IJAPOKUWA NALIWAUZUNISHA KWA WARAKA ULE, SIJUTI

  Biblia kwa kina, Uncategorized

Shalom, jina la Bwana Wetu na Mwokozi Wetu Yesu Kristo litukuzwe, sifa na Utukufu ni vyake milele na milele. Amina! Karibu tujifunze neno la Mungu, taa ya miguu yetu.


Mtume Paulo aliandika maneno haya katika waraka wake wa pili kwa Wakorintho 

2 Wakorinto 7:8  Kwa sababu, IJAPOKUWA NALIWAHUZUNISHA KWA WARAKA ULE, SIJUTI; hata ikiwa nalijuta, naona ya kwamba waraka ule uliwahuzunisha, ingawa ni kwa kitambo tu.

Mtume huyu wa Bwana Yesu aliye jaaliwa kupokea mafunuo mengi na kufanya kazi kwa neema ya Mungu kuliko mitume wote waliomtangulia (1 Wakorintho 15:10), alipoona kuwa kuna baadhi ya watu wanafanya mambo tofauti na Kristo alivyoagiza katika kanisa huko Korintho, alichukua jukumu la kuwaambia ukweli watu hao pasipo kukawia (ukweli huo unapatikana katika waraka wake wa kwanza kwa Wakorintho), lakini kama tunavyofahamu siku zote kuwa, ukweli huwa unaumiza sana na wala haufurahishi hata kidogo, ukweli unaweza ukakufanya hata utengane na ndugu, na hata jamaa wa karibu kabisa na pengine hata kuchukiwa, lakini hilo halikumzuia mtume Paulo kusema ukweli, aliwaambia ukweli na pia alisema HAJUTUI KWA KUWAAMBIA UKWELI HUO kwani alifahamu kabisa kuwa, endapo hatowaweka wazi watu hao mwisho wao utakuwa mbaya, watakufa na kwenda Jehanamu ya moto. 

 Ijapokuwa watu hao walijisikia vibaya sana na kukasirika baada ya kuambiwa ukweli, hatimaye walitubu na kurudi katika njia ya Mungu, hivyo ikawa faida kwa roho zao

2 Wakorinto 7:9  Sasa nafurahi, si kwa sababu ya ninyi kuhuzunishwa, BALI KWA SABABU MLIHUZUNISHWA, HATA MKATUBU. Maana mlihuzunishwa kwa jinsi ya Mungu, ili msipate hasara kwa tendo letu katika neno lo lote. 

Jambo hili hili pia linaendelea sasa hivi siku hizi za mwisho katika kanisa la Kristo, kuna watumishi wengi sana sasa hivi ambao Mungu amewapa maarifa yake ya kutosha  juu ya vigezo vya kanisa la Kristo na watu wanapaswa waweje mbele za Mungu, lakini watumishi hao wanaogopa kusema ukweli huo ndani ya kanisa na kwa watu wengine ambao bado hawajamfahmu Mungu kwa sababu tu! Wanaogopa kuwaumiza mioyo na kuwahuzunisha watu hao, wanaogopa kusema uzinzi wako utakupeleka Jehanamu ya moto usipotubu, miziki ya kidunia itakupeleka jehanamu ya moto, suruali zako, vimini vyako na vimapambo vyako vitakupeleka Jehanamu ya moto, kuabudu sanamu kwako na kuwaomba wafu kutakupeleka Jehanamu, maisha unayoishi na mume/mke wa mtu au  mwanamume unayeishi nae huku hamjafunga ndoa si sawa mbele za Mungu utaenda jehanamu usipotaka kurekebisha. Mambo haya na mengine mengi wanahofia kuyasema kwa sababu tu hawataki kuwaumiza watu na kuwahuzunisha mioyo yao.


Ndugu, ikiwa utaogopa au kuhofia leo hii kusema kweli ya Mungu, basi tambua kwamba, hutokuwa umewasaidia chochote watu hao kwa kutaka kutokuwahuzunisha, wewe waambie ukweli bila kujari utawaumiza au la! Waambie Mungu anachukia hiki na anapenda hiki, na wala usijute, waambie ukweli ili warekebisha njia zao mbele za Mungu kwani huwezi jua huenda wakatubu na kuitii injili ya Mungu kama watu wa Korintho

Tafadhari washirikishe na wengine habari hii njema.

Bwana akubariki, Shalom.

+255652274252/ +255789001312


Mada zinginezo:

KWA SABABU NALIWAOGOPA WALE WATU, NIKATII SAUTI YAO. 
 

Je! Waraka wa mtume Paulo kwa Wakorintho, ulikuwa ni kwaajiri ya Wakorintho pekee?


Ni hukumu ipi ya Ibilisi inayozungumziwa katika Waraka wa (1 Timotheo 3:6?)


DUMU KATIKA FUNDISHO LA MITUME.


USITUMAINIE HEKALU LA BWANA

3 thoughts on - IJAPOKUWA NALIWAUZUNISHA KWA WARAKA ULE, SIJUTI

LEAVE A COMMENT