Je! Kuna dhambi kubwa kuliko nyingine?

  Maswali ya Biblia, Uncategorized

Kibiblia hakuna dhambi kubwa kuliko nyingine kwasababu dhambi zote zina malipo sawa nayo ni mauti.


Warumi 6:23 Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.


Hii ikiwa na maana kama ulikufa kwa dhambi ya kuzini na mwingine akafa kwa dhambi ya kuua watu wengi..wote mtaishia katika lile ziwa la moto. Lakini pamoja na hayo biblia inaonyesha pia kuna tofauti ya adhabu kulingana  Aina ya dhambi ya mtu.


Tunalithibitisha hilo katika vifungu hivi;


Luka 12:47-48[47]Na mtumwa yule aliyejua mapenzi ya bwana wake, asijiweke tayari, wala kuyatenda mapenzi yake, atapigwa sana.[48]Na yule asiyejua, naye amefanya yastahiliyo mapigo, atapigwa kidogo. Na kila aliyepewa vingi, kwake huyo vitatakwa vingi; naye waliyemwekea amana vitu vingi, kwake huyo watataka na zaidi.


Maana yake ni kuwa kama ulifahamu jambo fulani ni kosa kulifanya, halafu ukaenda kulifanya makusudi adhabu yako itakuwa kubwa sana siku ile. 


Alisema pia..


Mathayo 23:14[Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnakula nyumba za wajane, na kwa unafiki mnasali sala ndefu; kwa hiyo mtapata hukumu iliyo kubwa zaidi.]


Yohana 19:11[11]Yesu akamjibu, Wewe hungekuwa na mamlaka yo yote juu yangu, kama usingepewa kutoka juu; kwa hiyo yeye aliyenitia mikononi mwako yuna dhambi iliyo kubwa zaidi.


Kwahiyo kwa hitimisho  ni kuwa hakuna dhambi yenye heri ukifa katika hizo mwisho wake utakuwa ni mauti tu..lakini adhabu za dhambi zinatofautiana kulingana na aina ya dhambi au wingi wa dhambi uliyoitenda.


Njia pekee ni kukaa mbali nazo kwa kumwamini Bwana Yesu Kristo na kumpokea Roho wake.

LEAVE A COMMENT