JE! YESHURUNI NI NANI?

Maswali ya Biblia No Comments

Yeshuruni ni jina lingine la taifa la Israeli, lililotumika zamani hususani katika Mashairi yao.

Kumbukumbu 32:12 “Bwana peke yake alimwongoza, Wala hapakuwa na mungu mgeni pamoja naye.

13 Alimpandisha mahali pa nchi palipoinuka, Naye akala mazao ya mashamba; Akamnyonyesha asali iliyotoka jabalini, Na mafuta yaliyotoka katika mwamba wa gumegume;

14 Siagi ya ng’ombe, na maziwa ya kondoo, Pamoja na mafuta ya wana-kondoo, Kondoo waume wa Kibashani, na mbuzi, Na unono wa ngano iliyo nzuri; Ukanywa divai, damu ya mizabibu.

15 LAKINI YESHURUNI ALINENEPA, AKAPIGA TEKE; Umenenepa, umekuwa mnene, umewanda; Ndipo akamwacha Mungu aliyemfanya, Akamdharau Mwamba wa wokovu wake.

16 Wakamtia wivu kwa miungu migeni, Wakamkasirisha kwa machukizo.

17 Walitoa sadaka kwa pepo, si Mungu, Kwa miungu wasiyoijua, Kwa miungu mipya iliyotokea siku zilizo karibu, Ambayo baba zenu hawakuiogopa.

18 Humkumbuki Mwamba aliyekuzaa, Mungu aliyekuzaa umemsahau”.

Kama vile wasraeli, walijulikana pia kwa majina kama Wayahudi, Waebrania, wana wa Yakobo, binti Sayuni, kufunua tabia zao na mazingira yao, Vivyo hivyo, Mungu aliwatambua pia kwa jina la Yeshuruni, kufunua tabia waliyokuwa nayo ya kumsahau Mungu pale walipofanikishwa.

Katika maandiko hayo tunaona  Musa kwa uweza wa Roho anatoa unabii kwa Israeli, jinsi watakavyokuja kumsahau Mungu huko mbeleni watakapokuwa wamestarehe katika nchi yao ya ahadi, ibubujikayo maziwa na asali, wataanza kuabudu miungu mingine na kuisahau sheria ya Mungu. Na kweli ndivyo ilivyokuja kuwa, Israeli walipoirithi nchi yao

Neno hilo utalipata pia katika vifungu hivi;

(Kumbukumbu 33:26, Isaya 44:2)

JE! YESHURUNI ANAMFUNUA NANI KWA SASA?

Ni kila mkristo, anayemsahau Mungu, pale anapokuwa katika kustarehe, kufanikiwa, afya na uzima. Leo hii utaona kundi kubwa la watu linakuwa karibu sana na Mungu pale tu, linapopita katika majaribu makubwa aidha magonjwa, misiba, na shida, lakini pale linapofanikiwa, Mungu kwao anabakia kuwa dini tu. Kama vile kitu cha Zaida.

Hii ni hatari sana, Upendo wa kweli wa Mungu unapimwa katika nyakati zote, za raha na shida, ikiwa utatembea na Mungu katika shida tu, lakini raha humtaki, mfano wa Waisraeli au utatembea naye katika raha tu, shida humtaki, mfano wa mke wa Ayubu, ujue upendo wa Mungu haujakamilika ndani yako.

Bwana atusaidie tusiwe na mioyo ya kumsahau yeye katika hizi siku za mwisho.

Shalom.

+255652274252 / +255693036618

Mada Nyinginezo:

MIHURI SABA

UCHAMBUZI WA KITABU CHA YONA

UNYAKUO WA KANISA

VITASA SABA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *