A COMMENT