ALIKUWA HAMJUI BWANA BADO, NA NENO LA BWANA LILIKUWA BADO HALIJAFUNULIWA KWAKE.

  Biblia kwa kina, Uncategorized

Shalom, jina la Bwana wetu Yesu Kristo lipewe sifa milele na milele. Nakukaribisha katika kujifunza neno la Mungu ambalo ndio taa ya miguu yetu inayotuongoza katika kuufikia ufalme wa Bwana wetu Yesu Kristo.

Leo napenda tumtazame  mtu mmoja katika biblia, ili kupitia yeye na sisi tujifunze kitu kutoka kwake, na mtu huyo si mwengine bali ni  nabii Samweli. Maandiko yanamtaja Samweli kuwa, alishindwa kumtambua Mungu pale sauti yake ilipomwita kwa mara ya kwanza katika maisha yake, na sababu ya kushindwa biblia inaeleza kuwa, ALIKUWA HAMJUI BWANA BADO na NENO LA BWANA LILIKUWA BADO HALIJAFUNULIWA KWAKE, sasa labda tusome kidogo.

1 Samueli 3: 6 Bwana akaita mara ya pili, Samweli! Samweli! Akaondoka akamwendea Eli, akasema, Mimi hapa; kwa maana uliniita. Akajibu, Sikukuita, mwanangu; kalale tena.

 7 Basi Samweli ALIKUWA HAMJUI BWANA BADO na NENO LA BWANA LILIKUWA BADO HALIJAFUNULIWA KWAKE. 

Sasa kumjua Bwana hapo kunapozungumziwa sio kumjua kwa kufahamu kwamba kuna Mungu au kwamba hajawahi kumsikia akitajwa na watu hapana, bali ni katika mahusiano binafsi kati yake yeye na Bwana. Lakini sababu ni kwamba NENO la Bwana lilikuwa bado alijafunuliwa kwake hadi sasa wakati alipopata mwongozo wa nini cha kufanya (mahubiri) kutoka kwa Eli.

Sasa hichi kitu kilichomtokea Samweli ndicho kinachoendelea sasa hivi, watu wengi hawamjui Bwana si kwasabubu hawajawahi kufahamu kuwa kuna Mungu aliyeumba mbingu na nchi hapana, bali ni kwasabubu NENO la Mungu bado alijafunuliwa kwao kama ilivyokuwa kwa Samweli. Sasa maandiko yanasema kuwa, neno la Mungu ni Yesu Kristo (Yohana 1:1) hivyo sasa, ili tumfahamu Mungu ni lazima Yesu Kristo (neno) afunuliwe kwetu, hakuna namna nyingine tutakayoweza kumfahamu Mungu kama Kristo hajafunuliwa kwetu, hakuna. Sasa ni kwa jinsi gani Kristo anafunuliwa kwetu? Jibu ni rahisi tu, kama vile Samweli alivyopewa na kusikia mahubiri yale (neno la Mungu)  kutoka kwa Eli na kutii, ndivyo ilivyo hata kwetu sisi  sasa hivi, ni lazima tusikie  neno la Mungu (ambalo ni Yesu Kristo) na kulitii ili tuweze kumfahamu Mungu katika maisha yetu, na tunasikia neno la Mungu pale tunapohubiriwa na mhubiri kama maandiko yanavyosema.

Warumi 10:14  Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? TENA WAMSIKIAJE PASIPO MHUBIRI? 

Lakini kinachoteka sasa hivi ni kinyume chake, watu hawataki hata kuyasikia hayo mahubiri kama Samweli alivyosikia kutoka kwa Eli, na bado tunataka kumwona Mungu, ndugu yangu kumbuka alichokifanya Samweli, huna budi kusikia na kutii, huna budi kusikia, kutii, kutubu dhambi zako zote na kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi ili upate  ondoleo la dhambi na umfahamu Mungu na mapenzi yake, huna budi kutii na kukubali kuacha uvaaji wako wa mawigi, mahereni, kucha bandia, vimini na suruali, huna budi kutii na kuacha ulevi, huna budi kutii na kukubali kuacha uzinzi na uasherati unaoufanya kwa kuishi na mwanamke au mwanaume ambaye hujafunga nae ndoa, huna budi kutii na kukubali kuacha chuki na usengenyaji uonaoufanya, huna budi kutii na kukubali kuacha utazamaji wa picha chafu mitandaoni ili Mungu awe karibu na wewe.

Yakobo 4:8 Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili. 

Tafadhari shea na wengine habari hii njema, Bwana akubariki, Shalom.

Maran atha! MADA ZINGINEZO

Je! Ni kweli majuma sabini aliyoambiwa Daniel yamekwisha timia?(Daniel 9:23-27)


WAO SI WA ULIMWENGU


JIANGALIENI BASI JINSI MSIKIAVYO.

LEAVE A COMMENT