BINTI YA KUHANI YE YOTE ATAKAPOJITIA UNAJISI KWA UKAHABA, AMEMTIA UNAJISI BABA YAKE, ATACHOMWA MOTO 

  Mwanamke, Uncategorized

FUNDISHO MAALUM KWA MABINTI.

Kama wewe ni binti Mkristo (uliyetubu dhambi zako kwa kumwamini Yesu Kristo, na kubatizwa katika ubatizo sahihi ambao ni wa maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO sawasawa maandiko), fahamu kuwa wewe ni binti wa Yesu Kristo. 


Lakini pia maandiko yanasema, Yesu Kristo ni kuhani, na tena sio kuhani tu, bali ni kuhani Mkuu (Waebrania 4:14), na wa milele kwa mfano wa Melkizedeki (Waebrania 5:6). Hivyo basi, kama wewe ni binti wa Kristo, pia wewe ni binti wa kuhani ambaye ni Yesu Kristo kwa sababu Kristo ndiye Kuhani wa makuhani (kuhani Mkuu). 

Sasa maandiko yanasema hivi katika 

Walawi 21:9 Na binti ya kuhani ye yote atakapojitia unajisi KWA UKAHABAAMEMTIA UNAJISI BABA YAKE; ATACHOMWA MOTO.

Leo hii mabinti wengi wa Kristo (mabinti wa Kuhani Mkuu), kutokana na mambo ya ukahaba yanayoyafanya, wanamtia unajisi Baba yao kwa kufanya jina lake kuudharauliwa na kutukanwa na watu wa mataifa wasiomjua Mungu kama biblia inavyosema.

Warumi 2:24 Kwa maana jina la Mungu latukanwa katika Mataifa KWA AJILI YENU, kama ilivyoandikwa. 

Yafuatayo ni mambo ya ukahaba yanayofanywa na wewe binti wa Kuhani Mkuu Yesu Kristo, unayesoma ujumbe huu ambayo yanapelekea jina la Mungu kutukanwa katika mataifa, na utachomwa moto siku ya mwisho usipotaka kubadilika


1 Mavazi ya kikahaba.

Binti wa Yesu, unapovaa mavazi ya kikahaba wewe ni kahaba na unafanya ukahaba na watu wanao kutazama na wanaokutamani na kuzini na wewe mioyoni mwao na mwisho wa siku utachomwa moto. 

Unakuta binti wa Yesu anavaa kimini mapaja yote nje, akisimama mapaja yote nje, akikaa mapaja yote nje hadi anavuta vuta sketi chini, akiinama ndio tatizo kabisa nguo ya ndani Inaweza hata onekana, anavaa gauni lenye mpasuo unaonesha mapaja yake, binti wa Yesu anavaa nguo inayoonesha kifua chake (maziwa yake), na mgongo wake, (hakuna tofauti na makahaba). Binti wa Yesu unavaa suruali, inachora maumbile yako na shepu yako, hakuna utofauti na kahaba. 


Je! Kwa stahiri hii unategemea vipi wewe binti wa Kristo jina la Mungu lisitiwe unajisi kwa kutukanwa na mataifa kwa ajili yako? Unamchafua Kristo na kumwaibisha, unakuwa kikwazo kwa kuwazuia watu kumgeukia Mungu wanapokutazama wewe binti wa Kristo ukifanya mambo hayo. Nakumbuka wakati fulani nikiwa na mwenzangu kumshukushuhudia mwanamke mmoja habari njema za wokovu uliopo katika Kristo, alisema “nendeni kwanza kwa hao wanawake wenu wa Kikristo mkawafundiashe jinsi ya kuvaa Vizuri” jambo hili halikutushangaza kwani alisema ukweli na alikuwa sahihi kabisa. Wewe binti wa Kristo unayesoma ujumbe huu, unasabisha jina la Mungu kutukanwa na kutiwa unajisi kwa matendo yako ya ukahaba, na mwisho wa siku UTACHOMWA MOTO kama usipotaka kubadilika


2 Mapambo.

Binti wa Kristo unapoweka make up na lipstick mwilini mwako, kucha bandia na kupaka rangi kucha, nywele bandia, kusuka nywele, kubadili rangi ya nywele zako, kuvaa hereni masikioni na vipini puani, vipini kwenye ulimi, cheni na mikufu shingoni, cheni na mikufu miguuni (vikuku), tambua kuwa unafanya mambo yanayofanywa na makahaba na yaliyo fanywa na makahaba kama Yezeberi (mwanamke mzinzi na mchawi), na tena unalichafua hekalu la Mungu ambalo ni mwili wako na kumtia unajisi Kristo kwa matendo yako, UTACHOMWA MOTO USIPOBADILIKA.

1 Wakorinto 3:17 Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi.


3. Uasherati 

Binti wa Kristo unapofanya mambo ya uasherati tambua kuwa unamwaibisha Kristo, wewe ni binti wa Kristo lakini unaishi na kulala na boyfriend ambaye hamjafunga ndoa, unatembea na mume wa mtu na unalizika na unaamani kabisa pasipo kujua kuwa unamwaibisha Kristo, mtoto wa Kristo, UTACHOMWA MOTO USIPOTUBU na kutaka kubadilika 

Walawi 21:9 Na binti ya kuhani ye yote atakapojitia unajisi KWA UKAHABAAMEMTIA UNAJISI BABA YAKE; ATACHOMWA MOTO.

Ikiwa mabinti wa makuhani wa kipindi hicho walichomwa moto kwa mambo ya ukahaba je! Si zaidi sana wewe binti wa Kuhani Mkuu wa sasa na wa milele kustahiri hayo siku ile ya mwisho? maana agano la kale ni kivuli cha agano jipya, na kama sheria hiyo ya agano la kale iliheshimiwa si zaidi sana hii sasa? Hivyo utachomwa moto siku ya mwisho binti wa Kuhani Mkuu kwa mambo ya ukahaba unayoyafanya. Tubu na ubadilike.

Waebrania 10:28 Mtu aliyeidharau sheria ya Musa hufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi wawili au watatu.

29 Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho wa neema? 

Bwana awasaidie mabinti, Shalom.

Tafadhari washirikishe na mabinti wengine habari hii njema.


Mada zinginezo:

SITAWAADHIBU BINTI ZENU WAZINIPO, WALA BIBI ARUSI ZENU WAFANYAPO UASHERATI


Je! Binti kujipamba mwili wake si ni jambo jema kwani atakua analipamba hekalu la Mungu?


Je! Ni dhambi kwa mwanamke wa Kikristo kuvaa suruali?


DAIMA HUWAAMBIA WAO WANAONIDHARAU, BWANA AMESEMA, MTAKUWA NA AMANI.


Ufisadi ni nini katika maandiko?(Waefeso 5:18)

LEAVE A COMMENT