KRISTO ALIZICHUKUA VIPI DHAMBI ZA WATAKATIFU WALIOKUFA KABLA YAKE?

  Maswali ya Biblia, Uncategorized

SWALI: Maandiko yanasema kuwa, Bwana wetu Yesu Kristo kama Mwana-kondoo wa Mungu, alizichukua dhambi za dunia nzima kwa kufa kwake pale msalabani [kwa kuchinjwa pale masalabani] sasa, alizichukua vipi dhambi za watakatifu ambao walikufa kabla yake yeye? Mfano; Adamu, Hawa, Ibrahimu, Isaka, Yakobo n.k

JIBU: Ni kweli kabisa kuwa, Bwana wetu Yesu kristo akiwa kama Mwana-kondoo wa Mungu alizichukua dhambi za ulimwengu wote, na hata Manabii kadhaa walishuhudia hilo; mfano Nabii Isaya. Lakini pia hata Nabii Yohana Mabatizaji alishuhudia hilo kwa uweza wa Roho, kuwa Bwana Yesu ni Mwana-kondoo wa Mungu, na si mwana kondoo tu, kwani hata sisi pia ni kondoo, bali anayezichukua dhambi za ulimwengu. Unaweza thibitiaha hilo katika..

[Yohana 1:37]  Akamtazama Yesu akitembea, akasema, TAZAMA, MWANA-KONDOO WA MUNGU!

SOMA TENA

 [Yohana 1:29]  Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, TAZAMA, MWANA-KONDOO WA MUNGU, AICHUKUAYE  DHAMBI YA ULIMWENGU!

Hivyo basi, mtu yeyoye leo hii akitubu na kumwamini Bwana Yesu, basi, anaoshwa na kupata msamaha wa dhambi zake kwa damu ya Mwana-kondoo [ Yesu Kristo]

Lakini tukirudi sasa kwa watakatifu waliokufa miaka mingi kabla ya Bwana Yesu, na wao pia vivyo hivyo, hawakukamilishwa pasipo damu hii ya Mwana-kondoo wa Mungu. Sasa ni kivipi? 

Jibu ni kwamba, damu hii ya Mwana-kondoo ilishamwagika kabla ya kuwekwa misingi ya dunia, kumaanishwa kwamba, huyu Mwana-kondoo wa Mungu alishachinjwa kabla ya kuwekwa misingi ya dunia?

 [Ufunuo wa Yohana 13:8]  Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo, ALIYECHINJWA TANGU KUWEKWA MISINGI YA DUNIA.

Umeona hapo? Kumbe katika roho tayari damu hii ya Mwana-kondoo ilishamwagika na kuwakamilisha hao wataatifu, lakini katika mwili sasa ukamilisho wao ulithibitika siku ile ya kufufuka kwakwe Bwana Yesu.

 [Mathayo 27:52]  makaburi yakafunuka ikainuka miili mingi ya watakatifu waliolala

[53]  nao wakiisha kutoka makaburini mwao, BAADA YA KUFUFUKA KWAKE, wakauingia mji mtakatifu, wakawatokea wengi.

Hapo anaposema “baada ya kufufuka kwake” anamaanisha kuwa, hao watakatifu waliokufa kabla ya Bwana, walifufuka baada ya Bwana Yesu kufufuka, na hii ilitokea ili kukamilisha unabii uliosema kwamba, Bwana Yesu atakuwa mzaliwa wa kwanza katika wafu.

[Zaburi 89:27]  Nami nitamjalia kuwa mzaliwa wangu wa kwanza, Kuwa juu sana kuliko wafalme wa dunia.

Soma pia.

[Wakolosai 1:18]  Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa naye ni mwanzo, NI MZALIWA WA KWANZA KATIKA WAFU, ILI KWAMBA AWE MTANGULIZI KATIKA YOTE.

Unaweza soma pia Warumi 8:39

Sasa na wewe ndugu yangu unayesoma ujumbe huu, umeshaoshwa dhambi zako kwa damu ya huyu Mwana-kondoo? Kama bado, basi jua kuwa nafasi ya kufanya hivyo bado unayo sasa, unachotakiwa kufanya ni kutubu dhambi zako kwa kumaanisha kuziacha kabisa, kama ulikuwa ni mzinzi unaacha, kama ulikiwa unawachukia watu unaacha, kama ulikuwa ni msengenyaji unaacha, kama ulikuwa ni mtukanaji unaacha, kama ulikuwa ni mtazamaji wa picha za ngono unaacha, kama ulikuwa ni mvaaji wa vimini, suruali kwa wanawake na nguo zinazochora maungo yako unaacha, kama ulikuwa unajichubua na kubandika vitu bandia kwenye mwili wako kama kucha, lipstick, kope, rasta, mawigi, n.k unaacha, kama ulikuwa ni mwimbaji na msikilizaji wa nyimbo za kidunia unaacha na kisha nenda kabatizwe katika ubatizo sahihi ambao ni wa kuzamishwa na kwa jina la YESU KRISTO kwaajiri ya ondoleo la dhambi zako.

[Matendo ya Mitume 2:38]  Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa JINA LAKE YESU KRISTO, MPATE ONDOLEO LA DHAMBI ZENU, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.

Tafadhari shea na wengine ujumbe huu.

Bwana akubariki sana, Shalom.

+255652274252/ +255789001312MADA ZINGINEZO:

Je! Hadi sasa kuna manabii wa Mungu?


Kuna injili ngapi katika biblia?


Je! Na wewe ni kama Belshaza?

LEAVE A COMMENT