Ufisadi ni nini kibiblia? .Waefeso 4:19

  Maswali ya Biblia, Uncategorized

Wengi wetu tunaposikia neno ufisadi moja kwa moja akili zetu zinatupeleka kwenye vitendo vya ubadhilifu wa fedha za shirika fulani au za taifa kwa faida binafsi..


Lakini kibiblia Neno hili linatumika tofauti..linamaanisha kitendo cha ukahaba au umalaya uliopindukia ambao haujali hata jinsia umri au mazingira..

Hivyo popote pale ukutanapo na Neno hili ujue hiyo ndio maana yake..
Utalisoma Neno hilo katika vifungu hivi..

Waefeso 4:19[19]ambao wakiisha kufa ganzi wanajitia katika mambo ya ufisadi wapate kufanyiza kila namna ya uchafu kwa kutamani.


Waefeso 5:18[18]Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho; 

 Tito 1:6-7[6]ikiwa mtu hakushitakiwa neno, naye ni mume wa mke mmoja, ana watoto waaminio, wasioshitakiwa kuwa ni wafisadi wala wasiotii.[7]Maana imempasa askofuawe mtu asiyeshitakiwa neno, kwa kuwa ni wakili wa Mungu; asiwe mtu wa kujipendeza nafsi yake, asiwe mwepesi wa hasira, asiwe mlevi wala mgomvi, asiwe mpenda mapato ya aibu;


Hapo ikiwa na maana kuwa hata maskofu ili waweze kupewa nafasi ya kulichunga kanisa hata watoto wao wanapaswa wahakikiwe kuwa hawana hizo tabia za ukahaba na umalaya..


Utasoma pia Neno hili katika vifungu hivi..1Petro 4:3-4. Marko 7:22, Yuda 1:4, 2Petro 2:18.

Hivyo Kwa kuhitimisha ni kuwa Biblia imeweka wazi kabisa kwa watu wenye tabia kama hizi…kwamba kamwe wasitazamie wataurithi uzima wa milele..

Wagalatia 5:19-21[19]Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,[20]ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,[21]husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.


Shalom.

LEAVE A COMMENT