MMEKWISHA KUSHIBA, MMEKWISHA KUPATA UTAJIRI, MMEMILIKI PASIPO SISI.

Maneno hayo aliyaandika mtume Paulo kwa makanisa yaliyokuwapo Korintho, ambayo kutokana na utajiri wa neema ya Mungu waliyoipata kwa kuamini, na kujaaliwa karama za rohoni, na nguvu za Mungu, wakaanza kuonesha tabia za kushiba kana kwamba tayari wanacho Kila kitu na wala hawajitaji tena chochote kile kutoka kwa mitume wa Kristo waliokuwapo kwa  kipindi kile, hawakutaka tena kudumu katika mafundisho ya mitume ambayo yanatokana na maandiko matakatifu, kila mtu kwa utaratibu wake alifanya alichoona kuwa ni sahihi hata kama hakipo kwenye maandiko, ili mradi tu ananeana kwa lugha, basi anafahamu kila kitu kupita maandiko, ili mradi tu anaombea watu na kufanya miujiza, au anafufua wafu, basi anajiona yeye hana haja ya kuambiwa tena chochote kile.

[1 Wakorintho 4:8] MMEKWISHA KUSHIBA, MMEKWISHA KUPATA UTAJIRI, MMEMILIKI PASIPO SISI. Naam, laiti mngemiliki, ili sisi nasi tumiliki pamoja nanyi!

Tabia hiyo ya kutaka kumiliki pasipo mitume [yaani mafundisho yao yaliyotokana na mandiko matakatifu ambayo ni ya Kristo] ndiyo iliyopelekea mtafaruko baina yao, mmoja kujiona yeye ni wa huyu na ni bora kuliko mwengine, mwingine kujiona yeye ni wa yule na ni bora kuliko mwengine, kwa sababu walishiba kwa miujiza na ishara pasipo kutaka kufuata maandiko. Na kibaya zaidi wengine wakaanza kwenda mbali zaidi na kufanya dhambi ambazo hazipo hata kwa watu wasioamini kama vile kuzini na wake za baba zao

[1 Wakorintho 5:1] Yakini habari imeenea ya kuwa kwenu kuna zinaa, na zinaa ya namna isiyokuwako hata katika Mataifa, kwamba mtu awe na mke wa babaye.

Wengine kwa kutaka kuongoza kanisa bila kufuata mafundisho ya awali ya Bwana Yesu na mitume, walianza kuingiza tamaduni zao za zamani walizokuwa nazo kabla ya kuamini, ambazo haziendani na imani waliyoipokea baada ya kuamini, wameshiba rohoni na hawana haja tena na msaada wa maandiko kama tu ilivyo kwa wakristo wengi leo hii.

[1 Wakorintho 4:8] MMEKWISHA KUSHIBA, MMEKWISHA KUPATA UTAJIRI, MMEMILIKI PASIPO SISI. Naam, laiti mngemiliki, ili sisi nasi tumiliki pamoja nanyi!

Tabia hii iliyokuwa kwa wakristo wa korintho, ipo hadi sasa miongoni mwa watu waliomwamini Yesu Kristo kuwa ni Bwana na Mwokozi wa roho zao, wengi Mungu amewajaalia neema kubwa mno, wengine karama za miujiza na kunena kwa lugha, wengine uponyaji n.k lakini wanajiona WAMESHIBA KWA HIZO, WAMEKUWA MATAJIRI NA KUANZA KUMILIKI PASIPO MAANDIKO MATAKATIFU kama watu wa makanisa ya Korintho. Kwa sababu tu wanafufua wafu na kuponya wagonjwa, basi wanaanza kumiliki na kutawala kwa kuingiza hekima zao na elimu zao za kidunia ambazo hazitokani na Kristo na kuwa mateka wa hizo

[Wakolosai 2:8] Angalieni mtu asiwafanye mateka kwa elimu yake ya bure na madanganyo matupu, KWA JINSI YA MAPIKEO YA WANADAMU, KWA JINSI YA MAFUNDISHO YA AWALI ULIMWENGU, WALA SI KWA JINSI YA KRISTO.

Wengine wamamili kwa tamaa zao za fedha, mali, umaarufu, na si kwa mitume tena [maandiko matakatifu] sasa hii ni hatari sana katika siku hizi za mwisho, kwani wengi wanapotezwa kwa hizo filosofia na miujiza na ishara pasipo kufahamu kwamba elimu hizo na ishara hizo, sio kipimo cha ukamilifu mbele za Mungu. 

Haijarishi ni kwa jinsi gani Mungu amekujaalia neema na karama na vipawa, kamwe hatakiwi kumiliki kwa hivyo wala kwa filosofia zako ila kwa maandiko matakatifu, na tena pasipo kuyavuka yale yaliyoandikwa kwa kupunguza wala kuongeza, vinginevyo utakuwa ni mtumishi wa uongo pasipo kujijua

[1 Wakorintho 4:6] Basi ndugu, mambo hayo nimeyafanya kuwa mfano wa mimi na Apolo kwa ajili yenu, ili kwamba kwa mfano wetu MPATE KUJIFUNZA KUTOKUPITA YALE YALIYOANDIKWA; ili mmoja wenu asijivune kwa ajili ya huyu, kinyume cha mwenziwe.

Hivyo na sisi wakristo wa sasa, tusimiliki na kuatawala na kujiona kuwa tumeshiba rohoni pasipo neno la Mungu lililohubiriwa kwetu na mitume.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Bwana akubariki, Shalom.

 +255652274252/ +255789001312


Mada zinginezo:

 Je! Waraka wa mtume Paulo kwa Wakorintho, ulikuwa ni kwaajiri ya Wakorintho pekee?


INJILI YA KRISTO HAIENDI NA WAKATI


ITAMBUE NA KUIFANYA HUDUMA YA YOHANA MBATIZAJI  KATIKA UKRISTO WAKO.


Je! ni kweli karama ya kunena kwa Lugha haikupewa kipaumbele na mtume Paulo kama yafanyavyo baadhi ya makanisa leo hii?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *