Jibu ni ndio, si sawa kabisa kwa mwanamke wa Kikristo kuvaa suruali, kwani biblia imesema ni MACHUKIZO mbele za Mungu kwa mwanamke yeyote yule anayefanya hivyo.
Kumbukumbu La Torati 22:5 Mwanamke asivae mavazi YAMPASAYO mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni MACHUKIZO KWA BWANA, MUNGU WAKO.
Na WACHUKIZAO wote, sehemu yao ni katika ziwa la moto, haijalishi wadhifa wako ulionao katika jamii wala cheo chako ulichonacho, kama hutotubu dhambi zako na kuacha kuvaa hizo suruali, wewe ni miongoni mwa WACHUKIZAO
Ufunuo 21:8 Bali waoga, na wasioamini, na WACHUKIZAO, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.
Vazi la suruali sio vazi linalompasa mwanamke hata kidogo, kwa sababu vazi lenyewe lipo kulingana na maumbile ya mwanamume. Mfano; utaona suruali ina zipu ambayo inatoa nafasi ya urahisi kwa mwanaume katika haja ndogo, sasa wewe mwanamke hiyo zipu hapo kwenye hiyo suruali yako ni kwa ajili ya haja ndogo? Huoni kama hilo vazi halikupasi kulingana na maumbile yako wewe mwanamke? Wewe vazi linalokupasa na linaloendana na maumbile yako ya jinsia ya kike ni sketi au gauni, ambayo yanakupa urahisi pia hata katika haja ndogo.
Mwanamke, unatakiwa kufahamu kuwa, lengo moja wapo la wewe kuvaa nguo ni ili KUUSITIRI MWILI WAKO, yaani MAUNGO YA MWILI WAKO na UCHI WAKO, sasa unapovaa suruali, unasitiri kweli MAUNGO YA MWILI WAKO au unasitiri uchi wako tu? Ni wazi kuwa, unasitiri uchi wako tu na si maungo yako, kwani unapovaa suruali inakuchora maumbile ya mwili wako, kitu ambacho kinapelekea wanaokutazama wakutamani na kuzini mioyoni mwao. Maandiko yanakutaka wewe mwanamke wa Kikristo kuvaa mavazi yanayositiri uchi na maungo ya mwili wako pia, na sio mavazi yanayo chora shepu ya mwili wako, huo ni ukahaba.
1 Timotheo 2:9 Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa MAVAZI YA KUJISITIRI, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;
10 bali kwa matendo mema, kama IWAPASAVYO WANAWAKE WANAOUKIRI UCHAJI WA MUNGU.
Hivyo, mama/dada/binti wa Kikristo unayeukiri uchaji wa Mungu, kachome moto hizo suruali zako zote na anza kuvaa nguo safi zinazoendana na maumbuile yako na zinazositiri mwili wako.
Bwana akubariki, Shalom.
Tafadhari washirikishe na wengine ujumbe huu.
Mada zinginezo:
BINTI YA KUHANI YE YOTE ATAKAPOJITIA UNAJISI KWA UKAHABA, AMEMTIA UNAJISI BABA YAKE, ATACHOMWA MOTO
Je! Binti kujipamba mwili wake si ni jambo jema kwani atakua analipamba hekalu la Mungu?
JE! MAPAMBO YA VITO NI DHAMBI?
ONDOENI MIUNGU MIGENI ILIYO KWENU.
Kwani kwa asili ni lipi vazi LA like na ni lipi vazi LA kiume nakwa waislael ni yapi mavazi ya asili waliyo kuwa wanayatumia toka yesu ni joho au maana JoJo ni gauni naomba jibu!
Mavazi yalikuwa mengi kwa wanaume wa Israel na suruali lilikuwa ni moja wapo kati ya mavazi hayo. Hivyo suruali ilivaliwa na wanaume tu! Ikiwemo na mavazi mengine kama joho, kofia n.k
Sasa hakuna mwanamke aliyevaa suruali katika maandiko, na zaidi sana sana ni kuwa, suruali sio vazi na kumsitiri mwanamke, mwanamke anapaswa avae vazi la kusitiri mwili wake (1 Timotheo 2:9)
Bwana akubariki