ITHAMINI NA KUIFANYIA MAAMUZI SAHIHI NAFASI NYINGINE ULIYOPEWA NA MUNGU 

  Biblia kwa kina, Uncategorized

Ndugu, kama bado hujatubu dhambi zako na kumwamini Yesu Kristo, na huku unajitambua kabisa kuwa, maisha yako kwa Muumba wako ni ya kusuasua, ni ya dhambi na uvuguvugu, na tena roho yako inakushuhudia kabisa, basi unapaswa uithamini sana nafasi ya kuvuta pumzi uliyopewa na Mungu leo hii na chukua uamuzi sahihi juu ya hatima ya roho yako, kwa sababu, kama Mungu angechukua roho yako katika hali hiyo ungekuwa kwenye mateso na majuto ya milele kuzimu kama yule tajiri.

Luka 16:24 Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, NIHURUMIE, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; KWA SABABU NINATESWA KATIKA MOTO HUU.

Unajijua kabisa wewe ni mwenda kwa waganga, mwabudu sanamu na muomba wafu, unajijua kabisa unaishi na mume wa mtu au mke wa mtu, unajijua kabisa wewe ni mtukanaji, muongo na msengenyaji, unajijua kabisa unaishi na mwanamke au na mwanaume na huku hamjafunga ndoa, unajijua kabisa wewe ni mzinzi na mwasherati, mfanyaji musturbration na matazamaji picha za ngono, unavaa nguo za kikahaba mwanamke (suruali na vimini), na Mungu amekupa neema kuiona asubuhi hii ya leo, basi tafakari sana mpendwa na chukua uamuzi ulio sahihi kutengeneza matendo yako, maana endapo ungekufa katika hali hiyo usingekuwa na tumaini tena kama la huyo tajiri. Mungu Ndiye Anayemiliki roho yako na siku yako ya kufa itakapofika hakuna wa kuzuia, haijalishi wewe ni nani, roho yako ni mali ya Mungu.

Ezekieli 18:4 Tazama, roho zote ni mali yangu; kama vile roho ya baba ni mali yangu, ndivyo ilivyo roho ya mwana mali yangu; roho ile itendayo dhambi itakufa. 

Lakini cha ajabu ni kuwa, watu tunashindwa kulitambua hili, tunadhani sisi ni matajiri sana, sisi ni maskini sana au sisi ni wasomi sana na huku maisha yetu ni ya kumchukiza Mungu (ya dhambi na anasa), tunashindwa kufikiri endapo tungekufa katika dhambi zetu hatima yetu ingekuwa wapi leo hii, starehe na mambo ya dunia hii ndio yametuzonga na kibaya zaidi tunamkata Mungu, tunawadharau watumishi wanaotuhubiria kutubu na kuacha kudhambi, na mwisho wa siku tunakufa na kushuka kuzimu ghafka kama maandiko yanavyosema.

Ayubu 21: 13 Siku zao hutumia katika kufanikiwa, KISHA HUSHULA KUZIMUNI GHAFULA.

14 WALAKINI WALIMWAMBIA MUNGU. TUONDOKEE; KWANI HATUTAKI KUZIJUA NJIA ZAKO

Hii inaumiza sana, hivyo mpendwa, ifanyie uamuzi sahihi siku hii ya leo kwa kutubu dhambi na kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi Sawasawa (matendo 2:38), kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako, nawe utapokea kipawa cha Roho Mtakatifu na kudumu katika fundisho la mitume.

Bwana atusaidie kulitambua hilo;

Tafadhari washirikishe na wengine habari hii njema.

Shalom.

+255652274252/ +255789001312


Mada zinginezo:

LAKINI KWA NENO LAKO NITAZISHUSHA NYAVU.


DAIMA HUWAAMBIA WAO WANAONIDHARAU, BWANA AMESEMA, MTAKUWA NA AMANI.


Kwanini watu wa Kanisa la kwanza walionekana kujazwa Roho Mtakatifu zaidi ya Mara moja?


KWANINI MNANIITA BWANA, BWANA, WALAKINI HAMYATENDI NISEMAYO?


NI BWANA GANI HUYO AMBAYE MANABII WALITABIRI KWA JINA LAKE NA KUTESWA KWA AJILI YAKE?

LEAVE A COMMENT