MAANA, TAZAMA, MIMI NAUMBA MBINGU MPYA NA NCHI MPYA.

  Biblia kwa kina, Uncategorized

Jina Kuu lipitalo majina yote la Mwokozi wetu Yesu Kristo lihimidiwe milele. Karibu katika kujifunza neno la Mungu.

Ukisoma maandiko utagundua kuwa, wakati Mungu anaumba dunia, kusudi lake au mlengwa mkubwa aliyekusudiwa  na Mungu alikuwa ni mtu, na ndio maana baada ya Mungu kuumba kila kitu akamuumba mtu, mke na mume na kumwambia waende wakazaliane na  kuvitiisha vitu vyote vya angani, baharini na nchi kavu (Mwanzo 1:28)

Lakini miaka mimgi mbeleni, maneno ya Mungu yanabadilka na kusema hivi.

Isaya 65:17  MAANA, TAZAMA, MIMI NAUMBA MBINGU MPYA NA NCHI MPYA, na mambo ya kwanza hayatakumbukwa, wala hayataingia moyoni. 

Sasa unaweza kujiuliza kwanini Mungu aseme hivyo? Jibu ni kuwa, Mungu hakukusudia kumuumba mtu ili atende dhambi, lile tendo la Adamu kufanya dhambi pale bustani ya Edeni lilibadili kabisa mpango wa Mungu kwa wakati ule, na dhambi ikaingia duniani hadi sasa na kuifanya dunia hii kuwa mbovu. Lakini Mungu mpango wa wake ni ulele wa kuifanya dunia hii kuwa mahali salama, na ndio maana sasa, akasema kuwa, anaumba mbingu mpya na nchi mpya.

Sasa kama tulivyojifunza kwamba, Mungu alipoumba dunia, alimkisudia mtu akaishi humo, hivyo basi, hata hii mbingu mpya na nchi mpya itakayokuja, Mungu bado anamkusudia mtu akaishi humo, sasa ili tujue ni watu gani au ni mtu gani atakayeishi humo katika nchi mpya, hatuna budi kufahamu kuwa, Mungu alifanya nini kabla ya mtu kuishi katika dunia hii mbovu ya sasa, hebu tusome. 

Mwanzo 1:3  MUNGU AKASEMA, IWE NURU; IKAWA NURU. 

Unaona? Kabla ya mtu kuishi katika dunia hii mbovu ya sasa iliyoumbwa na Mungu, Mungu alitamka kwanza “IWE NURU” kumaanisha kuwa, wakati huo dunia ilikuwa ni giza (Mwanzo 1:2) vivyo hivyo pia katika mbingu mpya na nchi mpya ambayo Mungu anaiumba, Mungu anatamka “IWE NURU” kumaanisha kuwa, duniani sasa hivi ni giza, na giza hili ni matendo  maovu yaliyopo sasa.

Yohana 3:19  Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu. 

Na nuru inayozungumziwa hapo ni YESU KRISTO, (Yohana 9:5) yeye ndiye nuru ya hii dunia na ulimwengu kwa ujumla, yeye alikufa ili atuokoe na dunia hii mbovu ya sasa iliyojawa giza na kumpokea yeye Nuru katika maisha yetu ili tuwemo katika ile mbingu mpya na nchi mpya.

Wagalatia 1:4  ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili ya dhambi zetu, Ili ATUOKOE NA DUNIA HII MBOVU ILIYOPO SASA, kama alivyopenda Mungu, Baba yetu.

Ndugu yangu, ili uwepo katika ile mbingu mpya Na nchi mpya, huda budi kuwa na nuru ndani yako, kwani pasipo hiyo utakuwa gizani na mwisho kuikosa mbingu mpya na nchi mpya. Mungu anapenda watu wote leo hii waikubari hii nuru katika maisha yao, anataka nuru hii ingaze ndani yao ili waweze kuishi katika mbingu mpya na nchi mpya.

Sasa unaweza jiuliza, naipataje hii nuru ili nistahili kuwepo katika mbingu mpya na nchi mpya? Jibu ni rahisi sana. Tubu dhambi zako zote kwa kumaanisha kabisa kuziacha katika maisha yako, kama ulikuwa ni mlevi unaacha pombe, kama ni mzinzi unaacha, kama ni mla rushwa unaacha, kama ni msema uongo na mtukanaji unaacha, kama ni mtazamaji wa picha ngono unaacha, kama ni mfanyaji masturbration unaacha, kama ulikuwa unaabudu masanamu na kuwaomba wafu unaacha, miziki ya kidunia inayosambaza ufalme wa giza wa bangi, pombe, uzinzi na uasherati unaacha. Unaacha kuvaa vimini na masuruali kwa wanawake, unaacha kuvaa mavazi yanayoonesha maungo ya mwili wako, unaacha kuvaa nywele bandia, makucha bandia, makeup, unaacha sigara, n.k kisha unamkiri BWANA YESU kwa kinywa chako kuwa ni Bwana na mwokozi wa maisha yako na kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi ambao ni wa maji mengi na kwa jina la Yesu kulingana na matendo 10:48 na matendo 19:5 na kupokea kipawa cha Roho mtakatifu ndani yako atakayekuwezesha kuishi maisha ya utakatifu kama yeye alivyo.

Ufunuo 21:1  Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena.

 2 Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.

 3 Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao. 

4 Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita. 

5 Na yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi akasema, Tazama, nayafanya yote kuwa mapya. Akaniambia, Andika ya kwamba maneno hayo ni amini na kweli. 

Tafadhari, washirikishe na wengine habari hii njema.

Bwana akubariki, Shalom.


MADA ZINGINEZO

Biblia imeruhusu ubatizo wa vichanga? (kulingana na matendo 16:33)


Je! Nikiwa naona maono si ndo basi Roho mtakatifu ninaye hivyo sina haja ya ubatizo?


Je ubatizo sahihi ni kwa jina la Yesu au Baba, Mwana na Roho Mtakatifu?

LEAVE A COMMENT