Mama kanisa ni nini? Na Je! bikira Maria ni mama wa kanisa la Kristo?

  Maswali ya Biblia, Uncategorized

JIBU: Neno mama kanisa asili yake ni kutoka katika lugha ya kilatini “Mater Ecclesiae” ambalo tafsiri yake kwa lugha ya kiswahili ni mama kanisa. Jina hili lilitolewa rasmi na papa Paulo wa VI wa kanisa katoliki kwa heshima ya Maria kama mama wa kanisa. Lakini je! Maria ni mama wa kanisa la Kristo? Na kanisa la Kristo lina mama?


JIBU NI HAPANA. Maria sio mama wa kanisa na wala kanisa la Kristo halina mama na halijawahi kuwa na mama kamwe, kinyume chake ni kwamba, kanisa linafananishwa na BIBI ARUSI (na Maria mwenyewe akiwapo ndani yake) na Mwana-Kondoo Yesu Kristo kama BWANA ARUSI.


Ufunuo 19:7  Na tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana-Kondoo imekuja, na mkewe amejiweka tayari. 

Katika mafundisho ya mitume, hakuna sehemu yoyote ile waliyofundisha watu kwamba Maria ni mama wa kanisa. Maria alikuwa ni miongoni mwa wanawake washirika wa kanisa la kwanza yeye pamoja na mabinti zake aliowazaa (soma Matendo 1:14) ambapo na wao nao walimwamini Kristo kama Bwana na mwokozi wa maisha yao na kuwa na tumaini la ufufuo wa wenye haki. Pia alikuwa na watoto wengine wa kiume, kwa mfano; Yakobo mtume (sio mwana wa Zebedayo) utaona biblia inamtaja mtoto huyu wa Maria kuwa alikuwa ni mtume wa Bwana Yesu.

Wagalatia 1:19  Lakini sikumwona mtume mwingine, ILA YAKOBO, NDUGU YAKE BWANA. 

Lakini pia, utaona mtoto mwengine wa Maria, Yuda nabii (siye Yuda mtume) alikuwepo katika kanisa la kwanza pale Yerusalemu.

Matendo Ya Mitume 15:32  Tena Yuda na Sila, kwa kuwa wao wenyewe ni manabii, wakawausia ndugu kwa maneno mengi, wakawathibitisha. 


Katika hao watoto wa Maria na mitume wengine wote, hakuna hata mmoja aliyehubiri na kufundisha u-mama wa Maria katika kanisa na wala hakukuwa na sanamu lolote la Maria lililochongwa na KIPIGIWA MAGOTI NA KULIBUSU kama baadhi ya watu wanavyofanya leo hii. (Huko ni kuabudu sanamu) Hivyo, wewe kiongozi wa dini ukijiona unafundisha watu vitu hivyo ambavyo hakuna mtume yoyote aliyefundisha na kuvihubiri fahamu kuwa, unafundisha watu elimu nyingine ambayo haipatani na mafundisho ya uzima ya Bwana Wetu na Mwokozi Wetu Yesu Kristo.

1 Timotheo 6:3 Mtu awaye yote akifundisha ELIMU NYINGINE, wala hayakubali maneno yenye uzima ya Bwana wetu Yesu Kristo, wala mafundisho yapatanayo na utauwa, 

4 amejivuna; wala hafahamu neno lo lote; bali ANA WAZIMU wa kuwazia habari za maswali, na mashindano ya maneno, ambayo katika hayo hutoka husuda, na ugomvi, na matukano, na shuku mbaya; 


Hivyo tubia leo  huo uovu uliokuwa ukiwafundisha watu na kuwapoteza kwa kutokujari na kuthamini roho zao zinazopotea kwa mafundisho yako potofu na ya kanisa lako yanayowafanya watu kumchukiza Mungu.


Na pia wewe muumini, ukiona unafundishwa mafundisho kama hayo ya mama wa kanisa, au maji na chumvi za upako, njoo upokee magari, usile chakula fulani, kuwa huru vaa tu unavyotaka mwanamke, nyoa viduku haina shida, oa mke wa pili wakati uliyenae bado yupo, basi, toka hapo kwa usalama wa nafsi yako na anza kusoma biblia yako na kuitii injili moja iletayowokovu wa roho za watu iliyohubiriwa na mitume wa Bwana Yesu. Na Kama bado hujabatizwa tafuta kanisa sahihi la kiroho lililopo karibu nawe uende ukabatizwe kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako. Na ubatizo sahihi wa kimaandiko ni wa maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo (kama ulibatizwa kwa jina la Baba, Mwana, Roho Mtakatifu huo ni ubatizo batili au Kama ulibatizwa kwa kunyunyuziwa maji, huo na ni batili na sio wa kimaandiko)

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Bwana akubariki, Shalom.

 +255652274252/ +255789001312


Mada zinginezo:

Je! Bikira Maria ni mkamilishaji wa mahitaji yetu pale tunapokwama? (kulingana na Yohana 2:3-5)


Biblia imeruhusu ubatizo wa vichanga? (kulingana na matendo 16:33)


IKIMBIENI IBADA YA SANAMU.


MADHARA YA KUTOKUSOMA BIBLIA YAKO.

4 thoughts on - Mama kanisa ni nini? Na Je! bikira Maria ni mama wa kanisa la Kristo?

LEAVE A COMMENT