Kumkufuru Roho Mtakatifu kukoje?

  Maswali ya Biblia, Uncategorized

Je mtu anamkufuru vipi Roho Mtakatifu mpaka kupeleke asisamehewe kabisa ?


Dhambi hii Bwana Yesu aliinena kutokana na tabia aliyoiona kwa wale mafarisayo na waandishi waliokuwa wamemzunguka.

Walikuwa ni watu wanaoishi maisha ya unafki wakijua ukweli lakini wasiutende na kibaya zaidi waliutumia ujuzi wao kuwapotosha hata na wengine wasiufahamu ukweli..na ndio maana Bwana Yesu aliwakemea  sana ukisoma katika
(Mathayo 23) jtalithibitisha hilo..na kuwaambia siku ile watakuwa na hukumu kubwa zaidi.


Kwamfano katika kisa hiki..walimwona Bwana akitoa pepo kwa uweza wa Roho wa Mungu..Na hilo walilifahamu kabisa..Na ndioaana yule farisayo mmoja aliyeitwa Nikodemo aliyemfuata usiku na kumwambia Rabi “TWAJUA” kuwa umetoka kwa Mungu..(Yohana 3:1-2)


Ikiwa na maana kumbe mafarisayo wote walijua ukweli lakini kwasababu ya wivu wakaanza kumzushia  Bwana uongo kuwa Roho iliyo ndani yake ni ya Beelzebuli na si ya Mungu  ili tu watu wasimwamini..Na kwasababu hiyo basi wakawa wameshaitenda dhambi hii ya kumkufuru Roho Mtakatifu..

Mathayo 12:22-32

[22]Wakati ule akaletewa mtu mwenye pepo, kipofu, naye ni bubu; akamponya, hata yule bubu akanena na kuona.[23]Makutano wote wakashangaa, wakasema, Huyu siye mwana wa Daudi?[24]Lakini Mafarisayo waliposikia, walisema, Huyu hatoi pepo, ila kwa Beelzebuli mkuu wa pepo.[25]Basi Yesu akijua mawazo yao, akawaambia, Kila ufalme ukifitinika juu ya nafsi yake, hufanyika ukiwa; tena mji au nyumba yo yote ikifitinika juu ya nafsi yake, haitasimama.[26]Na Shetani akimtoa Shetani, amefitinika juu ya nafsi yake; basi ufalme wake utasimamaje?[27]Na mimi nikitoa pepo kwa Beelzebuli, je! Wana wenu huwatoa kwa nani? Kwa sababu hiyo hao ndio watakaowahukumu.[28]Lakini mimi nikitoa pepo kwa Roho wa Mungu, basi ufalme wa Mungu umekwisha kuwajilia.[29]Ama awezaje mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuviteka vyombo vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu? Ndipo atakapoiteka nyumba yake.[30]Mtu asiye pamoja nami yu kinyume changu; na mtu asiyekusanya pamoja nami hutapanya.[31]Kwa sababu hiyo nawaambia, Kila dhambi na kila neno la kufuru watasamehewa wanadamu, ila kwa kumkufuru Roho hawatasamehewa.[32]Naye mtu ye yote atakayenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali yeye atakayenena neno juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao.


Hii ni kutufundisha kuwa tuwe makini na kazi za Roho Mtakatifu..mahali ambapo nguvu za Mungu za kweli zinaonekana..injili ya kweli inahubiriwa..Roho Mtakatifu anatenda kazi halafu tunatoa maneno ya kukebehi au kudhihaki..kusema. Zile ni nguvu za giza..za freemason..kwa wivu tu..tupo hatarini kuitenda dhambi hii.


Hivyo kwa kuhitimisha ni kuwa dhambi hii hutendwa kwa watu waufahamuo ukweli lakini kwa makusudi wanaupinga kwa faida zao wenyewe..lakini si kwa mtu ambaye hana maarifa..kwasababu wengine wanakufuru kwa ujinga wao tu,..Hawa wanasamehewa..Vilevile mawazo mabaya kinyume na Roho Mtakatifu hayakufanyi uwe umemkufuru Roho Mtakatifu.
Ukiona kuna vitisho ndani yako kwamba umemkufuru Roho Mtakatifu vikatae huo ni uongo wa shetani..wanaomkufuru Roho Mtakatifu hofu ya Mungu huwa haipo ndani yao hata kidogo, na ndio maana wanayafanya hayo hadharani.

LEAVE A COMMENT