Pazia la Hekalu ni nini katika biblia?

  Maswali ya Biblia, Uncategorized

SWALI: Pazia la hekalu ni kitu gani? Na kwanini lipasuke kuanzia juu hata chini? Na linafunua kitu gani?

JIBU: Pazia la hekalu lilikua ni pazia lililofumwa kwa nyuzi za rangi ya samawi ( blue) , dhambarau na nyekundu na nguo za kitani zilizosokotwa na kutiwa makerubi

Kutoka 26:31   Nawe fanya pazia la nyuzi za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na za rangi nyekundu, na nguo za kitani nzuri zenye kusokotwa, litafumwa na kutiwa makerubi, kazi ya fundi stadi; 

Sasa kazi ya hili pazia ilikua ni kutenganisha sehemu mbili tofauti katika ile maskani ambayo Bwana alimwamuru Musa aitengeneze kwa mfano aliomwonyesha kule mlimani na sehemu zenyewe zilikua ni PATAKATIFU na PATAKATIFU SANA (patakatifu pa patakatifu) 

Patakatifu ndipo palipokuwa na kile kinara cha taa, na meza, na mikate ya wonyesho.

Patakatifu sana ndipo palipokuwa na chetezo cha dhahabu, sanduku la agano lililofunikwa kwa dhahabu pande zote na palikuwamo na kopo la dhahabu lenye ile mana na ile fimbo ya haruni iliyochipuka na zile mbao za agano na juu yake makerubi na kiti cha rehema. 

Sasa kwa wakati huo kule kwenye kiti cha rehema hakupaswa kuingia mtu yoyote isipokua kuhani tu, na tena ni mara moja kwa mwaka kwa ajiri ya kwenda kufanya upatanisho wa dhambi za wana wa Israel na kukilaribia kile kiti cha rehema.  Hivyo basi lile pazia lilitenganisha hizo sehemu mbili yaani patakatifu na PATAKATIFU sana ambapo pana kile kiti cha rehema.

Sasa kwetu sisi watu wa agano jipya tunafahamu kuwa lile pazia ni mwili wa Bwana na mwokozi wetu Yesu Kristo na pazia kupasuka ni kumaanisha kifo cha Bwana Yesu yaani mwili wake.  Sasa kama pazia la hekalu limepasuka maana yake ni kuwa hakuna tena kizuizi cha sisi kukikaribia kiti cha rehema kwahivyo basi, kwa kifo cha Bwana Yesu sisi tumefunguliwa njia ya kukikaribia kiti cha rehema wenyewe na kupata ondoleo la dhambi zetu kabisa kwa ile damu yake 

Waebrania 10:19   Basi, ndugu, kwa kuwa tuna ujasiri wa kupaingia patakatifu kwa damu ya Yesu, 

20 njia ile aliyotuanzia iliyo mpya, iliyo hai, ipitayo katika pazia, yaani, mwili wake; 

      Tunakikalibiaje kiti huki cha rehema ?

Sasa hiki kiti cha rehema tunakikaribia kwanza kwa kutubu dhambi zetu zote na kudhamiria kuto kuzitenda tena na kumwamini Bwana Yesu na kisha kubatizwa katika ubatizo sahihi ambao ni wa maji mengi na kwa jina a YESU na kisha yeye mwenyewe atakupa uwezo wa kushinda dhambi na kuishi maisha matakatifu.

Ndugu yangu kama bado hujampokea Bwana Yesu na kubatizwa katika ubatizo sahihi fahamu kuwa wewe bado hujakiendea kiti hiki cha rehema, shetani hataki wewe ukiendee hicho kiti na ndio maana atakupa ubatizo mwengine ambao ni batili na kukufanya uishi maisha ya uzinz na uasherati, utukanaji, ulevi, chuki, uongo, uuaji n.k hivyo amua leo ndani ya moyo kukiendea kiti hiki kwa usahihi.  Na kama bado hujakiendea kiti hiki basi uamuzi ni leo tubu dhambi zako na ukabatizwe katika ubatizo sahihi kulingana na maandiko. Ndugu yangu fahamu kuwa siku za kukiendea kiti hiki zimebaki chache sana na neema hiyo itafungwa hivyo wahi sasa kuingia na kukiendea kiti hiki.

Luka 13:24   Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze. 

25 Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako; 

26 ndipo mtakapoanza kusema, Tulikula na kunywa mbele yako, nawe ulifundisha katika njia zetu. 

27 Naye atasema, Nawaambia, Siwajui mtokako; ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu. 

28 Ndipo kutakapokuwa na kilio na kusaga meno, mtakapomwona Ibrahimu na Isaka na Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, nanyi wenyewe mmetupwa nje. 

Bwana akubariki, Shalom.


Mada zinginezo:

Mana ni nini katika maandiko?


Makuhani wa Mungu ni watu gani katika biblia?


Ni Mtume gani aliyekuwa Mkuu na Wa kwanza  kuliko wote katika biblia?


Bwana alimaanisha nini katika  (Mathayo 24:46)?


Ni maneno yapi ya unabii yaliyotangulia juu ya Timotheo? (Kulingana na 1 Timotheo 1:18)

LEAVE A COMMENT