Kwanini Ibrahimu alihesabiwa haki na Mungu kabla ya kutahiriwa?

  Maswali ya Biblia, Uncategorized


JIBU: Ni kweli kabisa kuwa, Ibrahimu alihesabiwa haki kwanza na Mungu baada  tu! ya kumwamini Mungu.

Mwanzo 15:6  Akamwamini Bwana, naye AKAMHESABIA JAMBO HILI KUWA HAKI. 

Na baada ya Ibrahimu kuhesabiwa haki, Mungu akampa agano la kuwatahiri watu wote waume wa nyumbani mwake na watakao zaliwa kwake na kisha yeye mwenyewe kutahiriwa akiwa na umri wa miaka tisini na tisa.

Mwanzo 17:24  Naye Ibrahimu alikuwa mwenye umri wa miaka tisini na kenda alipotahiriwa nyama ya govi lake. 

Kwanini sasa atahiriwe baada ya kuhesabiwa haki? Au kwanini ahesabiwe haki kabla ya kutahiriwa?  Mungu alitaka tuufahamu ujumbe gani hapo? Ikumbukwe kwamba, Ibrahimu aliambiwa na Mungu kuwa, atakuwa baba wa mataifa mengi duniani, yaani atakuwa na wana wengi katika mataifa. Hivyo, basi, tukio la yeye kuhesabiwa haki kabla ya kutahiriwa, ni ili  kwamba awe baba wa wale wote watakao amini, yaani kwa wale wote watakao mwamini Mungu katika Yesu Kristo, na tena awe baba wa waliotahiriwa kwa tukio la yeye kutahiriwa huku wakizifuata nyayo za Ibrahimu za kuami ili wawe wana wa Ibrahimu.

Warumi 4: 10 Alihesabiwaje basi? Alipokwisha kutahiriwa, au kabla hajatahiriwa? Si baada ya kutahiriwa, bali kabla ya kutahiriwa.

 11 Naye aliipokea dalili hii ya kutahiriwa, muhuri ya ile haki ya imani aliyokuwa nayo kabla hajatahiriwa; apate kuwa baba yao wote waaminio, ijapokuwa hawakutahiriwa, ili na wao pia wahesabiwe haki; 

12 tena awe baba ya kutahiriwa, kwa wale ambao si waliotahiriwa tu, bali pia wanazifuata nyayo za imani yake baba yetu Ibrahimu aliyokuwa nayo kabla hajatahiriwa. 

Na ndio maana maandiko yanasema kuwa, wale walio wa imani hao ndio wana wa Ibrahimu, yaani wale walio wa tohara ambao wamemwamini Yesu Kristo na wale wasio wa tohara ambao wanamwamini Yesu Kristo 

Wagalatia 3:7  Fahamuni basi, ya kuwa wale walio wa imani, hao ndio wana wa Ibrahimu. 

Je! Na wewe ni miongoni mwa wana wa Ibrahimu? Kama bado, basi, amua leo hii ili ubarikiwe pamoja na Ibrahimu mwenye imani (Wagalatia 3:9) Kwa kutubu dhambi zako zote kwa kumaanisha, na mwamini Yesu Kristo kuwa ni Bwana na Mwokozi wa maisha yako na kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi ambao ni wa maji tele na kwa jina la Yesu Kristo kwaajiri ya ondoleo la dhambi zako.

Bwana akubariki, Shalom.

Tafadhari washirikishe na wengine ujumbe huu.

Mawasiliano  +255652274252/ +255789001312


Mada zinginezo:

Je Ibrahimu alizaa watoto wangapi?


Je Mke wa Kaini alikuwa nani?


Ufisadi ni nini kibiblia? .Waefeso 4:19


Je! Kuna dhambi kubwa kuliko nyingine?

2 thoughts on - Kwanini Ibrahimu alihesabiwa haki na Mungu kabla ya kutahiriwa?

LEAVE A COMMENT