Ni maneno yapi ya unabii yaliyotangulia juu ya Timotheo? (Kulingana na 1 Timotheo 1:18)

1 Timotheo 1:18  Mwanangu Timotheo, nakukabidhi agizo hilo liwe akiba, KWA AJILI YA MANENO YA UNABII YALIYOTANGULIA  JUU YAKO, ili katika hayo uvipige vile vita vizuri; 

SWALI: Ni maneno yapi hayo ya unabii yaliyotangulia juu ya Timotheo ambayo mtume Paulo anayazungumzia katika waraka wake wa kwanza kwa Timotheo?

JIBU: Kwanza inabidi tufahamu kuwa, hapo anaposema “maneno ya unabii” anamaanisha unabii zaidi ya mmoja uliyotolewa kwa ajiri yake Timotheo, lakini WENYE UJUMBE MMOJA.

Mfano: Mtume Paulo na yeye alipewa maneno ya unabii au unabii zaidi ya mmoja uliotangulia juu yake lakini wenye UJUMBE MMOJA na  ujumbe huo si mwengine zaidi ya shida atakazokutana nazo Yerusalemu, labda tusome kidogo.

Matendo Ya Mitume 21:4  Tukiisha kuwaona wanafunzi tukakaa huko siku saba, NAO WAKAMWAMBIA  PAULO KWA UWEZA WA ROHO ASIPANDE KWENDA YERUSALEMU. 

Teana baada ya siku nyingi, anapewa unabii mwengine na Agabo wenye ujumbe huo huo.

Matendo Ya Mitume 21:10  Basi tulipokuwa tukikaa huko siku nyingi, nabii mmoja jina lake Agabo akashuka kutoka Uyahudi.

 11 Alipotufikia akautwaa mshipi wa Paulo, akajifunga miguu na mikono, akasema, Roho Mtakatifu asema hivi, Hivyo ndivyo Wayahudi wa Yerusalemu watakavyomfunga mtu mwenye mshipi huu, nao watamtia katika mikono ya watu wa Mataifa. 

Hivyo basi, maneno ya unabii yaliyotangulia juu ya Timotheo yanaweza yakawa tofauti tofauti lakini yenye UJUMBE MMOJA kama tulivyoona hapo juu. Sasa maandiko hayajaweka wazi maneno hayo kama ilivyokuwa kwa Paulo lakini tunaweza elewa kwa ujumbe uliobebwa kwenye nabii  hizo.

Sasa ili tuelewe vizuri ujumbe wa nabii hizo ulikuwa ni nini, labda tusome tena kwenye kile kufungu.

1 Timotheo 1:18  Mwanangu Timotheo, nakukabidhi agizo hilo liwe akiba, kwa ajili ya maneno ya unabii yaliyotangulia juu yako, ILI KATIKA HAYO UVIPIGE VILE VITA VIZURI; 

Sasa vita inayoongelewa hapo ni vita ya kusambaza neno la Mungu la kweli kwa dunia. Hivyo basi, maneno hayo ya unabii yaliyotangulia juu ya Timotheo yalihusu huduma yake ya kuifanya kazi ya Mungu ya kuhubiri injili ya kweli ya msalaba kama alivyomwandikia mtume Paulo katika waraka wake wa pili.

2 Timotheo 4:5  Bali wewe, uwe na kiasi katika mambo yote, vumilia mabaya, FANYA  KAZI YA MHUBIRI WA INJILI, TIMILIZA  HUDUMA YAKO. 

Hivyo basi, maneno ya unabii au ujumbe wa nabii hizo zilikuwa zinahusu huduma ya Timotheo ya kuifanya kazi ya Mhubiri wa injili.

Vivyo hivyo na sisi pia tulio katika Kristo, hatuna budi kuvipiga vita vizuri katika maneno yaliyotangulia juu yetu na karama tulizopewa, Kama ni uimbaji basi, tufanye kwa nguvu zetu zote, kama ni uwalimu, unabii, uinjiristi n.k pia tufanye kwa nguvu zote, kwa kadiri tulivyojaariwa neema na Bwana wetu Yesu Kristo.

Bwana akubariki, Shalom.

Tafadhari washirikishe na wengine habari hii.

Maran atha!


MADA ZINGINEZO

UMEFUNGULIWA KAMA BARABA?


Nini maana ya wanawake saba watamshika mume mmoja?( Isaya 4:1)


Je! Ni kweli mshahara wa dhambi ni mauti na si moto wa milele?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *