Je Ibrahimu alizaa watoto wangapi?

  Uncategorized

Ibrahimu baba wa imani, alikuwa na jumla ya watoto (8).

 1) Mwana wake wa kwanza(1) aliitwa Ishmaeli: Huyu alikuwa ni mwana wa kijakazi wa mke wake, aliyeitwa Hajiri. Ishmaeli  alipatakana, kwasababu ya Sara kukosa mtoto kwa muda mrefu, hivyo akaona ili amstahi mume wake, akamruhusu akamruhusu kijakazi wake alale na mumewe, ampatie uzao. Ndipo akazaliwa Ishameli. (Mwanzo 16:1-4),

Mwana wa pili(2) aliitwa Isaka. Huyu ndiye aliyekuwa mwana wa Ahadi, ambaye Mungu alimwahidia Ibrahimu kuwa atakuwa urithi wake. Yeye ndiye aliyekuja kuzaliwa na Sara, miaka 14 baadaye baada ya Ishmaeli.

Mwanzo 21: 1 -3

Wana wengine sita (6) waliosalia: Walikuwa ni wa mwanamke aliyeitwa Ketura, Huyu alikuja kuolewa na Ibrahimu baada ya Sara kufa.

 Mwanzo 25: 1 “Ibrahimu alioa mke mwingine jina lake akiitwa Ketura. 2 Akamzalia Zimrani, na Yokshani, na Medani, na Midiani, na Ishbaki, na Sua. 3 Yokshani akamzaa Sheba, na Dedani; na wana wa Dedani walikuwa Waashuri na Waletushi, na Waleumi”.

Inakamilisha Jumla ya watoto nane (8), wa Ibrahimu.

Lakini ni nini tunajifunza kwa uzao wa Ibrahimu.

Japokuwa alikuwa na wana wengi, lakini aliyekuwa mwana wake wa pekee, mwana wa urithi alikuwa ni Isaka tu. Na ndio maana utaona wakati Ibrahimu alipokuwa anawabariki watoto wake, wale wengine 7 aliwapa zawadi tu lakini mwanawe Isaka alimpa vyote alivyokuwa navyo, yaani zawadi pamoja na urithi. (Mwanzo 25:5-6)

Hata leo hii, wana wa ahadi ni wachache sana. Watakaopewa kuurithi uzima wa milele watakuwa ni wachache sana, ndio wale waliompokea YESU KRISTO katika maisha yao wakiwa hapa duniani. Lakini kwa wengine wote walio nje ya neema ya Yesu Kristo, hawana sehemu yoyote katika ule ufalme wa mbinguni unaokuja baada ya ulimwengu huu kuisha. Hivyo usifurahie kufanikishwa na Mungu sasa hapa duniani, lakini huna uhusiano wowote na Mungu.. Furahia uhusiano wako na Mungu kwanza, na hivyo vyote vifuate baadaye.

Hapo ndipo unapokuwa mwana wa ahadi wa Mungu.

LEAVE A COMMENT