Ufisadi ni nini katika maandiko?(Waefeso 5:18)

Dhambi, Uncategorized No Comments

Tofauti na inavyofahamika au kuzoeleka, kuwa ufisadi ni kitendo cha kukosa uaminifu kwa kuhujumu fedha za shirika Fulani au taasisi Fulani, kwa lengo la kujipatia faida zako binafsi.

Lakini tukirudi katika biblia Neno ufisadi limetumika kueleza tabia nyingine tofauti. Na tabia yenyewe ni uasherati, uzinzi,  umalaya/ Ukahaba uliovuka mipaka, ambao haujali hata jinsia, umri, au kiumbe, tamaa iliyopilitiliza.

Kwamfano Neno hilo tunaweza kulisoma katika vifungu hivi;

Marko 7:21 “Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati,

22 wivi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu.

23 Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi.

Warumi 13:13 “Kama ilivyohusika na mchana na tuenende kwa adabu; si kwa ulafi na ulevi, si kwa ufisadi na uasherati, si kwa ugomvi na wivu”.

Waefeso 5:18 “Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho;”

2Wakorintho 12:21 “nami nitakapokuja tena, Mungu wangu asije akanidhili kwenu, nami nikawasikitikia wengi waliokosa tangu hapo, wasiutubie uchafu, na uasherati, na ufisadi walioufanya.

Kwamfano Hapa Paulo alilikemea sana kanisa la Korintho kwasababu hilo ndio lililokuwa limechafuka sana, kwa mambo ya zinaa za ufisadi, utalithibitisha hilo katika vifungu hivi;

1 Wakorintho 5:1

“1 Yakini habari imeenea ya kuwa kwenu kuna zinaa, na zinaa ya namna isiyokuwako hata katika Mataifa, kwamba mtu awe na mke wa babaye”.

Neno hilo unaweza kulisoma pia katika vifungu hivi;

Waefeso 4:19, 1Petro 4:3, 2Petro 2:7.

Hivyo ndugu yangu, kama vile maandiko yanavyosema hakuna mwasherati atakayeurithi uzima wa milele. Hivyo hatuna budi kukaa mbali nao. Lakini kwa nguvu zetu hatutaweza kushinda isipokuwa kwa msaada wa Yesu Kristo tutashinda ufisadi na dhambi nyingine zote.

Hivyo ikiwa upo nje ya Kristo, na utataka leo Yesu akuokoe na kukupa  uwezo huo wa kushinda dhambi, basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi, kwa msaada Zaidi. +255652274252 / +255693036618.

Na pia ikiwa utapenda kupata mafundisho haya kwa njia ya whatsapp basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizo hizo

Bwana akubariki.

Mada Nyinginezo:

Kwanini Ibrahimu alihesabiwa haki na Mungu kabla ya kutahiriwa?

JIFUNZE TABIA HII KUTOKA KWA MITUME ANDREA NA FILIPO.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *