JIFUNZE TABIA HII KUTOKA KWA MITUME ANDREA NA FILIPO.

  Biblia kwa kina, Uncategorized

Shalom, jina la Bwana wetu Yesu Kristo lihimidiwe milele. Kuna tabia moja iliyooneshwa  na mitume, Andrea na Filipo kwenye biblia ambayo na sisi kama wanafunzi wa Bwana Yesu hatuna budi kuwa nayo. Na tabii hii au kitu hicho kilichofanywa na hao mitume tunakisoma katika injili ya Yohana [ Zingatia maneno yaliyoandikwa kwa herufi kubwa]

 [Yohana 1:40]  Andrea, nduguye Simoni Petro, alikuwa mmoja wa wale wawili waliomsikia Yohana na KUMFUATA  YESU.

[41]  Huyo akamwona kwanza Simoni, ndugu yake mwenyewe, akamwambia, Tumemwona Masihi (maana yake, Kristo). 

[42] AKAMPELEKA KWA YESU. Naye Yesu akamtazama, akasema, Wewe u Simoni, mwana wa Yohana nawe utaitwa Kefa (tafsiri yake Petro, au Jiwe).

Baada ya Andrea (Aliyekuwa mwanafunzi wa Yohana Mbatizaji) kumsikia Yohana Mbatizaji akinena habari za Yesu, Andrea ALIMFUATA YESU yeye na mwenzake na kumuuliza Rabi unakaa wapi? Lakini Andrea hakuishia hapo tu, bali alifanya kitu ambacho nataka na sisi tujifunze leo, na kitu hicho tunakisoma katika mstari wa 42. Maandiko yanasema Andrea ALIMPELEKA KWA YESU ndugu yake ambaye ni Petro.  Lakini hata kwa Filipo pia, baada ya kupata ufunuo kwamba Yesu ndiye masihi na yeye akaenda kumwambia rafiki yake Nathanaeli kuwa tumemwona masihi NJOO UONE.

[Yohana 1:43]  Siku ya pili yake alitaka kuondoka kwenda Galilaya, naye akamwona Filipo. YESU AKAMWAMBIA, NIFUATE.

[44] Naye Filipo alikuwa mtu wa Bethsaida, mwenyeji wa mji wa Andrea na Petro.

[45] Filipo akamwona Nathanaeli, akamwambia, Tumemwona yeye aliyeandikiwa na Musa katika torati, na manabii, Yesu, mwana wa Yusufu, mtu wa Nazareti.

[46] Nathanaeli akamwambia, Laweza neno jema kutoka Nazareti? FILIPO AKAMWAMBIA, NJOO UONE.

Sasa hii ni kufunua nini kwetu? Hii ni kufunua kuwa, na sisi kama watu ambao tuliojaariwa kumfahamu Bwana au watu tuliojaariwa kuitwa na Bwana, hatuna budi na sisi KUWAPELEKA NDUGU ZETU Na MARAFIKI ZETU KWA BWANA YESU kama Andrea na Filipo walivyofanya, huku na sisi tukijitahidi kwa upande wetu kuyafanya mapenzi ya Mungu

Tunatakiwa kuwavuta kaka zetu, na dada zetu, mama zetu na baba zetu, wajomba zetu na shangazi zetu, wafanyakazi wenzetu na majirani wenzetu ili waje kwa Bwana. Hatuna budi kuwaambia kuhusu hukukumu iliyotangazwa na Mungu juu ya uasi wote na kukimbilia kwa Yesu Kristo.

Hatuna budi kuwaambia kuhusu kuitii injili ya Bwana wetu Yesu Kristo na nini kitatokea endapo tusipoitii.

 [2 Wathesalonike 1:8] katika mwali wa moto huku akiwalipiza kisasi wao wasiomjua Mungu, na wao wasioitii Injili ya Bwana wetu Yesu

Lakini pia, hata na sisi tunaoambiwa habari njema na ndugu zetu na marafiki zetu, hatuna budi kuwa wasikivu na kutii kama Petro na Nathanaeli. Tusiwe na mioyo migumu na kuwaona watu wanaotuambia habari njema ya Wokovu na hukumu ya Mungu juu dhambi ni kama watu waliochanganyikiwa. Bali tufanye kinyume chake.

Bwana akubariki sana, Shalom.

Tafadhari washirikishe na wengine habari hii njema.

+255652274252/ +255789001312




MADA ZINGINEZO

JIFUNZE TABIA HII KUTOKA KWA APOLO.


JIFUNZE TABIA HII KUTOKA KWA KORNELIO


Jifunze tabia hii kutoka kwa mtume Paulo.

LEAVE A COMMENT