Waliotakaswa kwa imani iliyo kwangu mimi. 

  Biblia kwa kina, Uncategorized

Shalom, Bwana Yesu apewe sifa. Ukisoma maandiko utakungua kuwa mtume Paulo alitokewa na Bwana Yesu wakati akiwa njiani kwenda kuwakamata Wakristo waliokimbilia Dameski, na kusudi au sababu ya Bwana kumtokea Paulo maandiko yanaeleza.

Matendo Ya Mitume 26:16 Lakini inuka, usimame kwa miguu yako, MAANA NIMEKUTOKEA KWA SABABU HII, NIKUWEKE  WEWE UWE MTUMISHI NA SHAHIDI WA MAMBO HAYA ULIYOYAONA , na wa mambo ambayo katika hayo nitajidhihirisha kwako;

 17 nikikuokoa na watu wako, na watu wa Mataifa, ambao nakutuma kwao; 

18 UWAFUMBUE MACHO YAO, NA KUWAGEUZA WAIACHE GIZA NA KUIELEKEA NURU, waziache na nguvu za Shetani na kumwelekea Mungu; KISHA WAPATE MSAMAHA WA DHAMBI ZAO, NA URITHI MIONGONI MWAO WALIOTAKASWA KWA IMANI ILIYO KWANNGU MIMI. 

Nachotaka uone ni kuwa, zamani watu wa mataifa hawakuwa na Mungu bali miungu, waliabudu miti, milima, masanamu, nyota, mizimu n.k na hivyo kuwa gizani wakimwabudu shetani bila kujua, japokuwa walitenda hayo lakini Mungu alikuwa akiwapa mvua  na chakula na furaha.

Matendo Ya Mitume 14:14  Walakini mitume Barnaba na Paulo, walipopata habari, wakararua nguo zao, wakaenda mbio wakaingia katika makutano, wakipiga kelele, 

15 wakisema, Akina bwana, mbona mnafanya haya? Sisi nasi tu wanadamu hali moja na ninyi; twawahubiri habari njema, ili mgeuke na kuyaacha mambo haya ya ubatili na kumwelekea Mungu aliye hai, aliyeumba mbingu na nchi na bahari na vitu vyote vilivyomo; 

16 AMBAYE ZAMANI ZILIZOPITA ALIWAACHA MATAIFA YOTE WAENDE KATIKA NJIA ZAO WENYEWE.

 17 LAKINI HAKUJIACHA PASIPO USHUHUDA, KWA KUWA ALITENDA MEMA, AKIWAPENI MVUA KUTOKA MBINGUNI, NA NYAKATI ZA MAVUNO, akiwashibisha mioyo yenu CHAKULA na RURAHA. 

Na matendo yote hayo ya mataifa yalikuwa ni uovu mbele za Mungu na ndio maana sasa, tuapoyaacha hayo mambo ya giza na kuelekea nuru tunapata msamaha wa Dhambi na kuwa warithi miongoni mwa waliotakaswa kwa imani iliyo kwa Bwana Yesu

Matendo Ya Mitume 26:18 uwafumbue macho yao, na kuwageuza waiache giza na kuielekea nuru, waziache na nguvu za Shetani na kumwelekea Mungu; kisha WAPATE MSAMAHA WA DHAMBI ZAO, na urithi miongoni mwao waliotakaswa kwa IMANI ILIYO KWANGU  MIMI. 

Ili tuwe warithi wa uzima wa milele ni lazima tutakaswe kwa imani iliyo kwa Bwana Yesu tu, hakuna imani nyingine tofauti na ya Bwana Yesu itakayomfanya mwanadamu awe mrithi wa uzima wa milele, lakini Bwana Yesu alisema watotokea makristo wengi na manabii wengi wa UONGO ambao wataleta imani zao tofauti na ile ya Bwana Yesu ambayo inamtakasa mtu na kumpa uzima wa milele, sasa lengo la hao makristo wa uongo ni kuwafanya watu wasiweze kuurithi uzima wa milele.

Sasa swali ni je! Na wewe mkristo umetakswa kwa umani iliyo kwa Bwana Yesu? Kwasababu sasa hivi kuna imani nyingi sana na zote zinadai kuwa ni za kikristo, kuna madhebu mengi sana yenye imani tofauti tofauti na yote yanadai kuwa ni ya kikristo, je umetakaswa kwa imani ipi? Kwani katika ukristo hakuna imani nyingi wala utofauti bali imani ni moja tu kama maandiko yanavyosema.

Waefeso 4:5  Bwana mmoja, IMANI MOJA, ubatizo mmoja. 

Hivyo ni jukumu lako wewe kama mkristo unayetafuta kwenda mbinguni kuhakikisha kuwa unatakaswa kwa imani iliyo kwa Bwana Yesu, ni jukumu lako kusoma maandiko na kumwomba Roho mtakatifu akuoneshe njia iliyo sahihi ili upate msamaha wa dhambi na kuwa mrithi miongoni mwa walio takaswa kwa imani iliyo kwa Bwana Yesu.

Bwana akubariki. Shalom.


MADA ZINGINEZO:

Je! Umeiamini Injili Ipi?


KANISA LA KWELI NI LIPI DUNIANI?


Je ubatizo sahihi ni kwa jina la Yesu au Baba, Mwana na Roho Mtakatifu?

LEAVE A COMMENT