JIHADHARI NA WAKINA BALAAMU WA NYAKATI ZA SASA.

  Siku za Mwisho, Uncategorized

Jina la Bwana Wetu na Mwokozi Wetu Yesu Kristo lihimidiwe milele na milele, karibu katika kujifunza neno la Mungu kwa pamoja, ili turekebishe yaliyopungua katika safari yetu ya hapa duniani, na kuifuata njia sahihi ya Mungu maadamu ametupa uhai.


Biblia inasema kuwa, mambo yote yaliyowapata watu wa agano la kale, yaliandikwa kwa kusudi la kutuonya, kututahadharisha, na kutufundisha sisi watu wa sasa.

[1 Wakorinto 10:11] Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, YAKAANDIKWA ILI KUTUONYA SISI, tuliofikiliwa na miisho ya zamani. 

Na mmoja wa mtu ambaye tutajifunza kwake leo hii, ni Balaamu mwana wa Boeri. Huyu Balaamu mwana wa Boeri alikuwa ni nabii  huko midiani, ambaye Mungu alikuwa akisema nae kabisa, na tena alimtabiri hadi Bwana Yesu na ujio wake na jinsi atakavyowahukumu wana wote wa uasi [Hesabu 14:17] Lakini kibaya zaidi ni kwamba, biblia inasema alikuwa ni nabii wa uongo na mchawi, na tena Bwana Yesu aliyachukia mafundisho yake [Ufunuo 2:14]. Sasa unaweza vuta picha, mtu ambaye anamtabiri hadi Yesu Kristo, tena kabla hata hajazaliwa, na Mungu azungumze nae harafu awe ni nabii wa uongo na mchawi?  Hiyo inawezekana kabisa na ndivyo ilivyo hata katika nyakati hizi za mwisho.

Huyo nabii licha tu yakuwa wa uongo na mchawi, lakini pia alikuwa ni KAIDI, kwa sababu ya tamaa za zawadi, fedha na mali, ijapokuwa mwanzo aliamua kusimama katika kweli ya Mungu.

[Hesabu 22:18] Balaamu akajibu akawaambia watumishi wa Balaki, Kama Balaki angenipa nyumba yake imejaa fedha na dhahabu, SIWEZI KUPITA MPAKA WA NENO LA BWANA, MUNGU WANGU, KULIPUNGUZA AU KULIONGEZA. 

Lakini yeye kwa tamaa aliyokuwa nayo, alimsisitiza Mungu ili aende na wajumbe wa mfalme kuliko kutii neno la Mungu, na Mungu alimruhusu lakini hasira yake iliwaka, hivyo kusudia uovu juu yake kwani alimtuma malaika ili amwangamize.

[Hesabu 22:20] Mungu akamjia Balaamu usiku, akamwambia, Kwa kuwa watu hawa wamekuja kukuita, enenda pamoja nao; lakini neno lile nitakalokuambia ndilo utakalolitenda, basi. 

21 Balaamu akaondoka asubuhi, akatandika punda wake, akaenda pamoja na wakuu wa Moabu. 

22 HASIRA YA MUNGU IKAWAKA KWA SABABU ALIKWENDA; MALAIKA WA BWANA AKAJIWEKA NJIANI, ILI KUMPIGA Basi alikuwa amepanda punda wake, na watumishi wake wawili walikuwa pamoja naye. 

Lakini kwa huruma za Mungu alinusurika kufa na kati ya wale wajumbe aliokuwa nao hakuna hata mmoja ambaye alifahamu kuwa, Balaam alionywa na Mungu lakini hakukubari, tena hadi mfalme akayakubari mafundisho yake maovu na kuyafuata.


HIYO INAFUNUA NINI SIKU HIZI ZA MWISHO?Nyakati hizi za mwisho pia kuna wakina Balaamu wengi sana ambao ni WAKAIDI, waongo na wachawi ijapokuwa Mungu amewapa vipawa na unapako. Wengine ni mitume, wengine manabii, wengine ni wainjilisti, na wengine ni wachungaji na waalimu. 


Ijapokuwa wana hivyo vipawa, lakini ni wa kaidi wa neno la Mungu kama alivyokuwa Balaamu, kwani hivyo vipawa Mungu anawapa hata watu wakaidi. 

[Zaburi 68:18] Wewe umepaa juu, umeteka mateka, Umepewa vipawa katikati ya wanadamu; NAAM, HATA WAKAIDI, Bwana Mungu akae nao. 

Kwa tamaa za mali, fedha, na anasa za dunia hii, wanashindwa kusimama katika kweli ya Mungu na Mungu anawaacha katika tamaa zao ila anakusudia uovu juu ya kama vile alivyofanya kwa Balaamu, watu hawa wana wahadaha watu na kuwadanganya kwa mafundisho yao ya uongo na kuwapoteza watu hao pamoja nao katika siku hizi za mwisho, ni watu waliyoacha kweli ya Mungu na kuifuata njia ya Balaamu kama maandiko yanavyosema..

[2 Petro 2:15] wakiiacha njia iliyonyoka, wakapotea, wakiifuata njia ya Balaamu, mwana wa Beori, aliyependa ujira wa udhalimu; 

Wanapinga maagizo ya Mungu kama ubatizo wa maji mengi na kwa jina la Yesu,   utakatifu wa ndani na nje n.k 

Lakini mimi na wewe tutajuaje kama watu hawa wameonywa na Mungu lakini wamekaidi? Kumbuka, hata mfalme wa Moabu na wajumbe wake, hawakutambua kuwa, Balaamu ameonywa na Mungu? Je! Tuwafuate na kuwauliza? Jibu ni hapana! Kwani hakuna atakayekiri kwamba yeye ni mtume au mchungaji wa uongo, hivyo tufanye nini basi? Hatuna budi kukaa chini na kusoma biblia zetu kwa msaada wa Roho Mtakatifu, neno la Mungu ndilo lituongoze mahari sahihi na wala sio miujiza, wala maji ya upako, wala masanamu n.k 

[Matayo 7:24] Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba; 

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Bwana akubariki, Shalom.

 +255652274252/ +255789001312


MADA ZINGINEZO:

BASI WAKIWAAMBIA, YUKO JANGWANI, MSITOKE; YUMO NYUMBANI, MSISADIKI. 


MADHARA YA KUTOKUSOMA BIBLIA YAKO.Ni Mtume gani aliyekuwa Mkuu na Wa kwanza  kuliko wote katika biblia?


Ni hukumu ipi ya Ibilisi inayozungumziwa katika Waraka wa (1 Timotheo 3:6?)

LEAVE A COMMENT