NIFANYE NINI KAMA MKRISTO ILI MUNGU ANIONGEZEE IMANI KWAKE?

  Maswali ya Biblia, Uncategorized

Ulishawahi kujiuliza swali kama hilo au swali linalofanna na hilo? Au ulishawahi kutamani kitu kama hicho kutoka kwa Bwana? Kama jibu ni ndio, basi fahamu kuwa wewe sio wa kwanza, kwani hata mitume wake waliotembea nae na kula walishawahi omba kitu kama hicho kutoka kwake.

Luka 17:5  MITUME WAKAMWAMBIA BWANA, TUONGEE IMANI.

Lakini Bwana aliwafundisha na kuwajibu kwa mfano, ambao na sisi kama wakristo hatuna budi kuzingatia ili tuwe na imani kwa Mungu wetu, na yeye awe na imani na sisi, labda tusome kidogo mfano huo wa Bwana katika injili ya luka, na kisha tujifunze nini cha kufanya

Luka 17:7 Lakini, ni nani kwenu mwenye mtumwa alimaye au achungaye ng’ombe, atakayemwambia mara arudipo kutoka shambani, Njoo upesi, keti, ule chakula?

 8 JE! HATAMWAMBIA, NIFANYIE TAYARI CHAKULA, NILE; JIFUNGE UNITUMIKIE, hata niishe kula na kunywa, ndipo nawe utakapokula na kunywa?

 9 Je! Atampa asante yule mtumwa, kwa sababu ameyafanya aliyoagizwa?

 10 Vivyo hivyo nanyi, MTAKAPOKWISHA KUFANYA YOTE MLIYOAGIZWA, semeni, Sisi tu watumwa wasio na faida; tumefanya tu yaliyotupasa kufanya. 

Mitume walipoomba kuongezewa imani na Bwana, walifahamu wazi kabisa kuwa, kila kitu kinatoka kwake, yeye ndiye anayetupatia vitu vyote na tunayaweza yote katika yeye Kristo atutiaye nguvu,  ikiwemo na kutuongezea imani pia. 

Sasa huyo ambaye anayetoa vitu hivyo vyote yaani Bwana Yesu, anawaambia ni nani aliye na mtumwa kwenu harafu akamwambia njoo upumzike tu kwanza ule chakula na kustarehe n.k Bila kumtumikia kwanza? Jibu ni hapana, hakuna bosi kama huyo. 

Kama mtumwa, kuna masharti ambayo anapaswa kuyafanya kwa ajili ya bosi wake kwanza, na bosi anataka kuona kazi yake ikifanyika kwanza na kutumikiwa, hivyo ndivyo ilivyo na kwa Kristo pia kwetu sisi, anataka kuona na sisi tanafanya kwanza tuliyoagizwa ili atupe baraka zake.

Hata katika maisha ya kawaida tu, au hapo kazini kwako, au hata popote pale watu wanapofanyia kazi, utagundua kwamba, ili mkubwa wako wa kazi akuamini, au awe na imani na wewe, huna budi siku zote kuonesha bidii fulani katika hiyo kazi yako, lazima uwe mtendaji kazi na kazi yako ionekana na bosi wako, ama kwa njia ya kujipendekeza au kwa njia yoyote ile, ni lazima uoneshe bidii fulani ili bosi wako aweze kukuamini, na kukupatia hadhi nyingine zaidi tofauti na hiyo kutokana na ufanyaji kazi wako.

Hivyo ndivyo ilivyo na kwa Bwana wetu Yesu Kristo, ili atuongezee vitu katika ukristo wetu ikiwemo na imani, hatuna budi kuonesha bidii katika hali hiyo hiyo tuliyonayo sasa, hatuna budi kufanya kazi yake kwa bidii kwanza ili kazi yetu ionekane mbele zake, hapo ndipo tutakapojiongezea uaminifu wetu kwake na yeye pia kama Bosi atatupatia zaidi na zaidi ikiwemo na imani.


Kazi hizo za Bwana ni zipi tunazotakiwa kuzifanya?


Kazi hizo ni kufanya bidii kujitenga na dhambi na kuishi maisha ya utakatifu kila siku, kuwahubiria wengine habari njema ya wokovu, kuwa wasomaji na watafakariji wa neno kwa bidii kila siku, kuwasaidia wengine wasiojiweza na wenye uhitaji, kuwa wafungaji na waombaji kila siku na kwa bidii. Tukijitahidi katika hayo na bila kuchoka, Mungu atathamini sana na kuwa na imani na sisi, pia ataona uaminifu wetu kwake, hivyo atatujaza na kutubariki rohoni ikiwemo na kutuongezea na imani pia.

 Matayo 17:21 [Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.] 

Kwa mana yoyote ile, tusikate tamaa, tufanye kazi ya Bwana, na kuomba msaada kwa Bwana, ili akuongezee imani na atusaidie kutokuamini kwetu kwani yeye ni mwaminifu sana.

Marko 9:24  Mara babaye yule kijana akapaza sauti, akasema, NAAMINI, NISAIDIE KUTOKUAMINI KWANGU. 

Tafadhari washirikishe na wengine ujumbe huu.

Lakini ikiwa bado hujatubu dhambi zako na  kumpa Kristo maisha yako, na kubatizwa kwa jina lake, basi amua leo kufanya hivyo na kwenda kubatizwa kwa jina lake kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu sawasawa na matendo 19:5

Bwana akubariki, Shalom.

+255 652274252 +255 789001312 +255 755 251 999


Mada zinginezo:

BWANA ALIMAANISHA NINI ALIPOSEMA “HAPA YUPO ALIYE MKUU KULIKO HEKALU?”


Kulingana na ( 1 Petro 4:1) Ni silaha ya nia gani aliyokuwa nayo Kristo ambayo na sisi tunapaswa kujivika? 


Mjumbe wa agano la kwanza alikuwa ni nani?


Ni maungamo gani aliyoyaungama Yesu Kristo mbele ya Pilato?


Ni tabia ipi ya Uungu tutakayoshiriki (kulingana na 2 Petro 1:4)

LEAVE A COMMENT