Ni Mtume gani aliyekuwa Mkuu na Wa kwanza  kuliko wote katika biblia?


JIBU: Tofauti na wengi wetu tunavyodhani leo hii kuwa mtume aliyekuwa mkuu na wa kwanza kuliko wote kwenye biblia alikuwa ni Petro, na wengi tunadhani hivyo kutokana na maneo kadha wa kadha ambayo Bwana aliyokuwa akiyanena juu ya Petro, na moja ya maneno hayo ambayo Bwana alimwambia Petro ni pale walipokuwa ufukweni na kumwambia alishe kondoo wake.


Yohana 21:15  Basi walipokwisha kula, Yesu akamwambia Simoni Petro, Je! Simoni wa Yohana, wewe wanipenda 

16 Akamwambia tena mara ya pili, Simoni wa Yohana, wanipenda? Akamwambia, Ndiyo, Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda. Akamwambia, Chunga kondoo zangu. 

17 Akamwambia mara ya tatu, Simoni wa Yohana, wanipenda? Petro alihuzunika kwa vile alivyomwambia mara ya tatu, Wanipenda? Akamwambia, Bwana, wewe wajua yote; wewe umetambua ya kuwa nakupenda. Yesu akamwambia, Lisha kondoo zangu. 


Kwa maneno hayo na mengine yote, hayakufanya Petro kuwa mtume mkuu wala wa kwanza. Na wala si yeye tu, bali hata Yohana na Yakobo pia, hao ni mitume ambao walipata neema hiyo ya kuwa karibu na Bwana kuliko wengine.


Sasa utauliza, je! Hakukuwa na Mtume Mkuu na wa kwanza? Na kama alikuwepo alikuwa ni nani?

Jibu ni kwamba, Mtume Mkuu na wa kwanza kuliko wote alikuwepo, na yupo hata sasa, na bado anaendelea kuwatuma mitume wengine, na Mtume huyo Mkuu na wa kwanza si mwingine bali ni Yesu Kristo Mwenyewe (Mungu katika mwili), huyo ndiye Mtume Mkuu kuliko wote na wa kwanza.

Ili tuelewe vizuri tusome kifungu kifuatacho cha kwenye maandiko.

Yohana 17:18  Kama vile ULIVYONITUMA MIMI ULIMWENGUNI, NAMI VIVYO HIVYO NALIWATUMA HAO ULIMWENGUNI.

Umeona hapo ni Mtume gani aliyekuwa Mkuu na Wakwanza kutumwa ulimwenguni? Ni Yesu Kristo, ndiye aliyekuwa Mkuu na wa kwanza kutumwa ulimwenguni kisha na yeye akawatuma wengine ambao, wa kwanza ni wale mitume kumi na wawili, na kisha kufuata wengine mbali mbali kama, Androniko na Yunia ambao tunawasoma katika kitabu cha Warumi 16:7, akina Barnaba na Paulo na wengine wengi wengi na hata wa sasa pia wapo.

Waefeso 4:8  Hivyo husema, Alipopaa juu aliteka mateka, AKAWAPA WANADAMU VIPAWA.

 9 Basi neno hilo, Alipaa, maana yake nini kama siyo kusema kwamba yeye naye alishuka mpaka pande zilizo chini za nchi?

 10 Naye aliyeshuka NDIYE YEYE ALIYEPAA JUU SANA KUPITA MBINGU ZOTE, ILI AVIJAZE VITU VYOTE. 

11 NAYE ALITOA WENGINE KUWA MITUME, NA WENGINE KUWA MANABII; NA WENGINE KUWA WAINJILISTI NA WENGINE KUWA WACHUNGAJI NA WAALIMU; 

Kristo kama Mkuu, ndiye aliyepaa juu na kuwapa wanadamu vipawa, kumaanisha kuwa yeye ndiye mkuu wa hivyo vipawa vyote tunavyivisoma kwenye mstari wa 11, yeye ndiye Mtume Mkuu, yeye ndiye Nabii Mkuu, yeye ndiye Mwinjilisti Mkuu, yeye ndiye Mchungaji Mkuu na Mwalimu Mkuu, hawa wengine wote ni wachungaji na mitume na manabii na wainjilisti na waalimu lakini si wakuu, aliye Mkuu ni Mmoja tu Yesu Kristo, ndiye aliye juu ya vyote, hivyo mtu yeyote anayejiita nabii mkuu au baba mkuu au mwalimu mkuu ni mwongo.


Tafadhari washirikishe na wengine ujumbe huu.

+255652274252/ +255789001312

Bwana akubariki, Shalom.



MADA ZINGINEZO

MAANA, TAZAMA, MIMI NAUMBA MBINGU MPYA NA NCHI MPYA.


KAMA YOSHUA ANGALIWAPA RAHA, ASINGALIINENA SIKU NYINGINE BAADAE. 



KWA SABABU NALIWAOGOPA WALE WATU, NIKATII SAUTI YAO. 



Waliotakaswa kwa imani iliyo kwangu mimi. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *