Kuna aina kuu tatu za dhambi.
- Dhambi isiyo ya mauti
- Dhambi ya Mauti
- Dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu.
Dhambi isiyo ya mauti ni dhambi ambayo mtu akiifanya anaweza kusamehewa, bila ya adhabu yoyote, au hata akipokea adhabu basi haitakuwa adhabu ya kumfanya afe.
Nyingi ya dhambi tunazozitenda leo hii zinaangukia katika kundi hili. Pale mtu anapotubu kwa kumaanisha Mungu anamsamehe, aidha kwa adhabu kidogo au bila adhabu kabisa,, kwamfano Petro alipomkana Bwana, alikwenda kutubu na akasamehewa, bila hata ya adhabu yoyote.
1Yohana 5:16 “Mtu akimwona ndugu yake anatenda dhambi isiyo ya mauti, ataomba, na Mungu atampa uzima kwa ajili ya hao watendao dhambi isiyo ya mauti. Iko dhambi iliyo ya mauti. Sisemi ya kwamba ataomba kwa ajili ya hiyo.
17 Kila lisilo la haki ni dhambi, na dhambi iko isiyo ya mauti.
DHAMBI YA MAUTI
Lakini zipo dhambi ambazo, mtu akizifanya, ataweza kweli kusamehewa na kuingia katika ufalme wa mbinguni, lakini adhabu ya kifo hapa duniani haikwepeki kwake. Mara nyingi dhambi hizi, huwa ni zile za makusudi, au za uzembe uliopitiliza.
Mfano wa watu waliofanya dhambi kama hizi katika biblia walikuwa ni Wana wa Israeli. Utaona japokuwa walitendewa mambo mengi na miujiza Mingi na Mungu lakini, hawakumcha yeye, kinyume chake, wakaendelea kuwa wanung’unikaji, wazinzi, na waabudu sanamu, Hivyo ikafika wakati Mungu akaghahiri kutembea nao, akaapa kuwa hakuna hata mmoja wao atakayeiona hiyo nchi ya Ahadi. Wote watakufa jangwani. Na kweli japokuwa walilia na kuomboleza na kutubu sana, lakini Mungu hakusikia kilio chao wote, walikufa wote jangwani.
1 Wakorintho 10 : 1-12
“1 Kwa maana, ndugu zangu, sipendi mkose kufahamu ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu; wote wakapita kati ya bahari;
2 wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingu na katika bahari;
3 wote wakala chakula kile kile cha roho;
4 wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo.
5 Lakini wengi sana katika wao, Mungu hakupendezwa nao; maana waliangamizwa jangwani.
6 Basi mambo hayo yalikuwa mifano kwetu, kusudi sisi tusiwe watu wa kutamani mabaya, kama wale nao walivyotamani.
7 Wala msiwe waabudu sanamu, kama wengine wao walivyokuwa; kama ilivyoandikwa, Watu waliketi kula na kunywa, kisha wakasimama wacheze.
8 Wala msifanye uasherati, kama wengine wao walivyofanya, wakaanguka siku moja watu ishirini na tatu elfu.
9 Wala tusimjaribu Bwana, kama wengine wao walivyomjaribu, wakaharibiwa na nyoka.
10 Wala msinung’unike, kama wengine wao walivyonung’unika, wakaharibiwa na mharabu.
11 Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani.
12 Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke”.
Ipo mifano mingi sana ya dhambi kama hizi katika biblia, Ukisoma agano jipya.. Utaona mitume walitoa maagizo kwa kanisa juu ya watu wanaotenda dhambi za uzinzi, wakabidhiwe shetani ili mwili uangamie lakini roho zao zipone katika siku ile ya Bwana..
1 Wakorintho 5 : 1-13
“1 Yakini habari imeenea ya kuwa kwenu kuna zinaa, na zinaa ya namna isiyokuwako hata katika Mataifa, kwamba mtu awe na mke wa babaye.
2 Nanyi mwajivuna, wala hamkusikitika, ili kwamba aondolewe miongoni mwenu huyo aliyetenda jambo hilo.
3 Kwa maana kweli, nisipokuwapo kwa mwili, lakini nikiwapo kwa roho, mimi mwenyewe nimekwisha kumhukumu yeye aliyetenda jambo hilo, kana kwamba nikiwapo.
4 Katika jina la Bwana wetu Yesu, ninyi mkiwa mmekusanyika pamoja na roho yangu, pamoja na uweza wa Bwana wetu Yesu;
5 kumtolea Shetani mtu huyo, ili mwili uadhibiwe, ili na roho iokolewe katika siku ya Bwana Yesu”.
Hivyo tunapaswa tuwe makini sana, na mambo tunayoyatenda hususani kwa sisi ambao tayari tumeshaujua ukweli lakini bado tunauchezea, na kuupuuzia. Kuna wakati utafika, hata tuombeje Mungu hatoweza kutusamehe hapa duniani. Tutakufa tu.
DHAMBI YA KUMKUFURU ROHO MTAKATIFU.
Hii ni dhambi ambayo, mtu husamehewi hapa, wala kule ng’ambo utakapokwenda.. Dhambi hii ndio ile ya kumkufuru Roho Mtakatifu. Ambayo Bwana Yesu aliizungumza katika..
Mathayo 12:32 “Naye mtu ye yote atakayenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali yeye atakayenena neno juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao”.
Kwa urefu wa dhambi hii Fungua hapa..>> Kumkufuru Roho Mtakatifu kukoje?
shalom wana wa mungu, kuna jambo limenitokea mpakasasa najiuliza kama nitaingia kweli katika ufalme wa mungu? nilibatizwa na wasabato,na, baada yakujuwa ubatizo nikautafuta lakini nilienda kubatizwa tena katika kanisa lakipentekosti na sikuhuliza hivo nikaenda kubatizwa mar ya pili lakini nikabatizwa tena vibaya, basi nikasema nitauliza dhehebu kwa dhehebu,nikauliza basi kuna dhehebu moja mchungaji wake akanidanganya eti wanabatiza ubatizo sahihi, hivo nilipokwenda kubatizwa mara yatatu tena wakanibatiza vibaya kama mwanzo na nikaamua kuacha lakini baada ya miezi sinyingi nikabatizwa sasa katika ubatizo sahihi yaani ulewa maji tele ma kwajina la yesu, lakini najiona kuwa mtu wakwanza kubatizwa mara 4 kisasa hata katika biblia, je!kweli nimepokelewa na mungu? na isitoshe bado nilikuwa najaribu kujitakasa lakini kuna muda nilikuwa nikiwaza vibaya nakufanya dhambi makusudi hata leo hivi jumatatu 3.4.2023 nimefanya dhambi makusudi na sio mara yakwanza, je nikitubu nitasamehewa kweli na kupokea roho?
Bwana Yesu apewe sifa, haujafanya kosa lo lote lile tena umechukua maamuzi sahihi kabisa ya kuutafuta Ubatizo wa kweli na kubatizwa katika huo, hivyo uwe na amani na zidi kumwomba Mungu akujaze Roho Mtakatifu