Bwana alimaanisha nini katika  (Mathayo 24:46)?

  Maswali ya Biblia, Uncategorized

Matayo 24:46  Heri mtumwa yule, ambaye bwana wake ajapo atamkuta akifanya hivyo. 

Jibu: Maneno hayo aliyasema Bwana Yesu baada ya kujibu swali aliloulizwa na mtume Petro, sasa Ili tuelewe vizuri tusome katika kitabu cha Luka.

Luka 12:41  Petro akamwambia, Bwana, mithali hiyo umetuambia sisi tu, au watu wote pia?

42  Bwana akasema, Ni nani, basi, aliye wakili mwaminifu, mwenye busara, ambaye bwana wake ATAMWEKA JUU YA UTUMISHI WAKE WOTE, AWAPE WATU POSHO KWA WAKATI WAKE?

 43  HERI MTUMWA YULE, AMBAYE BWANA WAKE AJAPO ATAMKUTA ANAFANYA HIVYO. 

Sasa hapo kuna vitu viwili ambavyo Bwana Yesu alivisema katika jibu lake, cha kwanza ni KUMWEKA MTUMWA KWENYE UTUMISHI WAKE na cha pili ni MTUMWA KUWAPA POSHO WATU WAKE, sasa mtumwa kama huyo ambaye amewekwa kwenye utumishi, na kuwapa watu wa huyo mfalme posho kwa wakati wake, basi huyo mtumwa atakuwa na heri sana endapo Bwana wake akirudi na kumkuta akifanya hivyo, na posho iliyozungumziwa hapo sio chakula hiki cha mwilini ambacho tunakula kila siku, bali ni chakula cha rohoni ambacho ni neno la Mungu, na ndio maana Sehemu nyingine pia Bwana alimwambia mtume Petro lisha kondoo wangu, akimaanisha chakula ambacho ni maneno yake Kristo mwenye (Yohana 21:17).  Sasa huyo mtumwa anachopaswa kuwalisha watu wa mfalme ni nini? Au ni nini daima anachopaswa kuwapa watu wa mfalme wake, jibu tunasoma katika 

Matayo 24:42  Kesheni basi; kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu.

43 Lakini fahamuni neno hili; kama mwenye nyumba angaliijua ile zamu mwivi atakayokuja, angalikesha, wala asingaliiacha nyumba yake kuvunjwa.

 44 KWA SABABU HIYO NINYI NANYI JIWEKENI TAYARI; KWA KUWA KATIKA SAA MSIYODHANI MWANA WA ADAMU YUAJA. 

45 Ni nani basi yule mtumwa mwaminifu mwenye akili, ambaye bwana wake ALIMWEKA JUU YA NYUMBA YAKE, AWAPE WATU CHAKULA KWA WAKATI WAKE? 

Kumbe chakula ambacho hawa watumwa wanatakiwa kuwapa watu wa huyo mfalme ni kuwaweka tayari, kuwafanya wawe katika hali ya kukesha ya kumngojea mfalme wao, kuwafanya wawe na vigezo vyote ambavyo vitawafanya wao kuweza kustahili ile siku ambayo mfalme wao atakapokuja, yaani kuhimiza juu ya utakatifu na kufanya mapenzi ya Mungu, mtumwa kama huyo mfalme atakapokuja atamweka juu sana

sasa mfalme anayezungumziwa hapo ni Yesu Kristo na kuja kwake ni ujio ule aliousema kama katika (Yohana 14:1-3) na ndio maana utaona watumwa wa Kristo wa wakati ule, yaani mitume, waliwafundisha watu na kuwahimiza juu ya utakatifu, juu ya kuyashika na kuyafanya mapenzi ya Mungu, tangu siku ile wanawekwa kuwa watumishi hadi walipofikia uzeeni, mfano mtume Petro.

1 Petro 5:1  Nawasihi wazee walio kwenu, MIMI NILIYE MZEE, MWENZI WAO, NA SHAHIDI WA MATESO YA KRISTO, na mshirika wa utukufu utakaofunuliwa baadaye; 

2 lichungeni kundi la Mungu lililo kwenu, na kulisimamia, si kwa kulazimishwa, bali kwa hiari kama Mungu atakavyo; si kwa kutaka fedha ya aibu, bali kwa moyo. 

3 Wala si kama wajifanyao mabwana juu ya mitaa yao, bali kwa kujifanya vielelezo kwa lile kundi. 

4 Na Mchungaji mkuu atakapodhihirishwa, MTAIPOKEA TAJI YA UTUKUFU, ILE ISIYOKAUKA. 

Lakini mambo ni tofauti kwa watumishi wa Mungu wa sasa, wengi wameacha kuhimiza tena kondoo wa mfalme Yesu Kristo juu ya kujiweka tayari ili kumlaki Mfalme wao, wameacha kuhimiza utakatifu, wameacha kuimiza upendo, wameacha kuhimiza watu kufanya na kushika maagizo ya Bwana Yesu, wengi wanahubiri fahari za ulimwengu huu kama magari, majumba n.k hawakemei tena uvaaji mbaya kwa wanawake na wanaume, hawawaonyi watu tena juu ya uzinzi na ulevi, sasa watumwa kama hao, maandiko yanasema kuwa, ile siku ambayo YESU KRISTO atakapokuja, atawakata vipande viwili na kumwekea fungu lake pamoja na wanafki. 

Matayo 24:50 bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani, na saa asiyojua,

 51 atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na wanafiki; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno. 

Hivyo kama wewe  ni mtumishi wa Mungu, basi hakikisha unawaandaa kondoo wa Bwana kwaajiri ya kumlaki mfalme wao, haikisha unahimiza utakatifu, na watu kuyafanya mapenzi ya Mungu, ili ile siku Bwana atakapokuja akuweke juu ya vitu vyake vyote.

Bwana akubariki. Shalom, 

Tafadhali washilikishe na wengine habari hii njema.


MADA ZINGINEZO

Mana ni nini katika maandiko?


Pazia la Hekalu ni nini katika biblia?

2 thoughts on - Bwana alimaanisha nini katika  (Mathayo 24:46)?

LEAVE A COMMENT