Kwanini watu wa Kanisa la kwanza walionekana kujazwa Roho Mtakatifu zaidi ya Mara moja?

  Maswali ya Biblia, Uncategorized

SWALI: Kwanini tukisoma maandiko tunaona watu wa kanisa la kwanza walikuwa wakijazwa Roho Mtakatifu zaidi ya mara moja?

Kwa Mfano, tukisoma kitabu cha [Matendo Ya Mitume 2:4] tunaona wanafunzi wa Bwana walipokuwa pamoja, Roho Mtakatifu alikuja juu yao kama upepo na ndimi za moto zilizogawanyika, na watu wote walijazwa Roho Mtakatifu kama alivyotabiri nabii Yoeli

[Matendo Ya Mitume 2:4] Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka. 

Lakini pia, wanafunzi hao hao waliokwisha kupokea na kujazwa Roho Mtakatifu tayari [na wale walioamini siku ile] tunaona wanajazwa tena Roho Mtakatifu baada ya kuomba, pale ambapo Petro na Yohana walipowasimulia yote yaliyowapata kwa wakuu wa makuhani,

[Matendo Ya Mitume 4: 23] Hata walipofunguliwa, WAKAENDA KWA WATU WAO, wakawapasha habari ya mambo yote waliyoambiwa na wakuu wa makuhani na wazee.

 [24] Nao waliposikia, wakampazia Mungu sauti zao kwa moyo mmoja, wakisema, Mola, wewe ndiwe Mungu, ndiwe uliyefanya mbingu na nchi na bahari na vitu vyote vilivyomo; 

[25] nawe ulinena kwa Roho Mtakatifu kwa kinywa cha babaetu Daudi, mtumishi wako, Mbona mataifa wamefanya ghasia, Na makabila wametafakari ubatili?

 [26] Wafalme wa dunia wamejipanga, Na wakuu wamefanya shauri pamoja Juu ya Bwana na juu ya Kristo wake.

[27] Maana ni kweli, Herode na Pontio Pilato pamoja na Mataifa na watu wa Israeli, walikusanyika katika mji huu juu ya Mtumishi wako mtakatifu Yesu, uliyemtia mafuta, 

[28] ili wafanye yote ambayo mkono wako na mashauri yako yamekusudia tangu zamani yatokee. 

[29] Basi sasa, Bwana, yaangalie matisho yao; ukawajalie watumwa wako kunena neno lako kwa ujasiri wote, 

[30] ukinyosha mkono wako kuponya; ishara na maajabu vifanyike kwa jina la Mtumishi wako mtakatifu Yesu.

 [31] HATA WALIPOKWISHA KUMWOMBA MUNGU, MAHALI PALE WALIPOKUSANYIKA PAKATILISWA, WOTE WAKAJAA ROHO MTAKATIFU, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri. 

Sasa Kwanini watu waliokwisha kujazwa Roho Mtakatifu tayari, wanendelee kujazwa Roho Mtakatifu tena?

JIBU: Hiyo ni kufunua kuwa, Roho Mtakatifu anatabia ya kuendelea kujaa ndani yetu kila siku katika maisha yetu ya wokovu hatakama tayari tumeshampokea na kututia muhuri, yeye anajaa tu kila siku tunapoomba. Na ndio maaana tunaona ijapokuwa hao wanafunzi walishajazwa Roho Mtakatifu, lakini waliendelea kujazwa tu zaidi na zaidi kadiri walivyokuwa wakiomba, ndivyo na sisi pia. 

Bwana Yesu alisema maneno haya katika..

[Luka 11:13] Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, JE! BABA ALIYEMBINGUNI HATAZIDI SANA KUWAPA ROHO MTAKATIFU HAO WAMWOMBAO? 

Hivyo, hiyo ni tabia ya Roho kujaa ndani Yetu tunapokuwa waombaji na kutufanya tuvutie na ng’aa zaidi mbele zake na kutufanya tuishi maisha ya utakatifu kwa kuzalisha matunda yake bora kabisa ambayo ni upendo, upole, uaminifu, fadhili, amani, utu wema, uvumilivu n.k 

Bwana akubariki. Shalom

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

 +255652274252/ +255789001312



Mada zinginezo:

Je! ni kweli karama ya kunena kwa Lugha haikupewa kipaumbele na mtume Paulo kama yafanyavyo baadhi ya makanisa leo hii?


JE! YESHURUNI NI NANI?


Mama kanisa ni nini? Na Je! bikira Maria ni mama wa kanisa la Kristo?


Ni maungamo gani aliyoyaungama Yesu Kristo mbele ya Pilato?


Kwanini Ibrahimu alihesabiwa haki na Mungu kabla ya kutahiriwa?

LEAVE A COMMENT