UMEPATA FAIDA GANI?

  Biblia kwa kina

Umepata faida gani ndugu? 

Umepata faida gani tangu ulipoanza kuvuta sigara hadi sasa hivi? Umepata faida gani? Umepata faida gani zaidi ya kuharibu afya yako ya mapafu na kifua? Umepata faida gani zaidi ya kuambulia TB na kansa? 

Je! Kuna nini cha kujivunia au kuna kitu gani unachoweza kujivunia ulichokipata tangu ulipoanza kuvuta sigara?

Umepata faida gani ndugu?

Umepata faida gani tangu uliopoanza kuwa mnywaji wa pombe na mlevi? Kuna chochote kile cha maana ulichokipata zaidi ya kujishushia heshima katika jamii kwa sifa mbaya ya ulevi? Kuna chochote kile ulichopata zaidi ya kufukuzwa kazi kwa sababu ya ulevi? Kuna chochote ulichopata zaidi ya kufirisika mali zako kwa sababu ya pombe? Kuna chochote cha maana ulichokipata zaidi ya watoto wako kushindwa kulipiwa ada ya shule kwa sababu ya unywaji wako wa pombe? Kuna nini cha maana ulichopata? Ni kitu gani unachoweza kujivunia nacho sasa?


Umepata faida gani katika uzinzi unaoufanya wewe kaka/dada? Umepata faida gani kwa punyeto unazofanya wewe kijana? Umepata faida gani kwa picha chafu za ngono unazozitazama? Umepata faida gani tangu uanze kufanya hivyo? Umepata faida gani kwa hao wanaume na wanawake unaofanya nao uasherati? Umepata faida gani zaidi ya kuambulia mapepo na magongwa ya zinaa? Kualibiwa maisha yako n.k (lakini nataka nikwambie kuwa, unaweza anza upya maisha yako kwa njia moja tu! Wala usizani kuwa umeshapotea na ndio basi tena, lipo tumaini kuu)


Ndugu, umepata faida gani kwa hiyo milegezo unayovaa? Umepata faida gani kwa hicho kiduku na mutindo katika kichwa chako uliyoinyoa? Unadhani wewe ni wa kisasa sana? Haya, Umepata faida tangu ulipoanza kufanya hivyo kijana? Je! Jua halikuchomoza kwa ajili ya usasa wako? Au mwezi ulipatwa kwa hizo unazoziita swaga? Umepata faida gani tangu ulipoanza kukesha night club? Umepata faida gani zaidi ya kupoteza muda wa kufanya vitu vya maana na fedha? Umepata faida gani sasa?


Umepata faida gani tangu ulipoanza kutukana? Hebu tafakari kwa umakini kijana, je! Kuna chochote kile cha maana ulichoongeza katika maisha yako tangu ulipoanza kutukana? Je! Ulizawadiwa chochote tangu ulipokuwa mtukanaji? Sasa kwa nini unatukana ndugu kama hupati chochote kile?

Dada, umepata faida gani tangu ulipoanza kujichubua zaidi ya kuharibu mwili wako? Umepata nini tangu ulipoanza kuweka vitu bandia katika mwili wako kama vile kucha, kope, make up, lipstick n.k? Unadhani unakuwa mrembo sana? Je hao wanaokusifia wamekupa nini? Je! Sifa zao zimekupa nini cha maana? Je! Ulipewa nyumba kwa ajili ya hivyo? Au Kuna cha ziada zaidi ya kupoteza pesa zako katika kununua vitu hivyo? Na tena umekuwa mtumwa wa hivyo vitu, yaani huwezi ishi pasipo hivyo, kwani ulizaliwa navyo hivyo? Au je! Mungu alikosea kukuumba? Jibu ni hapana, manake yeye anasema kila kitu alichokifanya kilikua ni chema sana, tukiwemo mimi na wewe.

Mwanzo 1:31 MUNGU AKAONA KILA KITU ALICHOKIFANYA, NA TAZAMA, NI CHEMA SANA. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya sita. 

Sasa kwa nini unataka kujibadilisha dada/mama? Huko ni kishindana na Muumba wako.

Umepata nini tangu ulipoanza kutembea nusu uchi barabarani na kuvaa suruali zinazochora maungo yako? Umepata nini zaidi ya kila mtu kuutazama utupu wako? Na kuonekana kama kahaba? Je! Huoni aibu? Wewe si unao watoto? Mbona unatembea nusu uchi? Unafundisha nini watoto zako? Umepata nini tangu ulipoanza kusema watu vibaya na kuwasengenya? 

Umepata nini tangu ulipoanza kuwa mshirikina na mchawi? Je! Ufukara wako wote uliondoka? Je! Unafuraha ndani yako zaidi ya kutoa kafara ndugu zako? Unatoa kafara baba yako, unatoa kafara mama yako, unatoa kafara watoto wako na dada zako, unapata faida gani ndugu (Lakini habari njema ni kwamba, Bwana Yesu anakupenda mno na ndio maana amekupa pumzi siku hii ya leo ili urekebishe njia zako na umfuate yeye, yeye yupo tayari kabisa kukusamehe dhambi zako na kukuombea kwa Mungu maana yupo tayari siku zote kufanya hivyo)

Waebrania 7:25 Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee. 

Rafiki, umepata faida gani tangu ulipoanza kwenda kwa waganga? Je! Uliponywa ugonjwa wako zaidi ya kupoteza fedha zako na kutapeliwa? Umepata faida gani tangu ulipokula keki za upako? Umepata faida gani tangu ulipokunywa maji ya upako? Umepata faida gani tangu ulipotumia chumvi za upako na udongo wa upako? Je! Vilikusaidia kuacha dhambi? Au Vilibadilisha uchumi wako? Jibu ni hapana, sasa ulipata nini? Umepata nini tangu ulipoanza kuwaomba wafu akina Yosefu, yasinta n.k umepata nini tangu ulipoyasujudia masanamu ya mawe, fedha na dhahabu kama ishara ya kumweshimu Mungu? Wakati biblia inasema Mungu hafananishwi na hivyo vitu.

Matendo ya Mitume 17:29 Basi, kwa kuwa sisi tu wazao wa Mungu, HAITUPASI KUDHANI YA KUWA UUNGU NI MFANO WA DHAHABU AU FEDHA AU JIWE, VITU VILIVYOCHONGWA KWA USTADI NA AKILI ZA WANADAMU. 

Yatafakari mambo hayo machache ambayo tunayafanya kila siku katika maisha yetu lakini hayatupi faida yoyote ile, yatafakari kwa umakini sana, na ukiona lipo moja wapo ambalo linakugusa,  na unataka kuachana nalo, basi, fahamu kuwa hujachelewa bado na wala usipoteze tumaini, fahamu kuwa unaweza badilisha mwenendo wa maisha yako sasa na ukawa na amani inayotoka kwa Mungu Mwenyezi. 

Mungu anawapokea watu kama wewe, haijalishi ni mwenye dhambi kiasi gani, au ulikuwa nani, Unachotakiwa kufanya ni kutubu dhambi zako zote kwa kudhamiria kuyaacha mambo yote maovu yasiyokuwa na maana uliyokuwa ukiyatenda hapo mwanzo, na kisha kumwamini Bwana Yesu Kristo kuwa ni Bwana na Mwokozi wa maisha yako, na kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako zote na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu atakayekufanya kuwa kiumbe kipya ndani ya Yesu Kristo (kumbuka ubatizo sahihi na wa kimaandiko ni wa maji mengi na kwa jina La Yesu Kristo sawasawa na matendo 2:38)

Matendo Ya Mitume 2:38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. 

Ikiwa utakuwa tayari kufanya hivyo, basi,  tafuta kanisa lolote la kiroho lililopo karibu nawe, au wasiliana nasi kwa namba hizi kwa msaada.

 +255 652274252

+255 789001312

+255 755 251 999

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Bwana akubariki, Shalom.


Mada zinginezo:

TAFUTA PESA!  TAFUTA PESA! 


Koga ni nini katika biblia? 


JIHADHARI NA WAKINA BALAAMU WA NYAKATI ZA SASA.


INJILI YA KRISTO HAIENDI NA WAKATI


Mama kanisa ni nini? Na Je! bikira Maria ni mama wa kanisa la Kristo?

LEAVE A COMMENT