DAMU YAKE NA IWE JUU YETU.

  Biblia kwa kina, Uncategorized

Shalom, Jina la Bwana Yesu na Mkuu wa uzima litukuzwe milele. Karibu tuyatafakari maneno ya uzima ya mwokozi wetu ambayo ndiyo chakula cha roho zetu kama maandiko yanavyosema kuwa mtu hatoishi kwa mkate tu, bali kwa kila neno litokalo kwa Mungu.

Ukisoma maandiko utagundua kuwa, Mungu huwa ana thamini sana damu ya mwenye haki ambaye anauwawa kwa fitina na siku zote damu hiyo huwa ina thamani sana mbele za Mungu na Mungu atakuja kuitaka damu hiyo juu ya wote waliofanya uovu kwa kumwanganiza huyo mwenye haki, utakumbuka kile kipindi ambacho Bwana Yesu alipowakemea waandishi na mafarisayo wanafki, juu ya matendo yao maovu kwa watumishi wa Mungu, aliwaambia kuwa, wanayoyafanya ndiyo yaliyofanywa na baba zao, ambao waliwauwa manabii na wenye haki na damu za hao wote wenye haki zitatakwa juu yao kwenye hukumu ya Jehanam, kuanzia damu ya Habili hadi Zakaria bin Barakia

Matayo 23:31  Hivi mwajishuhudia wenyewe, ya kwamba ninyi ni wana wao waliowaua manabii.

 32 Kijazeni basi kipimo cha baba zenu.

 33 Enyi nyoka, wana wa majoka, mtaikimbiaje HUKUMU YA JEHANAM?

 34 Kwa sababu hiyo, angalieni, mimi natuma kwenu manabii na wenye hekima na waandishi; na wengine wao ninyi mtawaua na kuwasulibisha, na wengine wao mtawapiga katika masinagogi yenu, na kuwafukuza mji kwa mji; 

35 hivyo IJE JUU YENU DAMU YOYE YA HAKI iliyomwagika juu ya nchi, tangu damu ya Habili, yule mwenye haki, hata damu ya Zakaria bin Barakia, mliyemwua kati ya patakatifu na madhabahu. 

Lakini ukiendelea mbele hadi mstari wa 36,  Bwana Yesu anasema kuwa, mambo hayo yatakuha juu ya kizazi hiki, juu ya kizazi ambacho tupo mimi na wewe.

Matayo 23:36  Amin, nawaambieni, Mambo hayo yote YATAKUJA JUU YA KIZAZI  HIKI. 

Sasa unaweza jiuliza, kama hadi kizazi hiki nacho kinausika, sasa Mungu ataitaka iyo damu juu ya watu gani? Na mwenye haki gani huyo?  Ili uelewe kwamba Mungu ataitaka hiyo damu juu ya watu gani  na mwenye haki gani tusome.

Matayo 27:24 Basi Pilato alipoona ya kuwa hafai lo lote, bali ghasia inazidi tu, akatwaa maji, akanawa mikono yake mbele ya mkutano, akasema, Mimi sina hatia katika damu ya mtu huyu mwenye haki; yaangalieni haya ninyi wenyewe.

 25 Watu wote wakajibu wakasema, DAMU  YAKE NA IWE JUU YETU, na juu ya watoto wetu. 

Damu ya mwenye haki ambayo Mungu ataitaka pia juu ya kizazi hiki ni damu ya Bwana wetu Yesu Kristo iliyomwagika pale msalabani, na damu hiyo Mungu ataitaka juu ya wote waliotamka maneno hayo kuwa, DAMU YAKE NA IWE JUU YETU na juu ya watoto zetu, sasa waliotamka hayo maneno maandiko yanatuambia kuwa, ni WENYE DHAMBI au watenda dhambi.

Luka 24:7  akisema, Imempasa Mwana wa Adamu kutiwa MIKONONI MWA WENYE DHAMBI, na kusulibiwa, na kufufuka siku ya tatu. 

Hivyo damu ya mwenye haki Yesu Kristo, itatakwa, na ipo juu ya WATENDA DHAMBI wote wa kizazi hiki, na Mungu ataitaka  damu hiyo juu yao katika hukumu ya Jehanam, damu ya mwenye haki Yesu Kristo ipo juu ya wazinzi wote, ipo juu ya watukanaji wote, ipo juu ya walevi wote, ipo juu ya wauaji wote, ipo juu ya walawiti na wasagaji wote, na Mungu ataitaka hiyo damu siku ya hukumu Jehanam. Kwasabau Kristo alikufa msalabani ili wanadamu wapate msamaha wa dhambi zao, ili damu ya Mwana wa Mungu isitakwe juu yao. 

Ndugu yangu kama unataka damu hii Mungu asiitake juu yako, utakua umefanya uamuzi mzuri sana ambao hautoujutia katika maisha yako, unachotakiwa kufanya ni kudhamiria ndani moyo wako kuacha dhambi zote, dhamiria kuacha uchafu wote kama uzinzi ulevi, uvaaji vimini na suruali kwa wanawake, mapambo n.k kisha mwamini Bwana Yesu kuwa ni Bwana na mwokozi wa maisha yako na kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi ambao ni wa MAJI MENGI NA KWA JINA LA YESU sawa sawa na matendo 19:5 matendo 10:48 na kupokea Roho mtakatifu ambaye atakuwezesha kuwa mtakatifu kama yeye alivyo na kukupa uelewa wa maandiko.

Bwana akubariki, Shalom.MADA ZINGINEZO

UMEFUNGULIWA KAMA BARABA?


Je! Binti kujipamba mwili wake si ni jambo jema kwani atakua analipamba hekalu la Mungu?

LEAVE A COMMENT